Inapakia...
Inapakia...

Dr Brighton Shoo
Mwandishi na Mwenyekiti
“SIKU YA PILI 02 6. Mungu Akasema, Na Liwe Anga ‘’Firmament’’ Katikati Ya Maji, Likayatenge Maji Na Maji. Mwanzo 1:6 Neno ‘’Anga-Firmament -Expanse -Raqia’’ Kama kuna sehemu inahitaji Teolojia ya manen…”
SIKU YA PILI 02
6. Mungu Akasema, Na Liwe Anga ‘’Firmament’’ Katikati Ya Maji, Likayatenge Maji Na Maji. Mwanzo 1:6Neno ‘’Anga-Firmament -Expanse -Raqia’’
Kama kuna sehemu inahitaji Teolojia ya maneno ni hapa. kwa kuwa ina utata sana wa maana za hayo maneno niliyoyaandika hapo juu. Na hapa pamepelekea kuibuka kwa nadharia Tatu za Kisayansi za Uumbaji wa Mungu. Ila shida iko zaidi kwa wasomi ambao siku zote huuzunguka zunguka ukweli. hasa kwa kutotaka changamoto juu ya mitazamo yao, maana ukweli huwa na Nguvu, hata kwa kushikiliwa na wachache. Nadharia zote mbili zilizouzunguka ukweli huu nitakao usema zimefeli kisayansi. hebu tuangalie kifupi mantiki ya maneno haya.
Neno hilo Anga limetafsiriwa toka neno la Kiebrania ‘’Raqia’’. Ambalo kwa Kiingereza linatafsiriwa kwa maana mbili ‘’Firmament’’ au ‘’Expanse’’. Neno hilo la Kiebrania ‘’Raqia’’ kama likifuatiwa na neno la kiingereza ‘’of the heavens’’, basi humaanisha ‘’Anga, Mbingu, Space au Mbinguni’’. Ila likitumika lenyewe peke yake, humaanisha ‘’Ardhi ya Dunia’’ au Earth’s Crust. Maneno ya Kiebrania yenye mzizi mmoja na neno Raqia, ni Raqa, baqia na baqa. Na maneno haya yote yatumikapo humaanisha Kitu Kigumu ‘’Solid’’ kama Dunia, na sio Anga. Mfano, neno raqa limetumika katika Hesabu 16:38 na 16:39 kumaanisha vyuma vilivyopondwa.
Watafsiri wa King James walitafsiri neno Raqia kama ‘’Firmament’’. ambayo kama una Biblia ya KJV ya kiingereza, unaweza ona hilo neno limeandikwa ‘’firmament’’. neno hilo lina maanisha, ‘’Kitu kigumu, yabisi, Solid, Firm’’.
Neno hili Expanse ‘’Raqia’’ limetumika mara tisa katika kitabu cha mwanzo, na zote katika uumbaji. Mara nne za kwanza zote hazijaongezewa neno ‘’of the heavens’’. Kumaanisha kinachozungumziwa ni Dunia. na ndiyo maana, hata siku zinazofuatia tutaona uumbaji wa mimea na sayari n.k. ambavyo ni vitu vinavyohusiana na nchi, na sio anga. Mara nne zote za mwisho, zimeongezewa ‘’of the heavens’’ kumaanisha kilichozungumziwa kinahusu ‘’anga, mbingu, space’’.
Kutumia neno Raqia lenyewe katika fungu hili kumaanisha Anga kutaleta changamoto ya maswali yafuatayo huko mbele. Kwanini neno Raqia ‘’anga kwa mantiki ya juu’’ lifatiwe na neno ‘’of the heavens’’ kama lenyewe tayari ni heaven? mwanzo 1:9 itasema Maji yakusanyike chini ya ‘’heavens’’ ili pakavu paonekane, kama raqia ni heaven! kwanini isingeandikwa na maji yakusanyike sehemu moja? Mwanzo 1:14 inasema, na iwe mianga ‘’nyota, sayari n.k’’ katika ‘’Raqia of heavens’’ kama raqia ina maana ni heaven, kwanini maneno yajirudie? ‘’Redundancy’’.
