Inapakia...
Inapakia...

Dr Brighton Shoo
Mwandishi na Mwenyekiti
“Historia Katika Vita Ya Kula Mimea Ulaji wa Mimea, mbogamboga, na matunda ni mtazamo imara zaidi wa vyakula uliokubalika kwa karne sasa, kwa kupewa uzito mkubwa sana na mtazamo wa Biblia ‘’Mw1:29’’, k…”
Historia Katika Vita Ya Kula Mimea
Ulaji wa Mimea, mbogamboga, na matunda ni mtazamo imara zaidi wa vyakula uliokubalika kwa karne sasa, kwa kupewa uzito mkubwa sana na mtazamo wa Biblia ‘’Mw1:29’’, kuwa Mungu alitoa kila mmea utoao mbegu, na kila mti ambao matunda yake yanatoa mbegu, kuwa chakula, si cha binadamu tu, bali viumbe wote kuanzia wadudu, mpaka Wanyama. Mtazamo huu ulibadilika ghafla tu baada ya dhambi, ambapo ukawa mwanzo wa kuvunjika kwake hasa baada ya viumbe wengine kama simba kuanza kula Wanyama wenzao. wadudu, bakteria, fangasi, nao wote wakaanza kula mizoga, na hata Mimea ambayo haikuwa ikifa nayo ikaanza kufa. Hakuna anayejua maisha yalikuwaje kabla ya dhambi, hakuna anayejua Mimea iliteteaje mbegu zake zisiliwe zote zikamaliza uzao wake, wala hakuna anayejua ikolojia ya ulimwengu ilijibalansije viumbe wote wakila nyasi kuanzia nzige, nyumbu, simba, mpaka binadamu.
Kwa kuwa wakristo wote wana ndoto za kurejea Edeni, ambapo hakuna mateso tena, basi wengi huamini sana katika mfumo wa ulaji wa mimea tu, kama namna ya kuirejesha hali yao ya utauwa uliopotea. Lakini kwa upande wa biolojia mitazamo hii huwa haina nguvu kabisa, na sababu kubwa ni kuwa; hata Mimea ina haki na inaonyesha kupambania uhai wake kama tutakavyoona. Kilimo cha Mimea kinahusisha kuangamiza sana wadudu kupitia madawa ya wadudu ‘’pesticides’’, je wadudu wana haki ya kufa? Asili yote imejaa kuua ili kuishi, kama Simba, Mamba, Nyoka, na Chui wasipoua Wanyama wala nyasi, basi dunia isingedumu kwa kukosa kabisa uoto, na viumbe wote wangekufa. Kama hutaua Bakteria kwa antibiotics mwilini mwako, watakuua ghafla. Mtazamo wa kuelekea utauwa kwa kutoua wenda usingeleta mantiki kabisa kwa Kristo mwenyewe aliyekufa ili kuokoa. Na haishangazi hata Yesu alikula Samaki baada ya Kufufuka, na hata alilisha watu elfu tano Samaki na mikate. Kuna Maana pana zaidi ya Mithali 12:10 kuwa ‘’Mwenye haki huufikiri uhai wa mnyama wake, bali huruma za mtu mwovu ni ukatili’. Ni kweli Kuku wana haki ya kuonewa huruma, lakini je, umejali maisha ya binadamu kwa kiwango cha kuujali uhai wa kuku? Wengi ni wanafiki, au wajinga.
Kwa upande wa wanabiolojia kama tulivyoona awali, kwao binadamu ni mnyama mla nyama ‘’carnivore’’ aliyejifunza kula mimea. Kwao binadamu ni kama simba zaidi ya kama ng’ombe. Tumbo la binadamu lina asidi kali sana, pH ya 1-2, ambayo huua bakteria maelfu, na halina vivunjaji ‘’enzymes’’ vya wanga, huvunja zaidi Protini kwa kuwa na vivunjaji kama ‘’Pepsin’’ ambavyo humaanisha lipo vizuri zaidi kuvunja nyama. Uvunjaji wa Mimea huitaji sana Kiwango kikubwa cha Vimelea wa tumboni ‘’hasa Bakteria’’ ambao huvunja sana kambakamba ngumu za Mimea kama ‘’Cellulose’’, kwa kuzivundisha, na Tumbo la Wanyama wala Mimea ‘’ruminants’’ huwa na chemba 4, ambapo kubwa zaidi huitwa ‘’Rumen’’, hili hushamiri mamilioni ya bakteria ambao huvunja nyasi aina mbalimbali, na ng’ombe hucheua ‘’regurgitate’’ na kuendeleza kumeng’enya zaidi nyasi hizi, na baadaye ndipo huenda sasa kwenye tumbo kama la Wanyama ‘’abomasum’’ ambapo hapo hufyonza virutubisho hivyo, hasa ‘’Short chain fatty acids’’.
