Inapakia...
Inapakia...

Dr Brighton Shoo
Mwandishi na Mwenyekiti
“SAYANSI YA UDANGANYIFU NA UUAJI HATARI ZAIDI WA BIDHAA ZA MABADILIKO YA KIJENETIKIA G.M.O ‘’GENETIC MODIFIED ORGANISMS’’ Sayansi yote ya jenetikia imejikita sana katika utendaji wa vinasaba au Genes.…”
SAYANSI YA UDANGANYIFU NA UUAJI HATARI ZAIDI WA BIDHAA ZA MABADILIKO YA KIJENETIKIA
G.M.O ‘’GENETIC MODIFIED ORGANISMS’’
Sayansi yote ya jenetikia
imejikita sana katika utendaji wa vinasaba au Genes. Ambazo, zipo ndani ya DNA.
Lakini hebu kwanza tukumbuke namna vitu hivi vilivyo.
Mwili umeundwa na seli, na
ndani ya seli kuna chembechembe kadhaa, lakini Pamoja na chembechembe hizo.
huwa kuna kiini au center au makao makuu au ‘’Nucleus’’ ambayo hiyo ndiyo
huunda kiini cha seli. Ndani ya Nyuklia pia kuna chembechembe kadhaa, lakini kati
ya zote, kuna chembechembe ambazo hizo zipo mithili ya kambakamba, ambazo
huitwa ‘’Chromosomes’’, na katika hizi ndipo unakutana na chembe chembe zenye
taarifa nyingi sana kuhusu mtu, zinazoitwa ‘’DNA’’. DNA ni zaidi ya
supercomputer yoyote kuwahi kutotea katika ulimwengu. Kama ambavyo unauona
ulimwengu, ukiwa mkubwa na kuwa na taarifa zisizo na mwisho, ndivyo zilivyo
pana taarifa katika DNA.
|
|
DNA
au ‘’Deoxyribonucleic acid’’ huwa ni chembechembe ambayo inaundwa na pande
mbili zilizo kama Kamba, ambazo zimejikunja, kama zinavyoonekana katika picha
chini, hizi DNA huwa na chembechembe kadha wa kadha. lakini huwa na miunganiko
ambayo, huundwa na chembechembe Nne tu zinazojirudia, hizi huitwa ‘’Nucleotide
bases’’, yaani A, G,T na C
Kama ukiikunjua DNA yote, basi
inaweza kujikunjua mpaka kufikia futi 10. Na ndani ya DNA, kuna maelekezo yote
kuhusu maelekezo ya namna seli inapaswa kufanya kazi, na kuwa.
DNA ya binadamu ina base pairs
Bilioni tatu. Na katika hizo zote, wanasayansi wameweza kuzigundua genes zikiwa
katika asilimia 1-3% tu.
Genes ni vipisi katika DNA,
ambavyo, vina maelekezo ya uundwaji, au taarifa kuhusu kitu Fulani tu, katika
mwili. Mfano, urefu wa nywele, rangi ya macho na Ngozi, seli za mifupa n.k,
kila unachokiona katika mwili, ni maelekezo ambayo katika mwili yameandikwa kutoka kwenye DNA, katika vipengele vya
genes.
Msingi
Katika Kuelewa Sayansi Genes
Ukielewa genes umeshaelewa
kila kitu, haiihitaji elimu na ufundi mkubwa sana kuitambua, ila inahitaji
msingi tu kuielewa. Genes ni vipisi vya DNA, ambavyo huwa na urefu Fulani, na
katika huo urefu au‘’segment’’, huwa
kuna mipangilio yake ya zile base pairs nne, ambazo, huwa na melekezo ya upekee
ya kuelekeza uundaji wa aina Fulani ya protini.
Mwili wako upo hivo tofauti na
wangu kwa sababu DNA yako, ina taarifa tofauti kidogo na mwili wangu, na
taarifa hizo zipo katika vipisi hivi vya genes. Kitu kinachofanyika ni kuwa,
unapokuwa hai muda wote. Huwa, unakuwa katika vipindi vya ukuaji au maendeleo
ya kimwili. Na sasa basi, hizi DNA huwa zikivunjwa na enzyme husika kabisa
anayeitwa ‘’DNA helicase’’. huyu na wenzake na katika mazingira Fulani,
huivunja DNA yenye pande mbili ‘’double strands’’ na kupelekea strand moja. Na
katika hii pande moja, inayokuwa ipo free, huundwa chembechembe nyingine ya
aina hii ambayo inaitwa RNA. Hii ni kama vile ambavyo, ungekuwa na kufuli na
funguo yake, vikiwa vimefungana, na kisha, uchomoe funguo, halafu ile funguo,
uikandamize kwenye sabuni, ili kuunda umbile kama lile la kufuli, na unaweza
kuunda mfanano kabisa wa lile kufuli. Na sasa hivi ndivyo huwa kwa DNA na RNA,
hapa RNA huwa ni kama kufuli hili jipya la sabuni. na sasa basi, hii RNA ambayo
huwa inaitwa mRNA. hutoka ndani ya Nyuklia ya seli, na kuingia katika seli.
Yapo matendo baadhi mengi lakini hoja ya mfanano, ni ya msingi zaidi kwa mRNA.
Inapifika katika seli, huwa
kuna matendo kadhaa ambayo huwa yakitokea, lakini la msingi hasa, katika kuelewa
huu msingi wetu ni hili, ile mRNA yetu, hupokelewa na chembechembe za seli
zinazoitwa Ribosomes, na hizi huwa na vipande viwili, ambavyo nitavionesha kwa
picha chini. kwa mRNA yetu, ni kama Kakamba Fulani ambako, kana vipisi vilivyo
nusu nusu ya zile bases za DNA, basi hii ribosome huishika hii mRNA, kwa upande
utakao achilia hii sehemu yenye bases huru, na baada ya hapa, kitakachotokea ni
kuwa, huwa wanakuja aina nyingine ya tRNA ambao hao, huwa wamebeba vipande vya
chembechembe za protini au amino acids. Na kwa mantiki hiyo, hawa kazi yao huja
katika ile chain ya RNA, na kisha husoma mfuatano wa base nne, na kisha huachia
amino acid moja.