Hitimisho La Raqia
Kwa Kiswahili, neno lililopaswa kutafsiriwa ‘’firmament’’, halikidhi vigezo vya neno ‘’anga’’ kwa mara nne za kwanza. kama ilivyo kwa Biblia nyingi za kiswahili. Na kama likitumiwa msomaji anapaswa kujua neno Anga, halina Ushahidi wa kutumiwa kumaanisha ‘’Anga kama sehemu ya wazi ‘’Space’’, kwa siku ya kwanza. maana ni neno linalomaanisha kitu kigumu, kama Biblia ya King James version ilivyoandika ‘’Firmament au Solid’. na kwa siku za mbele, za kuhusu Anga. wameandika ‘’Firmament of Heaven’’ KJV. Msomaji pia unaweza fatilia Zaidi. Kumbuka shida sio kuwa kuna makosa ya uandishi, ila kuna changamoto ya misamiati, na tafsiri kwa maneno yanayochangamana
Mungu Akaumba Firmament Kutenganisha Maji Na Maji
Katika hii sehemu tunaona namna Mungu anaumba Ardhi kutoka katika Maji. Hakuna mtu mwenye maelezo ya kisayansi ya kuweza elezea hapa. kwa maana hata hayo maji hakuna sayansi inayoweza elezea mwanzo wake. Hatuwezi kuelezea, ila kuna Ushahidi ufuatao kuonesha kuwa iliumbwa na Mungu. hii ni kama wewe unavyoweza kuwa hujui namna transistors kwenye CPU ya simu yako zinavyofanya mahesabu ya ‘’Boolean calculations’’ ambayo yanawezesha kufanya wewe uone hiyo sms unayoandika, ila una Ushahidi wa kujua ya kuwa imetengenezwa na watu, haijatokea tu kimaajabu.Miamba Ya Granite.
Granite ni miamba ambayo inapatikana kwa kiwango kikubwa sana katika sehemu ya ardhi ya dunia ‘’Earth’s crust’’. Miamba hii ndiyo msingi wa sehemu yabisi ya dunia. Leo hii miamba hii hupatikana kwa kiwango kikubwa sana katika maeneo baadhi, kama Milimani, au sehemu za chini ya ardhi. Hii ni kutokana na kuwa, miamba hii imefukiwa sana na miamba ya mabaki ya lava ‘’sedimentary rocks’’. baada ya gharika ya nuhu kama tutakavyoona huko mbele. Miamba hii ya Granite huundwa na madini muhimu Zaidi manne.-Quartz. Hii huchukua asilimia kubwa Zaidi ya Granite. Huundwa na chembe za silicates
-Feldspar
-Mica na Hornblende.
Miamba hii ya Granite kitu cha kushangaza Zaidi kuihusu ni namna ambavyo hakuna namna ambayo sayansi yoyote ile ikiwemo sayansi ya miamba ‘’Geology��’ inaweza ielezea uundwaji wake. Hakuna anaeweza elezea au kuunda miamba hii ya granite. Granite ni ya ajabu sana kwa maana ukijaribu kuelezea uumbaji wake kwa kupitia matokeo ya kuganda kwa Lava au ‘’Magma’’ ambayo huwa ndiyo msingi wa uundwaji wa miamba kama ‘’Igneous Rocks’’, mfano miamba ya ‘’Basalt’’, Hufeli kama nitakavyoonesha mbele kidogo. pia ukisema ni kama Sedimentary Rocks, ambayo nayo ni matokeo ya mabaki ya miamba mingine kama lava, ila ambayo huunganishwa au kuwa ‘’cemented’’ na madini kama ‘’Quartz’’.mfano miamba ya ‘’Sandstone, Limestones’’ n.k .nayo nadharia hii hufeli pia. kama mtu angesema ni miamba ya metarmorphic. ambayo yenyewe huundwa kwa matokeo ya mgandamizo, au joto kubwa, kiasi cha kubadilisha mpangilio wake wa awali. Mfano miamba kama ya ‘’Marble’’. na hata miamba ya almasi au ‘’Diamond’’. japokuwa wengi hupinga hili, lakini huko mbele tutaona upana wake Zaidi. pia mtazamo huu hufeli.