Kwao Binadamu ana vimelea kidogo sana wa kumsaidia kuvunja kambakamba hizi za mimea ‘’fibers’’, ambao huwa katika utumbo mkubwa ‘’colon’’ lakini sehemu ndogo sana. Na kwa kuwa binadamu sehemu hii ipo mwishoni, sio mwanzoni kama ‘Rumen’’ ilivyo kwa wala mimea, basi ni Dhahiri kwao kuwa binadamu haitaji mimea ambayo asilimia kubwa huwa ni wanga ‘’Polysaccharides’’. Kwa kuwa binadamu asilimia 50% ni protini, 40% ni mafuta, na kumi tu ndiyo madini, na wanga, basi uwepo wa asilimia 90% ya wanga katika mimea kwao humaanisha binadamu haitaji kula Mimea.
Kwao ulaji wa wanga ndiyo chanzo cha matatizo yote, kwa kuwa kwa kula Wanyama watu hujiepusha na kemikali sumu zilizomo katika mimea ‘’antinutrients’’ kama phytates, oxalates, lectins, saponins, n.k. na pia huamini kiwango kikubwa cha sukari za wanga hasa za vyakula vinavyoliwa vyote ni matokeo ya kuwa, mazao yote ya kisasa sio matokeo ya mimea ya asili, ni matokeo ya ‘’teknolojia za breeding’’, hivyo huwafanya watu kuwa na uraibu wa kula sana, kwa kuwa wengi huwa hawaridhiki. Tafiti kadhaa huonyesha jamii wanazokula sana Mimea mfano india si kwa kuwa wanapenda, bali hushindwa kumudu Uchumi wa kuipata, na wengi huishia sana kula Mchele, na mbegumbegu za maharagwe, au mbogamboga za msimu, kwa kuwa huwa na gharama ndogo. Na wengi wao huheshimu Ng’ombe kama Mungu kwa kuwa huwapatia maziwa, na huwauza ili wapate fedha. Pia watu hawa huamini kwa kuwa vyakula vya wanga husababisha kutoridhika, hata kula sana, wengi wa watu huwa hawana kiasi, na wengi wanapoiona nyama hushindwa kujizuia kwa kufura kwa hamu, na hushabihisha hili na tafiti za kianthropolojia zilizoonyesha kuwa, jamii kadhaa za milimani, na zilizokuwa visiwani, zilionekana hata kula watu ‘’cannibalism’’, au kula viumbe waajabu kama ‘’Vyura’’, na kadri watu wanapokosa protini ndivyo wanavyokula ‘’nyoka, mijusi, n.k.’’ kwao kuna uhusiano wa moja kwa moja wa shida za kiakili, hasira, na kukosa nyama, mafuta ya Wanyama, na huchochewa zaidi kwa kushamiri kwa sukari mwilini.
Kwa kuwa watu hawa huamasisha ulaji wa nyama, hata matokeo ya kitabibu ambayo huonekana kwa ulaji wa nyama, hasa utatuzi wa shida mbalimbali za magonjwa ya misismko ya kinga ‘’autoimmune diseases’’, mfano, shida za uvimbe wa tumbo ‘’Inflammatory bowel syndromes, ngozi; psoriasis, akili; depressions, uzazi; PCO’s, n.k. wala Mimea wamekuwa wakiyapuuza. Hapo ndipo nilipogundua dunia inateswa zaidi si kwa kukosa Maarifa, ili ni kupitia falsafa ambazo huziweka nyuma ya uhalisia. Na ndivyo ilivyopia kwao wanapojaribu kufanya Mimea kuonekana ni changamoto, hata kambakamba ‘’fibers’’, na kiwango kikubwa cha kemikali za ‘’antioxidants’’ kama ‘’polyphenols’’, kitu ambacho kinashindana na ukweli pia kutokana tu na imani yao.
Si kweli kuwa binadamu hawezi kabisa kuvunja wanga, ana uwezo wa kuimeng’enya kupitia vivunjaji na bakteria kadhaa waliomo mdomoni, lakini pia bakteria waliomo tumboni wanatosha kuvunja kambakamba na kuzalisha ‘’short chain fatty acids; kama Propionate, acetate, na butyrate’’ zenye manufaa ya kutosha mwilini. Mbeleni tutaona mengi ya ajabu yaliyo nyuma ya Mimea, na kugundua ukweli nusu ni hatari kuliko uongo kamili.
HOJA ZISIZO NA UHALISIA
1.Protini ya Mimea inaweza kukujenga kimisuli kama Ng'ombe au sokwe wanaokula tu mimea
Mimea huwa na protini lakini protini yake huwa sio sawa na ya wanyama. Gramu 30 za protini toka katika ndizi au hata maharagwe zinaambatana na kiwango kikubwa sana Cha Wanga, au "calories', Kwa Maharagwe inaweza fika 400-500. Wakati gramu 30 za protini Kwa kipande Cha steki ya Nyama ni 250 tu. Hivyo kufikia kiwango kikubwa Cha protini kupitia mimea TU huweza kupelekea mtu akawa mhanga wa Wanga nyingi sana.
