Inapakia...
Inapakia...

Dr Brighton Shoo
Mwandishi na Mwenyekiti
“Kwanini Carrots na Viazi vitamu ni vya njano? Kwasababu hazina majani mengi ya kijani ‘’chrolophyl’’, hivyo hujiinda na mwanga wa blue kwa kuwa na caretonoids nyingi sana. Carrots hutunza chakula chak…”
Kwanini Carrots na Viazi vitamu ni vya njano?
Kwasababu hazina majani mengi ya kijani ‘’chrolophyl’’, hivyo hujiinda na mwanga wa blue kwa kuwa na caretonoids nyingi sana. Carrots hutunza chakula chake chini kama ambavyo huwa kwa viazi vitamu. Ukiona mmea unatunza chakula chake chini ya ardhi maana yake ni kuwa; hakina walinzi wengi ‘’antioxidants’’ wa kujikinga na madhara ya mwanga wa jua ‘’oxidants’’. Na hili utaliona hasa kwa Carrots kwa kuwa nyingi ya hizi huwa sio matokeo ya asili, nyingi zilibadilishwa kupitia matendo ya kuizalisha kuibadili kijenetikia ‘’selective breeding’’. Mimea ya mtindo huu huwa haina kinga, na hivyo; hutumia mbinu ya kufukia chakula chake ili kupunguza vita dhidi ya vihatarishi ‘’oxidants’’.
Viazi vitamu hushamiri sana maeneo ya ukame, na huwa na kiwango kikubwa sana cha caretonoids kwa ajili ya kupambana na mwanga mkali wa jua. Viazi vya njano huwa na kiwango kikubwa sana cha Vitamin A kama ‘’Screen protector’’ dhidi ya madhara ya mwanga wa Blue unaoshamiri katika jua kali. Inafahamika pia kuwa viazi vitamu vina kiwango kikubwa sana cha wanga isiyovunjika kirahisi ‘’resistant starch’’, sababu bado inarudi kuwa ni namna yake ya kulinda chakula chake kwa ajili ya ukame.
Je wajua!
Viazi VITAMU vina vitamin A nyingi sana ila Sio vyote, ni vya NJANO au vya Lishe. Kizazi kitamu hiki pia kina sifa kubwa sana ya kushusha Cholesterol ya mwili. Kwa chaguo la vitamin A viazi VITAMU vya njano ni zaidi ya Carrots.
Mwandishi na Mwenyekiti
Mtaalamu wa sayansi ya wanyama, mwanabiofizikia, na mwandishi wa vitabu vya kisayansi. Mwanzilishi wa Injili ya Sayansi — taasisi inayounganisha maarifa ya kisayansi na imani.
Shiriki makala hii
29 min
1 min
11 min