Granite ukiiweka kwenye maji yenye joto sana, huyeyuka. na inapoganda haiwi tena granite. ila huwa miamba ya Rhyolite. Yaani Granite ni kama keki ambayo kama ukiikoroga kwenye maji ya moto, halafu uje kuyakausha maji. haitabaki keki tena.
Kama unavyoona hapo juu miamba hii miwili. hiyo granite ukiiyeyusha haitakuja kamwe kuwa tena granite, itakua hiyo rhyolite. watu wa nadharia ya evolution huchanganyikiwa maana wao husema dunia zamani ilikuwa ujiuji, sasa hii miamba imetoka wapi?
Mungu aliumba miamba ya Granite. Soma haya mafungu na uone ni elimu ya uumbaji ambayo bado hatujaifikia.
Ayubu 38:4 ‘’Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! sema, kama ukiwa na ufahamu.’’ Ayubu anaulizwa kama anajua kuelezea uundwaji wa Granite. Ayubu alishindwa kama sisi leo. Fungu hili linatoa namna Mungu alishaona miongoni mwa vitu ambavyo kamwe binadamu tutajifunza, ila hatutaweza kuelewa ni hii miamba.
Kuna vitabu vina vichwa vimeandika ‘’uundwaji wa Granite, lakini mwanzo mpaka mwisho hakuna maelezo’’. mwanajiolojia mkubwa sana ‘’Robert Gentry’’ katika kitabu chake cha ‘’Tiny Mystery’’ anaelezea namna miamba hii, inahusiana na maajabu yasiyoelezeka yanayo mnyooshea kidole Muumbaji Mwenyewe. na sio Lava iliyopoa, wala nadharia yoyote ya mabilioni ya dunia.
Zaburi 104:5 ‘’Uliiweka nchi juu ya misingi yake, isitikisike milele’’. Neno ‘’laid the Foundations of the earth’’ linakidhi kueleza ni maarifa yalitumika, sio matokeo ya kazi nyingine.
Mithali 8:29 ‘’Alipoipa bahari mpaka wake, kwamba maji yake yasiasi amri yake; Alipoiagiza misingi ya nchi; ‘’ neno alipoiagiza misingi ya dunia, linaleta maana ile ile ya uumbaji wa kitaalamu. na sio matokeo ya matukio mengine.
7.Mungu Akalifanya Anga ‘’Firmament’’ Akayatenga Yale Maji Yaliyo Juu Ya Anga Na Yale Yaliyo Chini Ya Anga; Ikawa Hivyo. Mwanzo 1:7
Hapa kuna watu kama nilivyosema awali, walitumia neno ‘’Raqia’’ moja kwa moja kama ‘’Raqia of the heavens’’. matokeo yake ni kuwa. ikaonekana kana kwamba Mungu akawa amefanya yafuatayo
Nadharia Ya Russel Humphreys Ya Anga ‘’Hewa’’ Badala Ya Anga ‘’Yabisi’’ Au Firmamnent
Iliwasilishwa na ‘’PhD Physicist Dr. Russel Humphreys, Professor at ICR America, alipitia Electric and Sandia National Laboratories na ni mgunduzi na mshindi wa Tuzo kadhaa za sayansi’’
Hii ni picha ya kielelezo chake, maji yakizunguka ulimwengu na dunia ambayo ni ndogo hata haionekani. ila unaweza ona galaxies. hizo ice au barafu anamaanisha kwasababu nje kwenye space kuna baridi sana, basi kuna maji yameganda.
Huyu mwanafizikia wa kuheshimiwa sana alisema ya kuwa Mungu alitanua Anga tokea kwenye maji. Anga hili lilipotanuka liliumba ‘’Space’’ambayo ndiyo msingi wa uumbaji wa sayari, na nyota hapo baadae. Na Anga hili lilitanuka kwa kiwango kikubwa ajabu, kuumba hili eneo la umbali wote wa mabilioni ya miaka ya mianga ‘’Light years’’.
