Inapakia...
Inapakia...
Tunajenga jamii yenye uwezo wa kuelewa afya yake, kujikinga na magonjwa, na kuishi kwa misingi ya sayansi, ukweli, na uwajibikaji binafsi.
Kupunguza utegemezi wa mfumo wa magonjwa sugu.
Wataalamu wa Afya
Nguzo za Mfumo
Mada kutoka PDF
Malengo ya Hatua Tatu
Injili ya Sayansi inalenga kujenga uwezo wa mtu kujitegemea kiafya, badala ya kubaki mtegemezi wa mfumo wa matibabu wa kudumu maisha yote. Takwimu za magonjwa sugu zinaonyesha hitaji la mwelekeo mpya: kinga, lishe bora, mazoezi, na maarifa ya kina yanayompa mtu mamlaka juu ya afya yake.
Tunakubali sayansi za kitabibu zilizopo, lakini tunasisitiza maono ya kutengeneza jamii ya watu wanaoweza kufanya maamuzi bora ya afya kila siku.
Wataalamu wa afya ndani ya Injili ya Sayansi wanaongoza elimu, uandishi, semina, na vipindi vya afya ili jamii ipate mwongozo unaotekelezeka kwa vitendo.
Tunafuata ushahidi wa kisayansi ili kuhakikisha kila mwelekeo wa afya una msingi imara na unaweza kuaminika na jamii nzima.
Soma zaidiKupitia semina, blogu, na vipindi vya afya, tunafikia jamii ili kuwapa ujuzi wa kujikinga na magonjwa na kuishi vizuri.
Soma zaidiMfumo wa Injili ya Sayansi unachanganya tiba ya kliniki kwa dharura, kinga ya magonjwa, na tiba asilia inayoongozwa na utafiti.
Tunatumia huduma za hospitali kwa hali tata na dharura, huku tukiwaunganisha watu na wataalamu wa afya wenye weledi na moyo wa kuhudumu.
Tunafundisha kinga dhidi ya magonjwa sugu kupitia lishe, mazoezi, miongozo ya afya ya jamii, na ufuatiliaji wa ushahidi wa kisayansi.
Tunathamini tiba asilia zenye historia ya kusaidia jamii, huku tukizichambua kwa msingi wa sayansi ili kupunguza utegemezi usio wa lazima wa dawa.
Sehemu hii inajumuisha maudhui ya kila ukurasa wa hati ya Afya na Sayansi kwa upana zaidi ili data yote ya PDF itumike moja kwa moja ndani ya ukurasa huu.
Injili ya Sayansi ina sera ya KUJITEGEMEA KIAFYA.
Maono ya Injili ya Sayansi katika afya na Sayansi zake ni kuwezesha Wajumbe wake wote kuwa na uwezo wa kujitegemea kiafya, bila kuwa na utegemezi kwa mfumo wa madawa ya hospitalini, au kuwa wahanga wa tiba za kienyeji.
Takwimu zinaonyesha ongezeko kubwa sana la magonjwa yasiyo ya kuambukiza, au magonjwa sugu.
Magonjwa haya yote hayatibiki, ni magonjwa ambayo huwafanya wagonjwa kuwa wategemezi wa mfumo wa afya kwa maisha yao yote mpaka kufa kwao.
Kipindi magonjwa sugu yakizidi kuongezeka, bado idadi ya watu wenye shida za kiakili na IQ ndogo inazidi kuongezeka.
Hii inadhihirisha uwezo wa watu kuweza kutatua shida hizi nao unazidi kupungua.
Injili ya Sayansi inatumia mfumo wa tiba kliniki, au "conventional medicine", kama namna pekee ya kusaidia wagonjwa walio katika hali tata "acute problems".
Na hili inalifanikisha kupitia hamasa toka kwa Madaktari Wajumbe ambao ni watumishi katika hospitali za Umma "public hospitals".
Pichani ni Daktari "MD" Daniel Kateshi kulia, na Clinical Officer Paalay Kasaine kushoto.
Pichani ni Daktari "MD" Sylvester Shinyanga, ni mjumbe na Mtaalamu mwenye upendo mkubwa sana wa kusaidia jamii katika Injili ya Sayansi.
Injili ya Sayansi inaamini katika Maarifa mapana ya Sayansi za matibabu kupitia mifumo ya afya iliyopo, lakini inaamini mifumo iliyopo haina maono ya kutengeneza jamii ya watu watakaokuwa na uwezo wa kujitegemea.
Na kwa kulitambua hili, inatumia taaluma ya Wataalamu waliopo kutengeneza msingi wa Maarifa ya Afya ya kujitegemea.
Katika Injili ya Sayansi kuna Wataalamu mbalimbali wa afya za jamii, Madaktari, walimu, Wana taaluma wa huduma za Afya, n.k.
Mfano mzuri ni namna Kinga dhidi ya vichochea vya Ugonjwa wa Kisukari imeonekana kuwezesha mafanikio makubwa sana katika kuwasaidia wagonjwa kuliko tiba.
Injili ya Sayansi imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha mfumo Kinga kupitia hamasa mbalimbali.
Mfano; Mfumo Bora wa utendaji kazi na Mazoezi.
Injili ya Sayansi inahamasisha matumizi ya viungo kwa kadri iwezekanavyo, ukaribu na asili kadri iwezekanavyo, na inahamasisha kiasi katika kila lifanywalo.
Pichani ni Wajumbe wa Injili ya Sayansi katika mazingira ya asili na Kilimo, Arusha vijijini.
Injili ya Sayansi inatoa masomo mbalimbali kupitia namna za kufanya mazoezi hasa zaidi kupitia kazi ambazo watu wamekuwa wakizifanya.
