Inapakia...
Inapakia...
Urejeshaji wa Mazingira kwa Maisha ya Asili
Kurejesha mazingira katika hali yake ya asili ya Edeni.
Maeneo ya Utaalamu
Changamoto
Mbinu za Kazi
Mtaalamu Mkuu
Injili ya Sayansi inajali sana afya ya mazingira, na hasa afya ya mazao, na mazingira ambayo yanazunguka makazi ya watu.
Sera kubwa ya Injili ya Sayansi ni kupiga vita namna zote za kuathiri mazingira, na kuwarejesha binadamu katika makazi yao ya asili mpaka sasa.
Tunafanikiwa katika kukamilisha malengo haya kupitia uwepo wa wataalamu wengi sana wa kilimo, toka Chuo Kikuu cha SUA Tanzania, ambao ni wanachama wake.
Wataalamu wa kilimo na mazingira kutoka Chuo Kikuu cha SUA wanaongoza juhudi za kurejesha mazingira na kuhamasisha kilimo endelevu katika jamii zetu.
Chuo Kikuu cha SUA
Sokoine University of Agriculture
Wataalamu wa kilimo na mazingira kutoka Chuo Kikuu cha SUA
Wataalam wa BSc Horticulture wanaolenga afya ya mbogamboga na matunda kwa uzalishaji bora.
Soma ZaidiWanasayansi wa BSc Agricultural General wanaotoa mwongozo kamili wa kilimo na ufugaji.
Soma ZaidiWataalamu wa Agricultural Extension wanaowaunganisha wakulima na maarifa ya kisasa.
Soma ZaidiHawa wote kwa pamoja ukijumlisha na wakulima wasiosomea wanadhumuni moja kubwa zaidi — mazingira safi na kilimo endelevu.
Kupambana na tatizo la uharibifu wa mazingira
Kushughulikia madhara ya matumizi ya madawa ya magugu kwa mimea, ambayo huathiri ubora wa vyakula na afya ya binadamu.
Kuelimisha kuhusu madhara ya kutumia mbolea za kisasa bila maarifa mapana ya athari zake kwa mimea na mazingira.
Kupiga vita namna zote za kuathiri mazingira na kukuza mbinu endelevu za kilimo na uhifadhi.
Injili ya Sayansi huwatumia wasomi walio wanachama wake kufahamishana namna sahihi za kilimo. Uwepo wa wataalamu wengi na wa fani mbalimbali husaidia hata utambuzi wa madhara unavyoweza leta shida katika ubora wa vyakula, afya ya vimelea, afya ya wanyama, na hatimaye afya ya binadamu.
Elimu ya mbinu sahihi za kilimo endelevu
Ushauri wa kitaalamu juu ya afya ya mimea
Mafunzo ya uhifadhi wa mazingira
Semina za kutatua changamoto za kilimo
Uhamasishaji wa kilimo hai (organic farming)
Wataalam wanaojitokeza kwa kilimo endelevu

BSc Applied Agriculture — SUA Tanzania
Edson Iskari Kanolo ni mkulima kweli. Amezaliwa katika familia ya wakulima. Baada ya elimu yake ya sekondari akajiunga na Chuo 'Ministry of Agriculture Training Institute Inyala Mbeya', ambapo akahitimu katika kilimo 'Certificate in General Agriculture'.
Baada ya hapo akaendeleza Diploma katika Chuo 'Ministry of Agriculture Training Institute Ukiriguru Mwanza', ambapo akahitimu tena katika kilimo 'Diploma in General Agriculture'. Kanolo hakuishia hapo, akaendelea hata hatua ya juu kabisa ya shahada toka Chuo Kikuu cha Sokoine, SUA, ambapo akaendelea hata kuhitimu katika shahada ya kilimo 'BSc Applied Agriculture'.
Mkulima Kanolo ni mwanachama hai wa Injili ya Sayansi, na kutokana na motisha yake kubwa kwa jamii kama ilivyo sera ya Injili ya Sayansi, ameandika kitabu kinachoitwa 'Kilimo Bora Ni Bustani kama Edeni'. Katika kitabu chake Kanolo ameelezea mbinu zote za msingi mkulima anazopaswa kuzizingatia ili kuwa na mafanikio makubwa katika kilimo, na kuepukana na hatari za mbinu hatarishi za kilimo.
Kanolo ni mhamasishaji mkubwa zaidi wa afya ya mimea katika familia ya Injili ya Sayansi.
Misingi ya msingi tunayojenga juu ya kilimo endelevu
Kutumia mbegu za asili zilizopo bila mabadiliko ya kijenetiki. Tunasadiki kuwa mazingira yameumbwa kwa hikima na kila mmea una nafasi yake maalum.
Kutumia njia za asili za kudhibiti magugu na wadudu badala ya kemikali hatari zinazoathiri afya ya binadamu na mazingira.
Kulinda udongo, maji, na hewa kwa kuzingatia mbinu za kilimo zisizoathiri mifumo ya asili ya mazingira.
Kuhamasisha jamii kuzalisha mazao yanayotosheleza mahitaji yao na kuuza surplus badala ya kutegemea msaada wa nje.
Vyakula vyenye lishe kamili bila mabaki ya kemikali
Udongo na maji safi kwa vizazi vijavyo
Kipato cha daima kwa familia za wakulima
Kufuga kwa heshima na kuzingatia ustawi wa wanyama
Jiunge nasi katika safari ya kurejesha mazingira yetu. Pata mwongozo wa kitaalamu, elimu, na rasilimali za kilimo endelevu.