Light Years Ina Maana Gani?
Kama ungeambiwa upime umbali ambao Kundi Fulani la nyota na sayari ‘’Galaxy’’ lipo tokea duniani, usingeweza kirahisi, hii ni kwa maana ni umbali mkubwa ajabu kwa kuuweka kwa vipimo vya mita ‘’metric system’’. Hivyo basi hapa hutumika kanuni hii, Umbali ambao mwanga ungetembea kwa mwaka mzima ni umbali wa karibia Kilomita Trilioni 9.461. kwa sababu spidi ya mwanga inafahamika ambayo ni 299,792 kilomita kwa sekunde. Sasa basi, kwa kuwa hizi Galaxy huenda mbali na Dunia kama inavyoaminiwa ya kuwa ulimwengu unatanuka. basi kadri zile Galaxy zinavyozidi kwenda mbali hupelekea kuzalishwa kwa mawimbi mekundu ‘’Redshift’’ ambayo haya sasa, wana anga hupima ‘’wavelengths zake’’ kwa kutumia kifaa kinachoitwa ‘’Spectroscopy’’. na baada ya kupata wavelengths zake, hulinganisha na wavelength za mianga ya maabara ‘’laboratory standard values’’. na baada ya hapo, hutafuta ‘’Doppler effect’’ ambayo hii ni namna ya kujua spidi ya galaxy kwa kulinganisha tofauti ya wavelengths zake zinazopimwa maabara, na zilizopatikana kutoka kwenye vipimo, hii hutuwezesha kupata spidi ambayo zile Galaxy zinatembea. na matokeo yake, tukishapata spidi, tunatafuta umbali wa hizo galaxy kwa kuingizia kwenye kanuni ya bwana Hubble ‘’hubble’s law’’. hiyo hugawanya spidi kwa constant ya hubble ili kupata umbali ambao ndiyo huwa katika namna ya light years. Zipo namna baadhi pia, ila hii ndio itumikayo Zaidi.******----------- ---------- --------------*****
Tukirejea kwa bwana Russel, Hii nadharia pia huamini ya kuwa utanuzi wa anga hili ulipelekea kubakishwa kwa baadhi ya maji kama ‘’waterballs’’ katika anga, au space. Ambazo ndizo zilizokuja kubadilika na kuwa sayari na nyota. Bwana Russel Humphreys ametoa Predictions nyingi sana kuhusu nadharia yake ambazo zilikuja kuwa kweli ukilinganisha na predictions za nadharia ya mabadiliko ya wasioamini Mungu ‘’Dynamo theory’’, hasa katika kuelezea Asili ya Usumaku wa sayari Dunia ‘’Origin of Earth’s Magnetic field’’, na zingine kadhaa.
Pia ameelezea namna ambavyo Kutanuka kwa Galaxies katika Space kwa umbali ambao leo tunauona ni mabilioni ya miaka ya mwanga, ‘’Billions of Lightyears’’. isingekuwa sababu ya kuwa ulimwengu ni wa miaka mingi sana nyuma, bali ni matokeo ya spidi kubwa ambayo Mungu aliutanua Ulimwengu. na pia akaweza kuelezea namna Mabadiliko ya muda kipindi cha uumbaji ndiyo chanzo cha utofauti wa muda tunauona kati ya galaxies.
