Inapakia...
Inapakia...

Dr Brighton Shoo
Mwandishi na Mwenyekiti
“Je wajua kuishi vijijini ni msingi wa Afya na ulinzi Kwa kuishi katika misitu, au maeneo yenye miti mingi; mimea huwa na tabia ya kufyonza mionzi yote ya mitambo ya kisasa ‘’nnEMFs’’, hufyonza pia mio…”
Je wajua kuishi vijijini ni msingi wa Afya na ulinzi
Kwa kuishi katika misitu, au maeneo yenye miti mingi; mimea huwa na tabia ya kufyonza mionzi yote ya mitambo ya kisasa ‘’nnEMFs’’, hufyonza pia mionzi ya Blue na myekundu, mimea huitumia hii katika kujitengenezea chakula chake; lakini wakati huohuo humuepusha kiumbe aliyechini yake dhidi ya madhara ya mionzi hatari ya blue na nnEMFs.
Mimea hutoa mionzi ya kijani ambayo huifanya ionekane ya kijani, na mionzi midogo ya ‘’NIR’’ ambayo huwa na faida kubwa kwa viumbe. Kukaa kwenye miti husaidia sana viumbe kupata Oksijeni ya kutosha, na kwa wale ambao hupanda miti au kukaa pekupeku chini ya mti; hupata chaji nzuri ya dunia, ambayo husaidia afya yao ya mfumo wa damu, kwa kuifanya damu isiwe nzito, kwa kuiongezea chaji ‘’zeta potential’’. Chini ya mguu kuna sensa za neva 1300 kwa inch square 1, hizi zinasaidia sana kuwezesha afya ya mfumo wote wa fahamu na viungo, na faida zingine nyingi sana kama zilivyogunduliwa na watafiti Clinton Ober, Dr. Stephen Sinatra, Martin Zucker, na mtaalamu wa Moyo Gaetan Chevallier, Ph.D. katika kitabu chao cha Kanyaga Ardhi ‘’Earthing’’.
Watu wanaokaa katika asili, wakichangamana na wanyama, rangi za asili zenye siri kubwa hutuliza afya zao kimwili na kiakili. Mfano mzuri ni rangi ya kijani ambayo huufanya ubongo u relax kwa kujiona upo salama, mwili unapoona kijani unaamini kuna maisha na hakuna stress. Rangi za maua, matunda, au magamba ya vyakula; za njano nyekundu, huashiria uwepo wa Carotenoids, ambazo ni chembechembe zenye Vitamin A, ambazo hizo ndizo hubalansi rangi za blue, ambazo zinatokana na hali za stress mwilini.
Sensa zote za mwili zenye ‘’Opsin’’, zinahizi Vitamin A, na hufanya kazi na Vitamin D zikishirikiana katika kuunda homoni zote, yaani; Vitamin A+pregnenolone+T3, T4 huunda homoni zote za uzazi + Vitamin D. Pia huunda kuta za viungo, ngozi, na hutawala mzunguko wa mwili ‘’circardian rhythm’’ kwa pamoja. Kwa kukaa katika asili balansi hii huwa sawa kabisa, lakini kwa kushinda katika usasa mwingi, mionzi ya blue kwenye taa za kisasa, au screen za simu; vitamin A zote huisha, na hupelekea tatizo la kuwahi kuzeeka, kupungukiwa homoni na afya ya uzazi, na shida ya viungo kwa kupungukiwa madini ya calcium, huku hali ya stress ikiwa juu sana, kutokana na pregnenolone kuishia kutengeneza homoni za stress zinazoitwa ‘’Cortisol’’.
Waafrika kwa asili huishi sana na wanyama, na makabila baadhi kama Wamaasai ni madaktari wazuri sana wa wanyama ‘’vet’’. Kwa kuishi na wanyama kama Wasukuma, hali za kisaikolojia huwa imara sana, watu hujifunza upendo, kujali, tafiti huonesha watu wanaowajali wanyama maranyingi sana huwa na huruma, na ubinadamu.
Mwandishi na Mwenyekiti
Mtaalamu wa sayansi ya wanyama, mwanabiofizikia, na mwandishi wa vitabu vya kisayansi. Mwanzilishi wa Injili ya Sayansi — taasisi inayounganisha maarifa ya kisayansi na imani.
Shiriki makala hii
29 min
1 min
11 min