Injili ya Sayansi haina falsafa kamili ya ulaji, na inakinzana na falsafa yoyote ile ya ulaji ambayo haina misingi ya ukweli, haki, historia, na Sayansi.
Injili ya Sayansi inashirikiana na wanahamasa wote wa falsafa ya ulaji wanaodidimiza matumizi ya bidhaa za kisasa "processed foods", matumizi yaliyokithiri ya sukari na mafuta ya mbegu.
Ulaji usio na staha wala kujali haki za wanyama, madawa ya mimea, na hatari za mabadiliko ya kijenetikia pia umetajwa kwenye sehemu hii.
Dr Brighton Shoo ameandika kitabu kinachochambua kwa kina Sayansi, historia, na ukweli kuhusu sera nyuma za ulaji na uhalisia wake.
Injili ya Sayansi haipuuzi tiba asilia ambazo zimekuwa msaada wa karne nyingi sana kwa Waafrika.
Inachofanya ni kutanua kwa mapana zaidi uelewa nyuma ya tiba hizi.
Imani yetu kubwa ni kuwa, tunaweza kusaidia kupunguza utegemezi wa madawa ya hospitalini ambayo yamezidi kuongeza hatari ya usugu wa vimelea kwa kutumia dawa asilia.
Tunaamini kwa matumizi ya dawa asilia kadhaa ambazo nyingi kati yake tayari huwa ni vyakula, au virutubisho kwa mwili, tunaweza kupunguza utegemezi wa madawa ya hospitalini.
Injili ya Sayansi inashirikiana na Wataalamu wa tiba asilia wenye msingi mpana wa Sayansi za Afya, na Wataalamu wasio na msingi mpana.
Kushoto ni Daktari "DVM" Magesa Matiku, kulia ni Mtaalamu wa Maabara na mzamili wa afya ya jamii, Gamba Manyama.
Malengo yetu ya awali katika mfumo wa kujitegemea wa afya ni kufikia watu kupitia mitandao ya kijamii kwa elimu kuhusiana na afya.
Mpaka sasa Wataalamu kadhaa wa injili ya Sayansi akiwemo Dr Shoo wamekuwa mstari wa mbele katika hili.
Hasa kupitia vipindi vya afya ambavyo amekuwa akitoa katika "Adventist World Radio".
Hatua ya pili ya Injili ya Sayansi katika afya ni kutengeneza kituo maalumu ambacho kitahusisha kutoa mwongozo wa huduma za afya ya kujitegemea.
Kituo hiki hakitakuwa hospitali wala kliniki, kwa kuwa hakuna umuhimu wa kutoa huduma zinazoweza patikana vizuri zaidi katika taasisi kubwa za huduma za afya za kitaifa na binafsi.
Kituo hiki kitatoa msaada wa huduma za kusapoti wagonjwa kama; supplements, vifaa na sample za vyakula vya kuchochea kinga, protocol za kujikinga na magonjwa mbalimbali, miongozo ya vyakula, miongozo ya mazoezi, na miongozo ya huduma baada ya upasuaji na matibabu ya hospitali.
Kituo hiki kitakuwa ni aina ya "Regenerative, preventive, alternative, and anti-aging center" na kitahusisha mwongozo wa Wataalamu wa afya tokea taasisi mbalimbali za afya.
Hatua ya tatu ya malengo ya Injili ya Sayansi katika afya ya kujitegemea, itahusisha mwongozo wa maisha ya vijijini, maisha ya kiasili, na kujikita katika mfumo wa kilimo cha asili.
Kuelekea Malengo Yetu: Injili ya Sayansi inaelekea malengo yake kupitia utayari wa Wajumbe wake kujitoa na kujitolea kusaidia jamii zao kwa huduma za afya.
Huduma hizi zimekuwa zikitolewa tangia mwaka 2024, kupitia masomo ya afya na miongozo yote ya afya bure kabisa kupitia blog za mitandaoni na mitandao ya kijamii.
Wajumbe wengi wana taaluma za afya ambazo wamekuwa wakizitumia kuandika nakala, vitabu, na kutoa semina.
Injili ya Sayansi ina mkakati wa kujenga kituo cha afya ya kujitegemea kupitia michango ya Wajumbe, na mpaka sasa tayari wameweza kufanikisha kupata kiwanja kwa Wajumbe waliojitolea eneo.
Mkakati wa kujenga utaanza rasmi Wajumbe watakapoweza kufanikisha uwezo kamili wa kuanza kujenga.
Injili ya Sayansi inahamasisha na kuomba wote wenye uwezo wa kusaidia malengo haya kusapoti kupitia michango yao hiari, au hata msaada wowote ule katika kuwezesha kazi hii.
Muhtasari wa msisitizo wa maudhui, hatua za utekelezaji, ufunikaji, na marudio ya maneno muhimu.
Kiwango cha msisitizo (1-5) kwa kila sehemu kuu ya hati
Maendeleo ya utekelezaji kwa kila hatua
Mara maneno muhimu yanajirudia katika hati nzima
Idadi ya vichwa vya habari kwa kila ukurasa (0-8)
Kadiri ya maneno kwa kila ukurasa (0-120)
Kufikia watu kupitia mitandao ya kijamii, blogu, semina, na vipindi vya afya kama njia ya kutoa maarifa ya kujikinga na kuboresha maisha.
Kituo kitakachotoa ushauri wa protocol, lishe, mazoezi, huduma baada ya matibabu, supplements, na mwongozo wa kinga bila kuwa hospitali kamili.
Kuimarisha mwongozo wa maisha ya vijijini, ukaribu na asili, na kilimo cha asili kama msingi wa afya ya kujitegemea.
Timu ya wataalamu yenye uzoefu na maarifa inayoongoza elimu ya afya katika Injili ya Sayansi.