Protini za mimea pia huwa na kiwango kidogo Cha aina ya protini "amino acid' inayoitwa "Leucine'. Hii ni protini ambayo huanzisha uundwaji wa misuli, hivyo ulaji wa protini za mimea huwa hazisisimui sana uundwaji wa misuli Kwa kiwango kikubwa kama zilivyo za wanyama ambazo huwa na leucine nyingi.
2. Wewe ni Kama Sokwe Kwa kulinganisha anatomia ya utumbo
Utumbo mkubwa "colon" kuwa mrefu humuwezesha sokwe kuvundisha Chakula zaidi Kwa kuwa na Bakteria wengi zaidi, na hivyo huweza kuvunja wanga za mimea nyingi zaidi. Hii Ndiyo sababu sokwe hutumia masaa 6-10 kula tu. Binadamu ana utumbo mdogo "small intestine" mkubwa zaidi Kwa kuwa hufyonza zaidi Virutubisho vingi kupitia Vyakula ambavyo huvipika Kwa moto, na hii humpa ufanisi Kwa kuwa ana Ubongo mkubwa zaidi.
Binadamu ni "omnivores', yaani mla Mimea na mla nyama, Sio vingine kibiolojia. Binadamu hafanani na Tembo Wala Ng'ombe Kwa kuwa Ng'ombe ana Rumen yenye Bakteria wengi wanaomsaidia kuvunja mimea "fibers", na kuzalisha "chembechembe za Nitrogen kama ammonia" ambazo huzitumia kuunda protini. Na Tembo nae ana utumbo mkubwa"colon" mrefu sana na ndiyo maana hula sana, kama alivyo Farasi, hii huwa-Fanya kupata protini nyingi toka Mimea ambayo Binadamu Kwa utumbo wake mkubwa "colon" mdogo, na kukosa "rumen", hawezi kuwafikia. Wanyama Wala Mimea hula sana pia sifa ambayo inalingana na Ubongo wao kutoendelea sana, Binadamu hatumii muda mrefu sana Kula.
3. Tumbo la Binadamu Lina asidi kidogo "high pH 4-5" si sawa na uasidi mkali wa matumbo ya wanyama Wala Nyama "low pH 1-2"
Hii hoja Sio ya kweli, tumbo la Binadamu linapovunja Chakula huwa na pH ya 1.5-3 sawa kabisa na ya wanyama Wala Nyama. Kama pH ingekuwa 4-5 basi Moja Kwa Moja mlaji angepatawa na matatizo ya kimetabolikia, au shida ya upungufu wa asidi "hypochlorhydria".
4.Nyama huwa inaoza Tumboni Kwa kuwa hutumia muda mrefu sana kuvunjwa
Sio hoja yenye mantiki kabisa. Nyama huwa haifiki hata mara Moja katika utumbo mkubwa, huwa inavunjwa ikaisha mapema sana tumboni. Mimea "kambakamba" ndiyo hufika na kuvunda katika utumbo mkubwa "colon' Kwa uwepo wa Bakteria.
5. Meno na Mate ya Binadamu
Mate ya Binadamu Sio makali "alkaline", hoja hii haimaanishi kuwa Wanyama Wala Nyama mate yao ni makali "acidic", maana Kama ingekuwa hivyo basi wangechubuka sana fizi zao. Binadamu ana mate "alkaline" ili kuwafanya Bakteria waishi wanaomsaidia kuanza kuvunja mimea"Wanga " mdomoni- salivary amylase'. Hii inathibitisha asili ilimuandaa Binadamu kula Mimea Sio nyama tu kama wanyama Wala Nyama ambao hawana Bakteria na enzymes wa kuvunja wanga mdomoni.
Meno ya Binadamu Sio kama ya Ng'ombe, Wala Sio kama ya Simba, Wala Sio Sio kama ya Sokwe. Binadamu yupo katikati. Tazama Picha chini.
Unaweza jifunza zaidi Kwa kusoma kitabu changu Cha "Vita za Vyakula"
Softcopy 10,000/=Tsh
Hardcopy 20,000/=Tsh
Contacts
Dr Brighton Shoo
+255 7406 10988
brightonshoo7@gmail.com
Mwandishi na Mwenyekiti
Mtaalamu wa sayansi ya wanyama, mwanabiofizikia, na mwandishi wa vitabu vya kisayansi. Mwanzilishi wa Injili ya Sayansi — taasisi inayounganisha maarifa ya kisayansi na imani.
Shiriki makala hii
5 min
6 min
83 min