Hii amino acid moja ambayo
huwa ni kama ka goroli kamoja. ambako huwa kanashikiliwa pale kwenye ribosome,
na kisha ribosome huivuta ile chain ya mRNA, ili sehemu nyingine ambayo
haijasomwa iweze kusomwa, na kwa hivyo itakuja tRNA nyingine, ambayo nayo itasoma
mpangilio mwingine wa bases nne, na kuacha amino acid yake. Hii amino acid
itaenda kujiongeza kwenye kale ka goroli ka kwanza, vitakuwa viwili na baadaye
vitatu, na baadae vinne mpaka utapata chain ya protein au ‘’polypeptide chain’’
ya kutosha. Mfumo huu huwa una chembechembe ambazo, huwa zinatoa taarifa za
kuanza na ku stop, chembechembe hizi huwa ni aina ya maelekezo tu ya zilezile
genes, yakiwa yanatafsiriwa kwa uzalishaji wa amino acids, katika kuanza, na
katika kumaliza.
Kitendo hiki nilichokisema
bado kina mengi sana ambayo huwa yakitokea, na hasa kwa wataalamu wa biolojia
za jenetikia, lakini kitendo hiki hasa kwa kila mwanasayansi ni kama vile
unavyoangalia movie, unauwezo wa kuizima au kuibadilisha kwa kuchukua original
film na kui edit, lakini bado hatuelewi nini hasa chanzo na ghala la taarifa
hizi.
Hapa lengo kubwa kwanza
lilikuwa tujue gene. Na kisha tujue namna inavyofanya kazi, na kisha tutaona
hasa ni nini ambacho ndicho chanzo cha sayansi za uharibufu mkubwa, katika
sehemu hii. Mchoro unaotoa ufupisho wa uundwaji huu.
Mfumo huu wa kutegemea
uzalianaji wa jinsia ya kiume, na ya kike tu ili uweze kufanya mabadiliko
katika kutengeneza tabia Fulani ya kiumbe ‘’traits’’. umekuwa kwa miaka mingi
sana. Lakini ghafla sasa wana biolojia wamekuja na mbinu mpya kabisa.
Kuhamisha
Genes Kutoka Kwa Kiumbe Mmoja Kwenda Kwa Mwingine
Wanabiolojia wamekuja na namna
ya kipekee sana, ya kuweza kuchukua genes kutoka kwa mnyama mmoja, na kuiweka
kwa mnyama mwingine. Kitendo hiki kinawezesha kitendo cha kuipata tabia Fulani
kwa mnyama Fulani, kwa kuipachika tu baada ya kuitoa kwa mnyama mwingine ambayo
ana sifa hiyo. Na kitendo hiki kinawezesha kuanzisha tabia Fulani, bila hata
kuwakutanisha Wanyama hawa.
Hiki kitendo maana yake ni
kuwa, kinaweza kutoa genes kutoka kwa mnyama mmoja, na kisha kuiweka ile gene
katika DNA ya mnyama mwingine. na ile gene inapofika kwa mnyama mwingine, basi
inaanza kuunda protini kama ambavyo huwa inaunda kwa mnyama yule wa awali.
Taaluma hii inawezekana
kwasababu kubwa moja, ambayo ni rahisi sana, Wanyama wote wana DNA, na kwa
mantiki hiyo, wanabiolojia wana uwanja mpana sana wa kuchagua aina za genes,
wanazozitaka na kuziweka popote pale.
Mfano
Wa Maajabu Ya Hii Teknolojia
Wanasayansi wanatambua specie
au aina ya Samaki wanaoitwa ‘’Arctic
Flounder’’ huwa wanaishi katika maji ya baridi sana, bila kuganda. samaki hawa
wanauwezo wa kuishi katika mazingira haya ya baridi, bila kuganda. kwa sababu
tu, wana sifa zinazowawezesha kutokuganda. Ikiwemo, kuwa na protini ambayo
inaitwa ‘’anti-freeze protein’’. Sasa
basi, kuna changamoto kubwa sana duniani ya kuharibika kwa nyanya, kutokana na
baridi kali au ‘’frost’’. Kwa hiyo sasa, ili tupate nyanya bora, ambayo
haitaathiriwa na mabadiliko haya ya hali ya hewa, na nyanya ambayo itawakomboa
wana biashara, kutokana na kuharibika kwa baridi kali. Hatupaswi kusubiria tena
miaka mamilioni ya mabadiliko ya viumbe au ‘’evolution’’. ambayo yatamtoa
Samaki huyu kutoka majini, ili aje nchi kavu kuzaliana na nyanya.
Watakachoweza kufanya hapa, ni
kuchukua ile gene ya kutengeneza hii protini, ya ‘’anti-freeze protein’’,
ambayo, iko kwenye Samaki. na kisha hii gene, tutaiingiza katika nyanya. Na kwa
mantiki hiyo, hii gene ikiingia katika nyanya, itasababisha uwepo wa protini za
kuzuia kuganda ‘’anti-freeze proteins’’ katika nyanya. Na sasa nyanya yetu
haigandi, kwa kuwa na faida ya kuweza kujitengenezea protini ya kuzuia kuganda.
Sayansi hii ni nzuri sana kwa
namna yake inavyoweza tengeneza maajabu makubwa, na ndoto kutimia. Unaweza
fikiria kitu na kujaribu kukifanyia kazi. Na kweli bidhaa za aina hii nyingi
sana, zimetengenezwa. na kuna uwezekano mkubwa sana, hata msomaji ukawa mtumiaji
mzuri sana, tena hata kwa zile ambazo huonekana kabisa sio matokeo ya ufundi
huu, huko mbele tutaangalia.
Kuchelewesha
Kifo Kwa Msaada Wa Genetic Engineering
Huko mbele kabisa,
nitakuonesha aina mpya kabisa za kisasa za mabadiliko haya. Ambazo, hazihusishi
hata namna ya kuingiza moja kwa moja, aina Fulani ya gene kutoka kwa mnyama
Fulani, kuja kwa mnyama mwingine. hawa huja na aina nyingine ya kutumia ‘’Artificial Intelligence’’. katika
kuiboresha gene, ‘’wao husema’’ ku shape makosa kadhaa katika gene, kwa msaada
wa teknolojia ya sayansi ya chembechembe za kutengenezwa kisasa, kupitia
teknolojia ya ‘’nanotechnology’’, hizi huwekwa kwa kuongozwa na AI, na kisha
kulenga genes Fulani ambazo, huonekana zikiwa na shida Fulani. na kisha,
kuzirekebisha. Lakini kabla hujajua watu hawa wanakudanganya au hawakudanganyi,
lazima ujue misingi kwanza ya sayansi. Hebu tuangalie kwanza misingi ya sayansi
pana chini, ya utendaji wa kijenetikia, na ufundi wa kuinjinia kijenetikia.