Huyu bwana ameonyesha kuwa kipindi ulimwengu unatanuka, Dunia iliyokuwa sehemu yenye mvuto mkubwa sana wa Gravitation, ilikuwa kama ndoo iliyopinduliwa na maji yakaanza kumwagika kwa spidi kubwa kwenda mbali na ndoo, hii inafanana na ‘’Inflation inayofundishwa katika big bang’’. Sehemu au Galaxy ya Dunia Muda ukawa ukienda polepole sana kwa umbali wa siku wa kawaida sababu gravitation bado ilikuwa kubwa. lakini zile sayari na Galaxy zingine zilizokuwa zikienda katika space kwa spidi kubwa, zilitumia muda mrefu zaidi kama inavyoonekana leo zipo ‘’Billion of light years’’ sababu muda ulikuwa unaenda fasta sana. ili mtu asichanganyikiwe hapa aelewe kuwa, unavyoondoka tokea kwenye gravitation kubwa, ukaenda sehemu yenye gravitation ndogo, basi muda nao huenda fasta sana (kumbuka kituko cha Mapacha ‘’twin paradox’’ anayeenda kwenye Space baada ya miaka tisini anakuwa mdogo kuliko pacha aliyebaki duniani, kwa sababu katika space muda umeenda fasta amefika miaka tisini akiwa mdogo kabla ya mwenzake). Hii katika kitabu cha mwanzo inaitwa ‘’Genesis Time Dilation’’. na ili kwa siku inayofuata baada ya nyota kusafiri mbali na muda kuwa mrefu kutokana na kuwa na spidi kubwa ya muda, ili Adamu aliyepo duniani aone ni uumbaji uliofanyika jana tu, Basi Mungu aliongeza Spidi ya Mwanga mamilioni ya spidi ya kawaida, na kisha akaurejesha katika spidi ya kawaida. aliongeza spidi ya mwanga ili kulipia gap la muda lililotofautiana kati ya dunia na space. maana muda na mwanga huenda pamoja. Kama hujaelewa nimeelezea sehemu Fulani mbele usijali.
Binafsi namshukuru sana bwana Russel Humphreys kwa maana ametoa mchango mkubwa sana ambao umetengeneza njia pana sana ya wasomi wa sayansi ya fizikia,kujua uwezekano wa kujibu maswali ambayo yasingejibika kwa mitazamo ya kifalsafa, kama vile kuamini uumbaji wa Galaxy zilizokamilika ‘’Mature Creation’’, maana ingemfanya Mungu awe kama anadanganya uumbaji wa jana uonekane ni wa miaka mingi sana nyuma. Hii mature creation huwa sahihi katika mantiki kama ya kusema, Mungu aliumba vitu ambavyo tayari vimeshakomaa, mfano alimuumba adamu mtu mzima na hivyo kama ungetokea siku ya sita ukamuona adamu. Ungesema dunia imeumbwa miaka 40 nyuma, mfano ungemkadiria ana miaka 40.’’nimekisia namba’’. Ni kweli kwa mantiki hizi, lakini sio kwa nyota na Galaxy.hiyo itakuwa ni sawa na kukimbia kujifunza.
Kama ilivyo kawaida katika sayansi huwa tunaangalia namna ya kuboresha Zaidi kwa kurekebisha makosa, na kuongezea uwezekano bora Zaidi wa ufahamu. Nadharia hii ina baadhi ya changamoto ambazo zilianzia kwenye lilelile neno Raqia au Anga au Firmament.
Changamoto za Nadharia ya Russel Humphreys
1. Haielezei uumbaji wa sehemu ya Ardhi ya Dunia.
Inaonesha Siku ya pili Mungu aliumba tu Anga. hii inaleta changamoto kwa siku ya tatu. Ambayo maji yatapaswa kukusanyika sehemu moja, ni mithili imepuuzwa sehemu ya ardhi ya dunia.
2. Haileti mantiki kisayansi Mungu kuyatanua maji mbali kuzunguka ‘’space’’. na mpaka sasa kwa umbali wa space uliokwisha pimwa, hata kama badala ya kuchukua nusu, ukichukua maji yote ya dunia ukayatandaza, hayatoshi kabisa kuzunguka space. hata ukichukua gramu moja, ukaitandandaza kwa maili kadhaa, ili ikutane na gramu nyingine haiwezekani. na bado ulimwengu unazidi kuonekana mkubwa Zaidi, na pia hakuna Ushahidi wa maji yoyote yaliyoonekana kuzunguka anga ‘’space’’. na pia haileti mantiki ya maana ya kutanuka kwa ulimwengu.
3.Neno ‘’Raqia’’ peke yake limetumika kumaanisha ‘’Firmament’’ kama King James version’’ ilivyoandika, na kwa mstari wa 8 na 9 wa mwanzo 1. Tutaona Maji yakikusanyika kwenye Firmament. Ambayo Mungu anaiita Mbingu ‘’Heaven’’. yanakusanyika sehemu moja, sasa yatakusanyikia wapi kwa mtazamo huu? Kwa maana hakuna ardhi iliyoundwa.
