5 minCODE 01, MAREKANI#
CODE 01, MAREKANI# Zama zote za mwanadamu, katika falme zote zilizowahi kupita, Tamaa kubwa ya wenye Nguvu kat
Inapakia...


✦ Maarifa, Imani, Huduma ✦
MUUNGANIKO WA MAARIFA NA IMANI
Tunachapisha na kukuza maarifa ya kisayansi yanayofikika, yaliyojengwa juu ya maadili—tukiunga mkono afya, elimu na ustahimilivu wa jamii.
Sokoine University of Agriculture, Morogoro

Tangu 2020
Injili ya Sayansi
Tunachapisha na kukuza maarifa ya kisayansi yanayofikika, yaliyojengwa juu ya maadili—tukiunga mkono afya, elimu na ustahimilivu wa jamii.
Tunaunganisha maarifa, imani na huduma
Falsafa ya Elimu
Injili ya sayansi imejikita kutoa masomo mbalimbali kivitendo kuhusiana na Elimu ya kweli na Malezi. Katika Kitengo cha Elimu na Malezi; Injili ya sayansi inashirikiana na wasomi mbalimbali wenye motisha ya kusaidia jamii zao kwa kutoa Elimu bora nje na mfumo tegemezi wa elimu. Malengo ya injili ya sayansi ni kutengeneza kizazi ambacho kitakuwa na Elimu ya kujitegemea.
Uchambuzi wa kina unaounganisha sayansi, imani, na maisha ya kila siku.
Utafiti wa kisasa kuhusu biolojia, fizikia na kemikali inayobadilisha ulimwengu.
Uhusiano wa kina kati ya imani ya kidini na elimu ya kisayansi ya uumbaji.
Maarifa ya kina kuhusu ulimwengu, galaksi na siri za uumbaji wa Mungu.
DNA, protini na misingi ya kisayansi ya uhai ndani ya kila chembe ya mwili.
Uwajibikaji wa kimaadili katika tafiti na matumizi ya teknolojia ya kisasa.
Kugundua uzuri na utata wa viumbe na mazingira kama ishara ya Muumba.
Watu wanaoendesha Injili ya Sayansi
MwanzilishiDr. Brighton G. Shoo
Mwanzilishi & Mwenyekiti
Tiba ya Wanyama, Sayansi za Ubongo, Tiba Asili
Ni daktari wa wanyama toka Chuo Kikuu cha Sua, Morogoro. Muda wake mwingi zaidi amejikita katika kusoma, kufuatilia, na kutafiti sayansi za Ubongo, Biofizikia, na Historia za jamii za watu, na sayansi za watu 'Anthropolojia'. Ameandika Mjumuisho wa Vitabu 'Compendium' ya Ubongo wa Mtu mweusi yenye sehemu 5 'Volumes', ameandika Vitabu vingine vinavyohusu tiba ya mwili kupitia asili, Sayansi ya Uumbaji, Afrika haihitaji serikali, na Madhara ya Teknolojia na Vyakula vya kisasa'. Masomo yake pia hupatikana bure kupitia Blog za injili ya sayansi, vipindi vya Redioni, na Mitandao kadhaa ya kijamii. Kwa sasa ni Mwenyekiti wa Injili ya sayansi.
KatibuWyclife Tuarira
Katibu Mkuu
Elimu ya Sayansi, Fizikia na Kemia
Ni Mhitimu wa Shahada ya Sayansi na Elimu toka Chuo Kikuu cha UDISM DUCE, Tanzania. Mwalimu Wyclife ni Mdadisi na mwenye shauku Mahususi katika sayansi za Fizikia na Kemia. Wyclife anapenda kufundisha, kukuza mapenzi ya sayansi kwa wanafunzi, na pia kuandika vitabu vya afya na dini kama mwandishi na mwanzilishi wa Wiki eBooks Publishers. Kupitia msingi wake imara katika masomo ya sayansi, pamoja na Mapenzi yake makubwa katika Hekima za Vitabu vya Mithali, Zaburi, na Mhubiri, Amejitolea kuunda mazingira ya ujifunzaji yenye mvuto na ufanisi mkubwa, huku akiendelea kuboresha ujuzi wake na wa jamii yake kitaaluma. Yuko tayari kuchangia katika taasisi za elimu kama mwalimu mwenye motisha na anayejibadilisha kulingana na mazingira. Kwa sasa Mwl Wycliffe ni Katibu mkuu wa Injili ya Sayansi.
MhaziniGamba G. Manyama
Mhazini
Afya ya Jamii, Bioteknolojia
Ni mtafiti wa kina na mwandishi anayependa uchunguzi wa maswali magumu ya kifalsafa ya maisha kupitia sayansi, akili, na tafakuri binafsi. Ni msomi wa Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Afya ya Jamii (Msc. Public Health Pest Management), na pia ana Shahada ya Kwanza (BSc) katika Bioteknolojia na Sayansi ya Maabara kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine, SUA, Morogoro Tanzania. Gamba amejikita sana kupambanua ufahamu wa kitaalamu na udadisi mkubwa kuhusu imani ya binadamu na uzoefu. Muda wote wa nje na kazi zake za kiofisi hupenda kuhariri vitabu na rasimu mbalimbali ili kusaidia watu wengine kudadavua hoja nzito kwa urahisi na uwazi zaidi. Kitabu chake cha A MAN WITH NO RELIGION ni safari yake ndefu ya kimawazo katika Kiini cha Imani, utambuzi binafsi, na kile kinachoitwa ukweli katika Ulimwengu wa uhalisia. Kwa sasa Gamba Manyama ni Mhazini wa Injili ya sayansi.
