Inapakia...
Inapakia...

Dr Brighton Shoo
Mwandishi na Mwenyekiti
“Kwanini Mbogamboga Na Matunda Ni Kiini Cha Uhai? Nadharia yangu na ya Wanasayansi wengi kwa zama hizi ni kuwa, Chanzo kikuu cha Uhai ni Maji, mwanga, Umeme-sumaku, na mfumo wa Maelekezo, wao wanauita…”
Kwanini Mbogamboga Na Matunda Ni Kiini Cha Uhai?
Nadharia yangu na ya Wanasayansi wengi kwa zama hizi ni kuwa, Chanzo kikuu cha Uhai ni Maji, mwanga, Umeme-sumaku, na mfumo wa Maelekezo, wao wanauita ‘’Universal consciousness’’, Mimi nauita ‘’Roho ya Mungu’. Tunaweza Jifunza uhai kibiolojia kupitia Fizikia ya kuanzia Maji, mwanga, na Usumaku. Mimea ndiyo hatua ya awali kabisa ya kula mifumo hii mitatu, yaani hutumia mwanga, maji, na usumaku-umeme kutengeneza chakula chake. Mfano, ukiyaweka maji katika Microwave, kisha ukayaweka kwenye Mmea, mmea hautakua. Ukiuweka Mmea kwenye Balbu za kisasa utengeneza chakula, hakika utakufa. Ukiupeleka Mmea, maji, na Udongo kwenye sayari kama Mars utakufa. Hii inamaanisha unahitaji uwiano sahihi wa misingi yote hiyo minne ili Mmea uweze Kuishi.
Kwanini Mmea tu ndiyo Chakula japo Simba hawawezi ridhia?
Ni mmea tu ndiyo unaoweza kuliwa na ukaendelea kuishi bila ulemavu. Ijapokuwa mijusi ‘’salamanders’’ katika tafiti za majiniazi wangu wa muda wote, ‘’Dr Robert O Becker’’ zinaonyesha wanauwezo wa kuumba tena upya mikia yao hata ikikatwa, lakini nao hawawezi jitegemea bila kuua wadudu wenzao ili waishi, ambao bado wadudu wanategemea mimea. Mimea inatumia namna mbili kuishi, kupitia kuwezesha viumbe wengine kwa kuwalaghai kwa chakula chao hasa cha wanga, ikiwatumia kusambaza mbegu zao, au ikiamua hujizalisha yenyewe tena ikiwafukuza mbali kwa miba, uchungu, ukali, au sumu.
Viumbe wengine wote ni wategemezi ‘’Parasites’’. Kadri kiumbe kinavyokuwa na mbinu zaidi, basi kinatumia zaidi namna ya kupata chakula bila gharama kubwa ya kukitengeneza, mfano; gharama ya kushinda juani siku nzima, kutafuta maji futi za kutosha chini ya ardhi, biolojia complex ya kuunda chakula kwa kutumia hewa chafu, madini, n.k. simba ni mfalme kwa kuwa hatumii gharama kubwa kutafuta chakula kama anavyotembea siku nzima nyumbu, hii ni sawa kabisa na wafalme tunavyowalipa wao na wajukuu zao ili watumie kodi zetu.
Mimea ni viumbe pekee ambao ungewaita leo chakula, na kesho ukawaita tena wakiwa hai na matunda mengine ya kukupa. Kama Simba akikuita chakula lazima utasali sala ya Baba yetu ukiwa na stress za kutosha katika damu, na hivyo kumsaidia kunywa damu yako tayari ikiwa na Glucose, na protini nyingi kama albumins, na homoni ambazo ulizihangaikia kwa kula gunia la mahindi, na maharagwe mwaka mzima.
Je, Mimea ina uhusiano na Urefu wa maisha?
Uhusiano upo Dhahiri kabisa, lakini si katika mantiki ya tafiti wanazotumia wasomi wa lishe. Upo katika mantiki ya Kimetabolikia. Dr Herman alishaonyesha miaka mingi nyuma kuwa sababu kubwa za kuzeeka ni kushamiri zaidi, na kushindwa kuchakata kemikali sumu ‘’free radicals’’. Na hizi kemikali sumu nyingi huwa ni ‘’Reactive oxygen species’’, ambazo huwepo ‘Superoxides, hydroxyl radicals, hydrogen peroxides, n.k. ‘’ si kweli kuwa ni sumu kuwa hazina kazi, kwa kusema hivyo ntamkosea Professor Nick Lane kwa kusema nimesoma vitabu vyake vyote vya ‘’Biochemistry’’, vinavyoonyesha hizi pia hutoa taarifa kwa seli kuratibu metabolikia. Mfano mzuri ni pale ambapo, kemikali sumu ‘’hydroxyl radical’’ inapodakwa na mlinzi wa mwili ‘’Glutathione’’ katika sehemu ‘’Thiol goup’’, hiki kitendo huzalisha mawimbi madogo ��’ UPE ‘Ultra weak photonic emission’’, ambayo huifanya Complex V kuzunguka uelekeo wa Saa na kuzalisha nishati ‘’ATP’’. Hivyo hoja ya kuzeeka sio tu kushamiri kwa kemikali sumu ‘’free radicals’’, ni kuanza kufeli kwa mfumo wa kuziratibu.