Sayansi
Ya Moto Katika Ujenzi Wa Kijenetikia Inayo Umbua Wataalamu Wa G.E
kuegemea
katika nadharia zilizopitwa na wakati
Hapo zamani ilikuwa ina
fahamika kuwa siku zote ‘’gene’’ moja huwa ikitoa maelekezo kuhusu kuundwa kwa
protini moja. Yaani ‘’one gene- one protein’’. Na kwa mantiki hii ilikuwa
inafahamika kuwa ‘’genes’’ ni unique au za pekee sana.
Baada ya muda Fulani, ikaja
kugundulika kuwa si kweli, yaani gene moja huweza kushughulika na protini zaidi
ya moja. Na hii ilianza kushanganza sana baada ya wanasayansi kugundua kuwa
kwanza, mwili wa binadamu kwa mfano, una idadi ya protini 100,000. Na kwa hivyo
tulitegemea kupata walau genes 100,000. Lakini cha ajabu ikaonekana kuna genes
30,000 tu.
Hili swala lilileta
kitendawili kikubwa sana hakijawahi kutokea hasa kwa wataalamu wa G.E. kama
tutakavyoendelea kuangalia huko mbele. Hii ni sawa na kushindwa kuelewa, sababu
za uwingi mkubwa wa aina mbalimbali za protini. kituko zaidi ni kuwa, bado kwa
magugu baadhi ya mimea kukaonekana kuna genes 26,000. Hii ni sawa na kusema,
kama magugu yana protini chache tu, halafu yana genes zote hizo, kwa nini sisi
wenye protini nyingi zaidi tusingepaswa kuwa na genes nyingi zaidi?
Rafiki yangu usidhani haya
mambo yanaendelea ukiwa haupo duniani!!! Ni mwaka 2000 tu hapo juzi.
mtazamo mpya
Ikatambulika tena kwa upya
kabisa kuwa, inaonekana aina mbalimbali za genes huwa hazitoi maelekezo kwa
uumbaji wa protini moja tu.
Yaani gene moja, inaweza kutoa
maelekezo ya kuunda aina mbalimbali za protini. Mfano, kwa mdudu mmoja
anayeitwa ‘’Fruitfly’’ ikaonekana kwake ‘’gene’’ moja, inaweza kuunda mpaka
protini 38,016. Kinadharia pia ikaonekana kana kama, kila gene ina uwezo wa kuunda
protini moja au zaidi. Na kama kuna genes ambazo huwa zinatoa maelekezo ya
kuunda aina moja tu ya protini, basi zipo kwa idadi ndogo sana ya kulinganisha
na idadi ya vidole vyako.
Kwanini
Hili Ni Pigo La Kwanza Kwa Genetic Engineers?
Kwao hawa wanataka kuchukua
gene moja tu, mfano ya kuunda protini ya kuzuia kuganda ‘’anti-freeze protein’’
na kwa hivyo, hii gene kwao wanategemea wakiiweka kwenye nyanya, basi itaunda
protini ‘’anti-freeze protein’’ tu. Lakini bahati mbaya, kwa nadharia hii mpya,
hii gene mbona inaonekana kana kwamba itaenda kuunda na protein zingine, ambazo
sisi hatuzihitaji. Hebu chukulia ile gene, iwe inatoa maelekezo ya kuunda na
protini za kuulia vimelea vinavyomshambulia Samaki?? Itakuwaje sasa ikiwa kuna
aina nyingine za protini, ambazo zinahatarisha ubora wa nyanya yetu?
Kumbuka, taaluma ya gene kuunda idadi Fulani ya protini, kwa majina yake haipo, kinachofahamika ni namna gene Fulani huusika na uundaji wa protini Fulani. Mfano mzuri hapa ni kama huu, tunafahamu kuwa Mimi ni Daktari, na huwa nafanya kazi ya kutibu wanyama, lakini kuhusu mimi pia kuhusika kwenye kulima, au siasa, au kuandika vitabu, hilo sio jambo ambalo unaweza lipata kirahisi! kwa maana linategemea taarifa nyingi ambazo huwezi kujua zinapotekea, ni kama maamuzi! Na hivyo ndivyo ilivyopia hapa katika hizi genes na protini.
Uwepo
Wa Chembechembe Zinazoitwa ‘’Spliceosomes’’
Hizi chembechembe za
‘’spliceosome’’ ni kama vile mama wa nyumbani, baada ya kuletewa Mahindi
mabichi na mme wake, anaweza yabadili kwakuamua, ayachome, na chakula kiwe
mhindi wa kuchoma, au ayachemshe, au apike kande, au akaushe na akasage liwe
dona, au hata akoboe, na liwe sembe!!
Baada ya DNA kuvunjwa katika
kitendo kinachoitwa ‘’DNA replication’’, ile copy ya RNA, ambayo huwa inaundwa
kama nilivyoielezea kule awali. Kabla ya Kwenda kutafsiriwa au ‘’translation’’
hupitiwa kwanza na hawa bwana ‘’Spliceosomes’’. Hawa huiboresha hii RNA, na
kama namna ambavyo huwa wakiiboresha, basi ndivyo taarifa ya mwisho pia huwa
ikiboreshwa. Kwa mantiki hii, hizi ‘’spliceosome’’, zinaweza kupelekea kuundwa
kwa protini nyingine, tofauti au mpya kabisa na ile ambayo uliifikiria awali.
Zipo Spliceosomes ambazo
zinaweza itafsiri gene moja, na kuipelekea kuundwa kwa mamia tena, mpaka maelfu
ya Protini.
Wewe sasa unaweka gene yako ya
kuunda protini, ya kuzuia kuganda au ‘’anti-freeze protein’’, sasa ile gene
yako itakavyokaa katika RNA ya mnyama, au mmea. Je, una uhakika gani kuwa hii
gene itakaposomwa na hawa ‘’spliceosome’’, itapelekea kuundwa kwa aina moja tu
ya protini?