Injili ya sayansi inalenga kutengeneza kizazi ambacho kitakuwa na Elimu ya kujitegemea.
Dhana ya Elimu
Injili ya sayansi imejikita kutoa masomo mbalimbali kivitendo kuhusiana na Elimu ya kweli na Malezi. Katika Kitengo cha Elimu na Malezi; Injili ya sayansi inashirikiana na wasomi mbalimbali wenye motisha ya kusaidia jamii zao kwa kutoa Elimu bora nje na mfumo tegemezi wa elimu. Malengo ya injili ya sayansi ni kutengeneza kizazi ambacho kitakuwa na Elimu ya kujitegemea.
Makao Makuu
Injili ya sayansi ina matawi yake ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali, huku Shule ya Sekondari ya Mzumbe, Morogoro, ikiwa Makao makuu kwa Shule zote. Tofauti na mfumo uliopo ambao waliojuu ndiyo wanapaswa kufikiria nini cha kuwafundisha waliochini, Injili ya sayansi inalenga waliochini kujua nini wanahitaji kufundishwa, kusoma, au kujisomea.
kuuliza maswali kuhusu kila aina ya imani, au misimamo iliyojengeka katika sayansi, falsafa, au mafundisho ya kidini kwa kutumia fikra huru na za msingi.
Kukuza hamu ya maarifa, na kuondoa hofu ya kukutana na hoja tofauti au za upinzani juu ya taarifa yoyote.
Tunategemea wanafunzi Kusoma kwa makini vitabu, kazi za kisayansi, maandiko ya kifalsafa, na dhana za kiteolojia zinazopendekezwa na Injili ya Sayansi.
ili Kujenga uwezo wa kimwili na kiakili wa kuhimili na kutawala mazingira katika nyanja za kisayansi, kijamii, kidini na kiuchumi.
na kuwa na uwezo wa kuzalisha mawazo mapya, Kujenga taswira, na kutengeneza mikakati ya kuendeleza maendeleo ya kisayansi ya Afrika.
Malengo makuu ya uongozi na kikundi yanayotuelekeza katika kutekeleza dira yetu.
Malengo na mipango ya viongozi wakuu wa Injili ya Sayansi katika kuendesha taasisi.
Malengo na mipango ya Timu ya Injili ya Sayansi katika kufanikisha shughuli zake.
Nguzo tatu zinazounga mkono maendeleo ya jamii kupitia Injili ya Sayansi.
Huduma mbalimbali tunazotoa ili kukuza maarifa na ustawi wa jamii kwa ujumla.
Tunasaidia watu binafsi na jamii kupitia ushauri wa kisayansi na kitaalamu katika maeneo mbalimbali ya maisha na afya.
Tunachapisha vitabu, makala na nyaraka za kisayansi zinazoweza kufikiwa na watu wa rika na tabaka zote.
Tunaandaa mafunzo, semina na warsha zinazolenga kuelimisha jamii kuhusu maswala ya kisayansi na kimaadili.
Tunashirikiana na vyombo vya habari kutoa maudhui ya elimu na uhamasishaji kwa njia mbalimbali za mawasiliano.
Tengeneza makala, video na maudhui ya kidijitali yanayoeneza maarifa ya kisayansi kwa watu wote mtandaoni.
Jiunge na familia ya Injili ya Sayansi na ufurahie manufaa yaliyoandaliwa maalum kwako.
Kadi rasmi ya utambulisho inayokuwa mwakilishi wa Injili ya Sayansi.
Vyeti vya kukamilisha mafunzo vinavyotambulika kitaaluma.
Unganika na wasomi na wataalamu kutoka pembe zote nchini.
Fursa za kukua kitaaluma kupitia mafunzo na semina maalum.
Tuandikie ujumbe kupitia WhatsApp. Timu yetu iko tayari kukusaidia haraka.
Wasiliana kupitia WhatsAppWanafunzi wanaweza kutembelea vituo vya utafiti na mashirika yanayoshirikiana na Injili ya Sayansi.
Ziara zinazolenga kugundua sayansi ya vitendo kupitia maabara na mifumo halisi ya asili.
Fursa za kukutana na wataalamu na kujifunza moja kwa moja kutoka kwao kuhusu sayansi ya uumbaji.
Injili ya Sayansi inashirikiana na taasisi mbalimbali za elimu, utafiti na jamii ili kufikisha maarifa ya kisayansi kwa watu wengi zaidi nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla.
5 minCODE 01, MAREKANI# Zama zote za mwanadamu, katika falme zote zilizowahi kupita, Tamaa kubwa ya wenye Nguvu kat
13 minWanavyologa Wachawi ‘’Magical Causality’’ Hili huwa ni miongoni mwa maswali makubwa sana ambayo watu hutamani
5 minyaliyomo Neno la Awali.............................................................................. 3 NYAMA..
10 minMACHO NA LUSIFA Utangulizi Kama nilivyoeleza awali kabisa, watu wengi wanahisi ulimi ndicho kitu ambacho kinaw
6 minLUSIFA DHIDI YA ULIMI Kama Nyoka Lusifa anatambua kwa kuchochea sana sensa za hisia za utamu wa protini kama n
10 minLUSIFA DHIDI YA NGOZI Kama Nyoka Ngozi ni mlango wa fahamu ambao lusifa huutumia sana, pengine kuliko wengi wa
Maarifa ni nuru, na nuru haliachi giza kamwe.
— INJILI YA SAYANSI