Kwanini Kimetabolikia Mimea inawezesha viumbe kuishi miaka mingi zaidi? Kwa kuwa mimea hushinda juani na kwenye oksijeni muda wote, hivyo huwa imejaa kemikali walinzi ‘’antioxidants’’ wa kujilinda, na hii ni kwa kuwa; oksijeni na mwanga wa UV ndiyo wauaji wakuu, na hii ndiyo sababu hata chupa nyingi za dawa huandikwa usiweke kwenye mwanga, hata chupa za beer huwa ‘’tinted’’. Hizi ndizo sababu pia ukikata tunda ukaliacha wazi tu baada ya muda utakuta limeharibika. Ni kwamba binadamu wengi hawajui kuwa hata chanzo cha hizi kemikali sumu ni Oksijeni unayovuta inapopokea electron mbili badala ya nne katika matendo ya kuzalisha nishati ‘’ECT’’. Matunda huzalisha rangi mbalimbali ‘’polyphenols’’ ambazo ni antioxidants kama tulivyokwisha ona kama namna ya kujilinda, hasa rangi za wekundu. Lakini ajabu ni kuwa; hata binadamu wakichubuka, mchubuko hukauka kwa rangi ya wekundu ambayo hutokana na kemikali za ‘’Billirubin’’, ambazo ni antioxidants pia za mwili ‘’endogenous’’, ni kuwa mwili hulinda seli zake zisiathiriwe na mwanga wa UV, na oksijeni nyingi. Hii tu inaweza kukueleza kwanini Binadamu tu ndiyo huingia katika mzunguko wa hedhi, kwanini asiirejeshe damu yake ndani aitumie tena kama nyani? Ni kwa kuwa tayari huwa imekutana na oksijeni nyingi hata kuwa kemikali sumu nyingi, kwa kuwa ng’ombe hawana Ubongo mkubwa, na wanaishi miaka michache wala hawajali.
Je Kila Mmea una ‘’Antioxidants’’?
Ndiyo, kwa kuwa kila kiumbe kinajilinda. Lakini sehemu pekee ambayo unaweza pata ‘’antioxidants’’ nyingi zaidi ni katika matunda yenye rangi. Rangi nyingi ni ‘’Polyphenols’’ ambazo tulikwisha ziona. Kwa kuwa mtu anayekula wali, au ugali kila siku naye anakula Mimea, basi niko sahihi pia kusema sio kila mmea una ‘’antioxidants’’ kwa kulenga kiasi chenye kuweza kuleta matokeo kiafya. Ni wale tu wanaokula zaidi mbogamboga, au wanaokula ‘’Upinde’’ kumaanisha wanaokula aina mbalimbali za rangi za matunda na mbogamboga.
Inasikitisha kuwa viungo vingi sana vya uzazi vya mimea ndivyo huwa na virutubisho, yaani Matunda, mbegu, na majani. Huku ndiko unapoweza pata Vitamin C nyingi ambayo tulikwisha iona kemia yake, na kwanini imejaa zaidi kwenye machungwa au malimao. Na ndivyo ilivyo kwa antioxidants nyingine zote kama vile Vitamin E ambayo huwa kwenye mafuta kuzunguka mbegu, au ya matunda. Polyphenols kama ‘’Carotenoids, Flavonoids, phenolic compounds’’, hizi zote huwa kwenye Ngozi za matunda, na pia madini kadhaa kama selenium ambayo nayo huwepo zaidi kwenye mbegumbegu. Ni kweli matumizi ya mimea yenye ‘’antioxidants’’ husaidia sana mwili kupunguza kemikali sumu, hasa zinazotokana na stress, na ulaji wa mafuta ya mbegu mfano ‘’4-HNE’’.
Je Nini unapaswa kufahamu zaidi?
Mwandishi na Mwenyekiti
Mtaalamu wa sayansi ya wanyama, mwanabiofizikia, na mwandishi wa vitabu vya kisayansi. Mwanzilishi wa Injili ya Sayansi — taasisi inayounganisha maarifa ya kisayansi na imani.
Shiriki makala hii
29 min
17 min
11 min