Huku ni kucheza na Maisha ya
watu kwa kweli. Kwa maana, kama Spliceosome za Wanyama, au binadamu, zitapokea
hii taarifa na kuunda protini nyingine tofauti na iliyotegemewa! basi unaenda
kuunda sumu ambazo hakuna anayeweza kuzitambua, hata mwili wenyewe hatujui
utashtushwa kwa kiwango gani!!! Na
kwanza, hakuna anayejua namna hizi spliceosome za mnyama namna
zitakavyoshtushwa, kwa kukutana na maelekezo ambayo haijawai yaona, na hata
hatujui zitakavyo chukulia hatua swala hili, na ndiyo maana, G.E ni hatari kuliko
mtu anaweza kukuelezea.
Wataalamu
Wa G.E Wajitetea Na Kufeli Tena
Hizi Spliceosome ili ziweze
kuichukua hii gene, na kuiboresha, zinahitaji uwepo wa chembechembe zingine
ambazo huwa zinaitwa ‘’Introns’’. Hizi Introns huwa zinakwepo katika genes za
kila mmea na Wanyama. Lakini huwa hazipo kwa genes za Bakteria.
Kwa mantiki yao ni kuwa, kama
unahamisha genes kutoka kwa Bakteria kuja kwa mnyama, au mmea, basi hiyo gene
haitabadilishwa na spliceosome ya huyo mnyama. Maana, introns ni kama vile huwa
ni sehemu katika genes za Wanyama, na mimea, ambayo, huwa inamwita spliceosome
‘’Njoo, nichukue!!’’ na sasa basi, hawa wataalamu wa G.E wakataka wajitetee kwa
namna hii kwamba, kama watatoa genes kwa bakteria, na kuziingiza kwa Wanyama,
zitaenda kufanya kazi yake husika tu kama ambavyo ilikuwa imelengwa.
Cha
Ajabu Wanarejea Spliceosomes
Wakachukua genes kutoka kwa
Bakteria za kujikinga na wadudu ‘’insecticides genes’’. na kuziingiza kwa
Mimea. ambayo ilikuwa ni Mahindi na Pamba, ilikwamba hizi genes zikatengeneze
protini za sumu kwa mimea, ya kujikinga na wadudu. kwa pamba na mahindi. ili
tupate mahindi ambayo, hayatadhuriwa na wadudu bila hata kupuliziwa dawa.
Lakini kitu cha ajabu kutokea ni kuwa, baada tu ya kuweka zile genes za
bakteria za sumu, za wadudu, kwa mimea. uzalishaji wa mimea wa protini za sumu
hizi, ulikuwa hafifu sana. na hata kuelekea kutokuwepo kabisa. Hii ilimaanisha
kuwa, hizi genes za bakteria zikiingizwa moja kwa moja kwa mimea, na Wanyama,
hazina nguvu ya kuamsha mfumo wa jenetikia wa mimea wa kuzalisha protini.
Walichofanya, wakaongeza ‘’Spliceosome’’. na hatimaye, mmea ukaanza kuzalisha
protini. Swali likaja, spliceosome itafanya nini tena kwa RNA hizi za sumu??
Protini yoyote ile
inayotengenezwa katika mwili, huwa inatengenezwa ikiambatana na kemikali
zingine za kiwango maalumu, za kuiwezesha iweze kufanya kazi vizuri. Yaani,
kama ikiundwa protini ya ‘’Enzyme’’ Fulani. Basi moja kwa moja, huwa kuna kuwa
na kemikali kadhaa hasa chembechembe za madini, kama vile ‘’Phosphates,
Sulfates, Sugars na lipids’’, hizi huwepo kwa kiwango maalumu. ili kuiwezesha
hiyo protini iliyoundwa iweze kufanya kazi yake maalumu. au iweze kukamilisha
uundwaji wake, na matendo yake ya kibiolojia. Mfano wa kuelewa hizi kemikali,
ni sawa na mavazi yako. Kila mtu huwa ana nguo za kumfiti yeye vizuri, kuanzia
nguo za juu, za ndani mpaka viatu. Kwa uwezo wako na saizi yako. Na ndivyo
zilivyo pia protini.
Tatizo
La Protini Kwa Genetic Engineering
Mwili wote una viwango
vinavyolingana, ni kama saizi ya shati lako na suruali au sketi yako
vinavyolingana, na kama mkanda utakua mdogo sana, kuliko suruali iliyokubwa
sana. basi tayari mtu hataweza kuvaa nguo zake vizuri, na kufanya kazi zake
vizuri. Sasa hizi protini za kigeni, zinapoundwa katika mwili, huwa na hizi
molekuli zake, zilizo kwa viwango tofauti na viwango vya kawaida vya mwili. Na
kitendo hiki huaribu kabisa utendaji wa kawaida wa matendo ya kibiolojia ya
mwili au ‘’body’s metabolisms’’.
Kila seli katika mwili, ina
kiwango maalumu kabisa cha molekuli zake za kuisapoti kuweza kufanya shughuli
zake. Na hivyo basi, unapoingiza katika seli vitu au protini zinazo hatarisha
utaratibu huu, basi moja kwa moja unaziua seli.
Mfano mzuri ni namna protini
zilezile zilizo katika Ini, na zilizo katika Ubongo, huwa zina viwango tofauti
kabisa vya molekuli zinazozinguka, au kuziwezesha.
Nani anayejua kuwa molekuli
kutoka kwa hizi ‘’genes’’ mpya, ambazo zitaongezwa katika mmea au mnyama,
zitasababisha nini katika mwili?