Mtafiti wa Sayansi za Ubongo na Tiba Asilia

Tiba ya Kliniki na Matibabu ya Jumla

Mwanzilishi wa PUANAY

Tiba ya Ndani ya Mwili, Kinga na Upasuaji Mdogo

Tiba ya Wanyama, Utafiti wa Kisayansi

Afya ya Jamii na Uchambuzi wa Maabara
Kuelekea malengo yetu kupitia utayari wa Wajumbe wetu kujitoa na kujitolea kusaidia jamii.
Huduma hizi zimekuwa zikitolewa tangia mwaka 2024, kupitia masomo ya afya na miongozo yote ya afya bure kabisa kupitia blog za mitandaoni na mitandao ya kijamii.
Wajumbe wengi wana taaluma za afya ambazo wamekuwa wakizitumia kuandika nakala, vitabu, na kutoa semina.
Injili ya Sayansi ina mkakati wa kujenga kituo cha afya ya kujitegemea kupitia michango ya Wajumbe, na mpaka sasa tayari wameweza kufanikisha kupata kiwanja kwa Wajumbe waliojitolea eneo.
Kazi hii inaendelea kupitia kujitoa kwa wajumbe, maarifa ya wataalamu, na ushirikiano wa jamii. Tunakaribisha mchango wa mawazo, muda, na rasilimali.