Inapakia...
Inapakia...

Dr Brighton Shoo
Mwandishi na Mwenyekiti
“Kwanini kuna Mbegu zimejaa Protini kama- Maharagwe, au Kunde, na zingine Wanga- Mahindi, au Mpunga? Kama Hoja ya Mimea ni kutunza chakula kwa ajili tu ya mbegu, iweje mbegu kama za maharagwe, njegele,…”
Kwanini kuna Mbegu zimejaa Protini kama- Maharagwe, au Kunde, na zingine Wanga- Mahindi, au Mpunga?
Kama Hoja ya Mimea ni kutunza chakula kwa ajili tu ya mbegu, iweje mbegu kama za maharagwe, njegele, kunde, choroko, na zinginezo ‘’legumes’’ ziwe na protini nyingi, huku nyingi kama Mpunga, Mahindi, ngano, na zinginezo ‘’Cereals’’ zikijaa wanga, sababu kubwa imejificha katika hoja ya msingi ya awali.
Ili Mmea ukue haraka sana unahitaji wanga sana, na hii ndiyo sababu mazao kama mpunga ambayo hutegemea kipindi kifupi cha msimu wa mvua, huwekeza sana katika wanga ili kuwahi kukua kwa kuwa mashina yake hutegemea tu wanga ‘’cellulose’’, na huwa na majani kidogo sana hivyo huitaji madini kidogo sana. Mimea hii hustawi sana pia katika maji mengi, na sehemu zenye joto na jua kali kama Morogoro, Ifakara Tanzania. Mimea hii huwa dhaifu sana kutokana na sukari yake nyingi, hivyo huliwa sana na wadudu, ndege, n.k.
Mimea ya Maharagwe na jamii za kundekunde, na soya, huwa na uwezo mkubwa zaidi ya mimea jamii ya mpunga, na mahindi. Mimea hii huweza kushirikiana na bakteria waliomo katika udongo wanaoitwa ‘’Rhizobium’’ kuchakata madini ya Nitrogen na kuweza kuunda Protini. Mimea hii kwa kuwa na protini nyingi katika mbegu zake asilimia zaidi ya 40% huwa na ukuaji wa polepole, lakini huweza kushamiri hata katika ardhi isiyo na madini ya Nitrogen kwa kutegemea akiba yake, jambo ambalo Mahindi hushindwa. Na Protini hizi ‘’albumins na globulins’’ hutengeneza kemikali ambazo Ladha zake huwa ni chungu kwa Wanyama, hivyo huwa haziliwi kirahisi na hudumu sana, na pia huziwezesha kutengeneza matawi imara, na majani.
Kama ambavyo pundamilia ana akili kuliko nyumbu ijapokuwa amezidiwa umbile la ukubwa na spidi ya ukuaji, ndivyo ilivyo pia kwa Mahindi yalivyozidiwa akili na soya, au maharagwe. Kama ilivyorahisi kwa simba kumla nyumbu kuliko pundamilia, ndivyo ilivyorahisi kwa binadamu kula mchele hata mbichi, lakini sio kula maharagwe, au njegele, au soya bila kuzichemsha kuvunja tabaka la nje. Maisha ni vita iliyojikita katika mbinu, spidi, na uwezo wa kutumia nafasi yako kufanikisha uzao wako. Na akili yako inaanza katika uchaguzi wa vyakula vyako.
Mwandishi na Mwenyekiti
Mtaalamu wa sayansi ya wanyama, mwanabiofizikia, na mwandishi wa vitabu vya kisayansi. Mwanzilishi wa Injili ya Sayansi — taasisi inayounganisha maarifa ya kisayansi na imani.
Shiriki makala hii
29 min
1 min
11 min