Professor Joseph Cummins wa
Jenetikia kutoka Chuo cha Ontario Magharibi aliwahi kusema kuwa ‘’Ukiachana na
Ushahidi uliopitiliza juu ya hatari za njia hizi za kijenetikia, Kiwanda cha mabadiliko ya kijenetikia ‘’biotech
industry’’ kina namna moja tu ya kuamua
kufanya makisio kuwa, Wanyama wao wanaowaongezea genes, hawataathiriwa na
spliceosome, na zaidi ya hivyo, basi hizi njia ni za hatari sana’’
Uwepo
Wa Viboresha Protini ‘’Chaperones’’
Ukiachana na ushahidi ambao
tumekwisha kuuona, lakini pia umbile la protini, lina maana sana. Hapo zamani
kulikuwepo na nadharia ambayo, ilikuwa inaamini kuwa, Baada ya Protini kuundwa
kutoka katika mabadiliko ya kijenetikia, basi huwa ina tengenezea umbile lake
yenyewe. Hii iko hivi, siku zote protini huwa inaundwa kama likambakamba Fulani
hivi, halafu baada ya muda hubadilika na kuumba umbile maalumu la protini
Fulani. Sasa basi, hapo zamani walikuwa wakihisi labda mabadiliko haya
hujiongoza yenyewe, lakini kadri muda ulipokuwa ukiendelea ndipo wakagundua
yafuatayo
Miaka ya 1980 iligundulika
kuwa, protini ikiwa peke yake huwa na umbile lisilo rasmi ‘’misfold’’ na huwa
haiwezi kufanya kazi ‘’inactive’’ mpaka itakapo kutana na aina maalumu ya
protini inayoitwa ‘’Chaperones’’, hii chaperone huiboreshea umbile lake au hui
‘’folds’’.
Mtu akitaka kujibu kuwa
itabadilishwa na ‘’Chaperone’’ ya mnyama mpya, swali litakuja je, unaweza
kubadilisha kitu ambacho hukifahamu?
Yaani chaperone haijawahi iona hii protini sasa itaibadilishaje?
Dr.Peter Wills wa Chuo cha
Auckland alionya kuwa ‘’ Protini ya kawaida ya seli itakayo kunjwa vibaya,
inaweza katika mazingira Fulani kujizalisha mara mbili, na kuzalisha maambukizi
au magonjwa yatakayo ushambulia mfumo wa Ubongo’’ na mfano wake ni magonjwa
yanayoitwa ‘’mashambulizi ya Prions, ambazo hizi prions ni aina ya hizi
protini. Ambazo, hupelekea ugonjwa wa kichaa cha ng’ombe au ‘’mad cow
disease’’. na ugonjwa hatari ‘’deadly creutz field Jacob disease’’ kwa
binadamu.
Kwa hiyo hapa, ni muhimu
kutambua kuwa, hizi protini zinazozalishwa katika mwili, ambazo sio asili za
mwili, zinapochakatwa na chaperone, huweza kupelekea uzalishaji wa sumu hatari
sana kwa afya za watu.
Namna yoyote ya kuingiza genes
mpya kwa viumbe, huisababisha DNA mithili ya mtikiso. Ambao, utaaribu mfumo au
mfuatano mzuri wa taarifa uliokuwepo awali. Zipo namna mbalimbali za kuweka
gene katika DNA, na hizi namna huwa zikibadilika kadri teknolojia na maarifa
yanapoongezeka, lakini kumbuka kuwa bado hatuna maarifa ya kutosha kuhusu
jenetikia.
namna
kadhaa za kuingiza genes katika dna
Kulipua mchanganyo wenye gene,
ili gene iingie au ipenye kuelekea kwa DNA. Hapa hutumika mithili ya bunduki
‘’22 caliber gun’’ ambapo hapa, wanasayansi huchanganya kiwango kikubwa cha
kemikali za kulipuka, zenye vipisi vya dhahabu au tungsten na gene yao
wanayoitaka kuiingiza kwenye DNA. kwa hiyo, hivi vipisi huviweka kwenye Dishi
na maelfu ya seli na kisha hulipua. Na baada ya kulipua, hutegemea kuwa genes
zitapenya na kuingia kwenye seli, mpaka kwenye DNA. Na kwa mantiki hiyo hiyo,
hii aina ni sawa na kutaka kutumia bunduki, kuingiza dawa mwilini ikiwa kama
risasi.
Madhara ya spidi kubwa,
vipande kutoka mlipuko huu, moja kwa moja, huenda kuathiri mpangilio, na umbile zima la DNA. Na kibaya
zaidi ni kuwa, madhara haya yanayotokea katika DNA, ni vigumu sana kuyagundua.
Mwalimu wa Sayansi ya namna za
uharibifu wa viwango vya chini kabisa vya magonjwa au ‘’Molecular Pathology’’,
na mkuu wa Kitendo cha Utafiti wa Hospitali ya Ualimu ya London, bwana Michael
Antonious alisema kuwa ‘’Hii namna hupelekea madhara ya uharibifu katika
vinasaba vya jenetikia vya kiumbe, katika namna isiyo tarajiwa au fahamika
kabisa’’.
kuna namna ya kutumia ‘’Chip
Technology’’.ambayo hii inawawezesha wanasayansi kuratibu mabadiliko katika DNA baada ya
kuingiza genes mpya. Katika moja ya majaribio kulikuwa na uharibu wa asilimia
5% wa uwasilishaji wa genes au ‘’gene expression’’, hii ina maanisha kuwa,
katika kila gene moja waliyoiongeza, kulikuwa kuna gene moja kati ya 20 genes,
ambayo ilikuwa inaunda protini aidha kwa kiwango kilichozidi wastani, au
kilichopungua wastani.
Mwanasayansi ‘’Schubert’’
alisema pia kuwa ‘’Ijapokuwa mabadiliko haya tusiyoyatarajia katika utendaji wa jenetikia, hasa ‘’gene
expression’’ ni ya kweli sana, lakini hakuna anayeyazingatia sana katika jamii
ya watumiaji wa Chip za DNA.
Kwa hiyo hizi genes,
zinapokuwa zikiingizwa katika DNA, huwa zikipelekea mabadiliko ya kijenetikia.
Ambayo, yanaitwa ‘’Insertion mutations’’ na miongoni mwa madhara ya aina hii,
hupelekea utokeaji wa saratani kama vile saratani za damu ‘’leukemia’’. na aina
zingine za visababishi vya saratani, au ‘’insertion carcinogenicity’’.