4. Nadharia haitoi maelezo mazuri kuhusu ujio wa sayari, na galaxies ‘’heavenly bodies’’
5. Nadharia inatumia Ushahidi wa fungu la zaburi 148:4 ‘’Msifuni, enyi mbingu za mbingu, Nanyi maji mlioko juu ya mbingu” akasahau mstari wa 3 unasema ‘’Msifuni, jua na mwezi; Msifuni, nyota zote zenye mwanga’’. Kumbe hapa vinatajwa vilivyopo kwenye space. Akasahau kuna Quasars zenye maji matrilioni ya maji ya dunia.
Hitimisho Ya Hii Nadharia
Kwa siku inayofuata nitaelezea namna ile changamoto ya lugha ndiyo iliyomletea shida bwana Russel.
Nadharia Ya Mithili Ya Mfuniko Wa Maji Unaoizunguka Dunia ‘’Canopy Theory’’
Tabaka la maji linaizunguka dunia, hilo ndilo linaitwa ‘’canopy’’.
Hii nadharia ilichochewa sana na mwalimu mmoja, na mwanasayansi za kufikirika ‘’Pseudoscientist’’. Ambaye anaaminiwa pia kuchukua hii nadharia toka kwa Imani za kipagani za awali kabisa. ambazo tayari zilikuwa na hii nadharia ‘’canopy model’’. alichofanya huyu bwana ni kuiingiza katika sayansi ya uumbaji akiamini itakidhi vigezo vya sayansi ya uumbaji. Nadharia hii ilipokewa kwa wingi sana na watu kutokana na urahisi wake wa kimantiki. na taasisi kadhaa ziliipokea vizuri na kuifundisha, na hata binafsi kwa mara ya kwanza ilinistaajabisha! lakini kadri nadharia hii ilipofanyiwa utafiti, ikagundulika kuwa na changamoto kubwa kiasi kuwa haitumiki tena, lakini hebu tuitazame.
Canopy theory inaelezea kuwa, Mungu alipotenganisha maji ya chini na juu ya Firmament au Anga au Raqia au Expanse. Basi yale maji yalikuwa ndiyo maji yaliyokuwa yakiizunguka Dunia. Na hii inasema kuwa, kulikuwa na Tabaka la maji lililokuwa juu angani likiizunguka dunia. Tabaka hili lilisaidia sana katika kuiepusha dunia dhidi ya Mionzi toka kwenye Jua, na Space, au Cosmos kwa ujumla. Tabaka hili la maji pia linaaminiwa kusaidia katika kufanya hali Joto ya Dunia kuwa nzuri au Rafiki. Na Pia inaaminiwa kuwa tabaka hili la maji ndilo ambalo lilipelekea mvua ya kwanza katika kipindi cha gharika ya Nuhu, kwa siku arobaini za kwanza.
Changamoto za Kufeli kwa Nadharia ya Canopy model.
1. Tatizo la Joto ‘’Heat Problem’’.
Kiwango cha Joto kitakachokuwa kinaingia Duniani, hakitatoka kirahisi na kupelekea uwepo wa joto sana katika ulimwengu hata kutosapoti Maisha. vuta picha tu ya joto kabla ya mvua kutokana na mawingu ya maji kidogo vile.
2. Tatizo la Kukaa kwa Maji Angani ‘’Support Problem’’,
Maji yasingeweza kukaa angani. lazima yangebadilika kuwa mvuke, kwa maana maji yatawezaje kukaa angani. na hata kama ingelikuwa ni barafu, bado isingekubaliana na mtazamo wa nadharia hii na ingeleta changamoto nyingine.