Kufeli
Kwa Dawa ‘’Antimicrobial Resistance’’ Na Kusambaa Kwa Genes Mpya
Kama tulivyoona hapo juu
kidogo, baada ya kuingiza genes mpya katika DNA, genes ni chache sana ambazo
hufika kabisa katika DNA. Nyingi ya hizi genes huishia katika sehemu zingine.
tatizo na lilipoanzia
Kumbuka kuwa mara nyingi
wanapokuwa wakitaka kuingiza genes katika DNA ndani ya seli. huwa wanatumia
njia ya mlipuko kama tulivyoona, sasa basi, watakuwaje na uhakika kuwa ile gene
imeingia katika sehemu maalumu au DNA. Basi ile gene walikuwa wanaichanganya au
iweka Pamoja na chembechembe ambazo haziwezi zuilika na dawa. Hizi zinaitwa
‘’Antibiotic Resistant Marker’’ au ‘’ARM’’,
‘’hizi ni sawa na namna zilivyo zile ‘’antidote’’ ambazo hata kama
ukipewa sumu, ukipewa antidote yake basi haudhuliki’’ kwa hiyo sasa, hizi
zinapolipuliwa kama zitafanikiwa kuingia mpaka ndani kabisa ya seli, basi na
genes nazo zitakuwa humo ndani kabisa ya seli. Sasa basi, hawa jamaa ili kuziua
zile seli zingine ambazo genes hazijaingia kisawasawa, basi hujaza kiwango
kikubwa sana cha dawa, au ‘’Antibiotics’’, na hivyo seli zote zisizo na hii
‘’ARM’’ hufa na zile zenye ‘’ARM’’ huendelea kuishi.
tatizo
kwa kutumia antibiotic resistant marker
Hizi genes zenye ‘’ARM’’ au
molekuli za kujikinga na maangamizi ya dawa, zinapokuwa ndani ya seli ya mnyama
au mmea, na kuendelea kuzaliana na kusambaa na hata kuingia kwa Bakteria.
Kitendo cha kuingia kwa Bakteria. moja kwa moja, hupelekea kutokea kwa bakteria
ambao, hawadhuliki na dawa. hii ni sawa na kusema kuwa, tayari unakuwa na
bakteria ambao wana antidote za dawa ambazo tunazitumia.
Unapokula Chakula ambacho
kimetengenezwa kutoka kwa bidhaa za kemikali hizi za kijenetikia, basi
hupelekea moja kwa moja wale bakteria wanaokuwaga tumboni, kupata hizi genes za
kuzuia dawa. Na hawa huweza kuzipata kutokana na tabia za genes, kusambaa kwa
aina inayoitwa ‘’Horizontal gene transfer’’, na hii hupelekea viumbe hatari
wasiotibika.
Kujitetea Kwa Biotech Industry
Hawa walijetetea kuwa, jamii
isiwaze kwa kusambaa kwa genes za kukinzana na dawa. kupitia chakula, na
bakteria, kwa kusema kuwa, genes hizi na DNA zinapokuwa tumboni, humeng’enywa
moja kwa moja na vimeng’enya katika tumbo.
Kufeli
Wa Mtazamo Wa Ge Juu Ya Arm
Mwaka 1980 iligundulika kuwa,
sio tu kuwa DNA iliweza kutomeng’enywa na vimeng’enywa vya tumboni, bali pia
ilionekana kusambaa katika Damu, kwenye Utumbo, Ini, Bandama na Kinyesi, na
hata mabaki zaidi yalionekana katika kuta za tumbo. kwa siku tano.
DNA zilionekana pia kusafiri
kupitia Placenta mpaka kwa panya ambaye bado hajazaliwa.
Mwaka 2002 waligundua mabaki
ya chakula, au kinyesi, yana mabaki ya molekuli au chembechembe za DNA,
zilizofanyiwa mabadiliko ya kijenetikia ‘’G.E’’ kwa watu saba, ambao walikuwa
wanashida za mfumo wa haja kubwa, walikuwa wakitumia tu ‘’mabegi ya kujisaidia’’
au ‘’Colostomy bags’’
Na pia ilionekana kuwa, mabaki
hayakuonekana tu baada ya kula, na hivyo ikaonekana pia, matumizi ya muda mrefu
zaidi huongeza hatari zaidi ya kujaliwa na molekuli za bidhaa za mabadiliko ya kijenetika, au
‘’Genetic modified oirganisms’’ G.M.O
Mfano mahindi yenye protini
sumu za kujikinga ‘’Bt’’.ambayo, yametengenezwa kwa njia hizi za kijenetikia
‘’G.E’’. yameonekana kuwa na genes za ‘’ARM’’ za kujikinga na dawa ya
Ampicillin.
Shida Ya Switch Za Kijenetikia ‘’Promoter ‘’
Gene ya kutengeneza rangi ya
Bluu, au Kahawia ya kiini cha macho. itakuwa ikiwa ON sehemu ya kutengeneza
rangi hii tu, lakini haitakuwa ON sehemu unohitajika weupe wa jicho. Na ndiyo
maana, kuna sehemu kuna protini Fulani, na sehemu nyingine hazipo. Ijapokuwa,
kila seli ya mwili ina DNA yenye maelekezo ya kuunda tishu au kitu chochote
kile. Hii inatokana na uwepo wa chembechembe hizi zinazoitwa ‘’Promoter’’. hizi
ndizo huwasha mtambo wa jenetikia ya ujenzi wa kitu Fulani, au huweza kuzima.
Huyu bwana asipozuiliwa.
Mfano, yule wakutengeneza au kuchochea kutengeneza rangi nyeupe ya Jicho, basi
matokeo yake, yangekuwa mwili wote ungekuwa mweupe.
Nani anayetoa maelekezo ya
kuwa wewe Promoter sasa fanya kazi hii? Au hebu Tulia hapa? Au hebu ongeza hapa
au punguza? Bila shaka hapa jibu ni seli
mwenyewe, na haya maelekezo hatuwezi jua hasa yanapotokea.
changamoto
Unapoweka gene mpya katika
seli, je ni nani anayetoa maelekezo kuhusu utendaji wa gene hii mpya. Je ni
promoter za seli! ndizo ambazo zitaongoza utendaji wa seli hizi? Moja kwa moja
ni kuwa, seli haitatumia promoter zake kuhangaika kuongoza uundaji wa genes
usiozifahamu, na maana yake, mradi mzima wa jenetikia ya hizi genes hufeli.
Suluhisho
La G.E Ambalo Ndiyo Mauaji Ya Jenetikia Ya Mwili
Hawa bwana huiweka gene Pamoja
na Promoter yao. Kama ni gene ya kutengeneza protini ya kuua wadudu. Basi
huiweka na Promoter ya Kwenda kuichochea, ikifika katika mwili wa viumbe.
Uchaguzi wa Promoter hapa ni changamoto kubwa sana. hii ni kwasababu, siku zote
seli huwa ikijikinga na chembechembe au molekuli ambazo, zinaweza lenga katika
kubadili DNA yake. Huu ni mfumo wa ulinzi wa seli, kwa hiyo kama utaweka
Promoter, tegemea uwezekano mkubwa sana wa hiyo Promoter, kuzimishwa na seli za
mwili wako. hawa jamaa hutafuta Promoters kutoka kwa Virusi na seli za cancer.
Wanabiolojia hawa huchukua
promoters kutoka kwa virusi, na cancer. kwasababu kubwa moja, ambayo ni hii,
siku zote virusi huwa na sifa za kuteka mfumo wa seli za mwili au mimea, na
ndiyo maana, ni vigumu sana kujikinga na magonjwa ya virusi baadhi. kwa kuwa,
hawa huweza kutumia mfumo wa seli kufanya kazi zao wenyewe za kujizalisha, na
ndivyo ilivyo hivyo hivyo kwa seli za cancer.
Mfano watu hawa hutumia
Promoter kutoka kwa Virusi wa ‘’Cauliflower Mosaic Virus’’, na kifupi huitwa
‘’CaMV Promoter’’, hizi promoter hutumika kuhamasisha mabadiliko ya
kijenetikia, kwa seli za mimea. bila kuathiriwa na mfumo wa kujikinga wa mmea.
Hizi promoter zinazoweza
kuwasha mtambo wa seli, bila kuingiliwa. zinaweza kufanya kazi zake, bila
kuathiriwa na mifumo ya utendaji wa seli. na pia, hufanya kazi bila
kurekebishwa na seli, kwa namna yeyote ile.
Wanabiolojia kadhaa huonya
kuwa, kwa mfano, mimea huitaji Nishati, na Malighafi zake, katika kuwasha mfumo
wake Fulani wa jenetikia. na kuutuliza mwingine. lakini matumizi ya hizi
promoters, huwasha mifumo ya seli mfululizo, na kibaya zaidi hakuna anayejua,
mifumo ipi hutelekezwa?
Daktari Psutzai na timu yake
ya Utafiti waligundua kuwa, Promoter hizi huwa
hazina uimara, hazina mipangilio maalumu, na zina utendaji wa hatari
sana. unao athiri mifumo ya kinga, na viungo, kwa panya wao waliowafanyia
utafiti.
G.E Na
Kuamshwa Kwa Hatari Zilizolala
Hizi Promoters kwa kuwa huwa
zinaamsha amsha tu mifumo ya seli, basi huwa zikiamsha hata virusi ambao
walikuwa wametulia bila madhara, na kuwafanya waanze kuwa hatari tena, lakini
pia mwilini. kuna genes nyingi sana ambazo, hazipaswi kuamshwa. kama vile,
genes za magonjwa. lakini matumizi ya hizi Promoter, huamsha hizi genes, na
kupelekea madhara makubwa sana kwa utokeaji wa hatari za ajabu sana, na
kuathiriwa sana kwa miili yetu.
Hakuna namna za kuweza
kuziongoza au kuratibu hizi Promoters.
Madhara
Ya Mahali Ambapo Genes Hizi Hutua
Hizi genes zinapoingia katika
DNA, huwa haifahamiki kuwa zitatua wapi. Na madhara yake ni kuwa, zinapoingia
na kutua katika sehemu Fulani, ambayo, ilikuwa tayari na gene Fulani, basi
huaribu kabisa tabia Fulani. ambayo, ilikuwa ikiratibiwa na ile gene.
Ijapokuwa husemwa kuwa, yapo
maeneo katika DNA ambayo hayana gene. na unaweza kuweka hapo hizi genes za
kigeni, katika DNA, lakini matokeo yanaonesha, si kweli kuwa kuna sehemu zisizo
na kitu ‘’junk DNA’’, ila ni kuwa, sisi ndiyo tuliokuwa hatujui, ila kila
sehemu ina kazi yake.
Miongoni mwa madhara haya ni
pale ambapo, gene hizi huweza kupelekea kuzimishwa kabisa katika mtambo mzima
wa DNA, wa kuzalisha genes
Mwanasayansi Michael Hansen, pia aliwahi kusema kuwa ‘’kama itawekwa gene ambayo inaweza kupelekea kuzima kwa mtambo mzima wa gene, ya uzalishaji wa chembechembe za kupambana na sumu mwilini. maana yake, matokeo makubwa kabisa tutakayo yapata ni kujaa kwa sumu mwilini.’’
Madhara
Ya Kusambaa Kwa Genes Hatari
Mwaka 2003, watu 39 waliokuwa
wanaishi pembezoni na mashamba ya mahindi, yaliyokuwa yameboreshwa kijenetikia
huko Ufilipino, walionekana kupatwa na changamoto kubwa sana za matatizo ya
upumuaji, Matatizo katika utumbo, na shida za Ngozi. Na matatizo haya
yalionekana kutokana na kutoa Pollen kwa mahindi.
Taasisi ya Norwegian ya
Jenetikia katika Mazingira ‘’Gene
Ecology’’ ilidhihirisha kuwa, changamoto hizi zilitokana na mwili kuhangaika
kujikinga na sumu zilizopandikizwa, kwa kuwekwa kwa genes katika mahindi, za
kuzalisha protini sumu kwa wadudu. Na hivyo sumu hizi, kusambaa kwenye pollen
za mahindi.
Kuhusu
Kirusi Wa Camv Promoter
Nikimnukuu MaeWanto ambaye ni
mtaalamu wa jenetikia, na Biofizikia katika Open University UK. ‘’Hawa virusi
kwa asili, huwa wanapatikana kwa mimea, au mbogamboga tu kwa asili, na huwa
hawawezi kuathiri Wanyama, kwa kuwa, huwa wana koti la Protini kuzunguka DNA
zao, lakini hawa wanaotumika katika mabadiliko ya kijenetikia, huwa wametolewa
lile koti na kuwa na DNA iliyo wazi. na hivyo kuwa na uhuru, wa kufanya lolote
bila kuzingirwa.’’
Na pia miongoni mwa makisio
ambayo wanabiolojia hawa huyatumia, lakini sio sahihi. ni kuamini kuwa, matokeo
ya gene Fulani kwa mnyama Fulani, yatakuwa yaleyale kwa mnyama mwingine, kitu
ambacho kinaweza kisiwe kweli kabisa.
Hii ni kwamba, protini ileile.
lakini kwa Wanyama tofauti, au Wanyama na mmea, au mmea na bakteria, inaweza
kuwa ikitengenezwa kwa genes zilizopishana maelekezo. katika namna Fulani. Na
hivyo basi, teknolojia hizi, huusisha kubadilisha maelekezo haya ili kufikia
lengo lao.
Unaweza kuweka gene ile ile
kwa aina mbalimbali za viumbe, ikaleta matokeo tofauti tofauti. Mfano, kwa
mimea utakuta unapata matokeo tofauti na ambayo unapata, katika Wanyama
wengine.
Sababu za swala hili bado
hazijafahamika! lakini kuna kisio la viwango tofauti tofauti, huweza
kuhamasisha matokeo tofauti tofauti.
Kuharibu
Mfumo Mzima Wa Uhusiano Wa Mwili
Unapoweka gene Fulani kwa
kiumbe mwingine, unabadilisha mfumo mzima wa
matendo ya kibiolojia ya huyo kiumbe.
Hufahamika kuwa, genes
huusiana na genes zingine. genes huusiana na protini. Lakini pia Protini
huusiana na Protini zingine. Kwa hiyo, kusababisha mabadiliko yoyote yale ya
genes, huweza kupelekea mfululizo wa uharibifu kiutendaji wa mwili mzima.
Kuharibu
Mfumo Wa Code Za Mwili
Matendo haya ya kuinjinia
jenetikia ya mwili. huaribu mfumo wa upangiliaji wa taarifa za jenetikia za
mwili. Neno ‘’code’’ lina maanisha mpangilio maalumu wa bases za DNA, ambazo,
hutoa taarifa kuhusiana na uundaji wa protini Fulani tu. Na sasa basi, hizi G.E
zimeonekana ijapokuwa kwa sababu zisizo fahamika sana, hupelekea kubadilishwa
kwa code hizi za utu wa watu.
Kujaa
Kwa Genes Mbalimbali ‘’Gene Stacking’’
Mfano, aina moja ya Viazi
kutoka kwa kampuni la Monsato, vinavyoitwa ‘’monsato’s new leaf potatoes’’,
zilikuwa na sifa 8 tofauti tofauti, kutoka genes mbali mbali. kama vile,
zilikuwa na ‘’sumu ya kujikinga na wadudu ‘’own pesticides’’, kujikinga na magonjwa,
kuvumilia viua mimea ‘’herbicide tolerant’’, kuongeza uzito, na kupambana na
michubuko.n.k. na mimea mingine, ilionyesha kuwa na genes nyingi zaidi, kupitia
kusambaziana pollen ‘’cross pollination’’
Na hata ilionekana kitendo
hiki cha kusambaziana hizi genes, kunazifanya ziwe na sumu yenye nguvu sana, au
hata pale ambapo ilionekana mfano, sumu ile ya Bt iliyowekwa kwenye Mahindi ya
GM, ikichanganyika kidogo tu na kemikali za antibiotiki kutoka kwa bakteria.
basi sumu yake inakuwa hatari sana kwa wadudu.
Lakini huwa hawafanyi vipimo
vya kujua nguvu ya sumu hizi, inavyokuwa kwa binadamu.
Kubadili
Viwango Vya Virutubisho Kwa Mimea
Badiliko la DNA, ambalo limelengwa au halijalengwa,
limeonekana kubadilisha kiwango cha virutubisho vilivyopo katika mmea.
Masomo mbalimbali yamezigundua
tofauti zilizopo kati ya mimea ya asili, na mimea iliyobadilishwa kwa
mabadiliko ya kijenetikia.
Mfano maziwa ya Ng’ombe
waliolishwa Soya iliyobadilishwa kijenetikia, kwa kuwekewa gene ya kujikinga na
Roundup, yalikuwa na mafuta mengi, ukilinganisha na maziwa ya ng’ombe wa
kawaida.
Ukisikia allergy, ujue moja
kwa moja mwili umeshtushwa sana, na molekuli hizo zilizokutana nazo. kiasi cha
kusisimka sana, na hata kuweza kupelekea ugonjwa. Visababishaji hivi vya
allergy huwa vinaitwa ‘’allergens’’
Na mabadiliko haya ya
kijenetikia, huweza kupelekea kiwango kikubwa cha allergens, kwa kuongeza
kiwango cha allergens. au kusambaza genes zitakazo pelekea allergy, au kwa
kuchanganya genes. na kupelekea kuundwa kwa molekuli, ambazo, zitakuwa sumu na
kupelekea allergy.
Matatizo
Ya Kibinadamu Na Giza La Maarifa
Hakuna maarifa makubwa tuliyo
nayo kuhusiana na utendaji huu wa jenetikia. Na jambo hili limekuwa likipelekea
sana kufanyika makosa, ambayo, baada ya teknolojia kuongezeka kidogo. ndiyo
huwa yakigundulika kuwa yameathiri watu. Lakini pia watu wengi kutokuweza kujua
madhara ya makosa haya ya kijenetikia, ni rahisi kukimbilia matatizo mengine
kabisa. ambayo hayahusiki, lakini wasijue wapi hasa tatizo lilipoanzia.
Mwaka 2003 mwezi wa pili,
karibia Nguruwe 400 huko Marekani waliokuwa wametoka kufanyiwa majaribio haya
ya kijenetikia, waliingizwa katika soko la chakula! badala ya kuuwawa. Na watu
pasipo kujua, wakawanunua wote kwa lengo la chakula.
Monsato pia wamefanya matatizo
mengi sana ambayo yamegharimu sana afya za watu na yanaendelea.
|
|
Mwandishi na Mwenyekiti
Mtaalamu wa sayansi ya wanyama, mwanabiofizikia, na mwandishi wa vitabu vya kisayansi. Mwanzilishi wa Injili ya Sayansi — taasisi inayounganisha maarifa ya kisayansi na imani.
Shiriki makala hii
35 min
82 min
6 min