3. Tatizo la Mwanga ‘’Light Problem’’
Kwa kawaida Mwanga ambao ungepita kwenye hili tabaka la maji yaliyo angani ungebadilishwa baadhi ya tabia zake, kwa kupitia kuakisiwa, kupindishwa, kugongana mionzi n.k ‘’reflections, refractions, interference’’ hii yote ingepelekea mwanga unaofika duniani usiwe wa ubora wake wa awali. na mtu aliye duniani asingeweza ona vizuri taarifa za vitu vilivyo juu angani.
4. Tatizo la Mgandamizo wa Presha ‘’Pressure Problem’’
Kama kiwango cha maji yaliyopaswa kuwepo yangelikuwa katika anga. Basi yangesababisha mgandamizo mkubwa sana wa hali ya hewa duniani ukilinganisha na huu uliopo leo. hii ingepelekea viumbe kushindwa kuhema vizuri, na hata kufa kwa ‘’Suffocation’’.
5. Kukosa Ushahidi kwa Sayari zingine, hata sayari zingine kama Venus. ambazo zina anga ‘’Atmosphere’’. hazina Ushahidi wa uwepo wa kitu mfanano wa ‘’Canopy’’.
Hitimisho
Nadharia hii ambayo nayo ilitumia neno ‘’Raqia’’ kumaanisha Anga, ilifeli kwa kukosa Ushahidi wa kisayansi. Hii inatoa namna ya ajabu, namna kosa dogo tu la hata kutoelewa ukweli katika taarifa Fulani. huaribu mantiki nzima na elimu yoyote ile. Ukweli huwa na nguvu, na umejifungamanisha katika kila Nyanja. wapo wanasayansi walioipigania kwa kujaribu hata kutumia nadharia ya kuwa, maji yalikuwa ni mithili ‘’Metallic Hydrogen’’ kutokana na mgandamizo mkubwa, na kuwa sifa hiyo ingeongezea ubora wa utendaji wake, lakini bado haina nguvu.
********************--------------*****************
Ukweli Ni Upi?
Biblia iko wazi ‘’Firmament ni kitu kigumu -Ardhi ya Dunia -Earth’s Crust’’. Mungu akatenganisha maji yaliyo Juu- hayo ndiyo mbeleni yataenda kutengeneza Bahari. Na pia maji Yaliyo Chini, ambayo hayo ndiyo maji yaliyokuja baadae kuleta gharika ya nuhu, baada ya milango ya chemchemi za Vilindi vikuu kupasuka ‘’Fountains of Great Deep’’.
Na Haimaanishi! Mungu akatenganisha Maji yaliyo chini ya anga la hewa, na Maji yaliyo juu ya hewa.
Ushahidi Mkubwa Zaidi
2Petro3:5 ‘’Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa, zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu’’. hii ni kama kukumbushia uumbaji wa Firmament ambao unaumbwa tokea kwenye maji na ukawa ndani ya maji hata alipotenganisha.
8. Mungu Akaliita Lile Anga Mbingu. Ikawa Jioni Ikawa Asubuhi, Siku Ya Pili.
Mwanzo 1:8
Mungu akaiita ‘’Firmament’’ Mbingu ‘’heaven’’. Hapa inajirudia ile ile changamoto ya awali, ya wale wale ambao wamezoea kutumia neno ‘’Raqia’’ kumaanisha ‘’Raqia of the heavens’’. Kiufupi hapa ‘’sehemu inayoitwa Mbingu au Heaven’’ ni sehemu ambayo sisi Binadamu tunaishi, ambayo ndiyo Firmament au ‘’Ardhi ya Dunia’’.
Linatumika neno Heaven kwa kuwa, ndiyo sehemu ambayo Mungu anakutana na Watoto wake. Wengi hawatambui ya kuwa hii dunia Mungu aliiumba awali awe akiwa na wana na binti zake, na ndiyo maana Adamu na Eva walikuwa wakionana na Mungu kila siku. hata walipopoteza utukufu kwa dhambi.
Kukimbilia kutafsiri ‘’Raqia’’ kama anga la hewa, baadhi wakihisi hii ‘’Space’’ itakimbia maswali. wakajikuta wakikutana na maswali mengi Zaidi. Mtu mmoja alikuwa akimuuliza Prof.Russsel Humphreys kwenye presentation yake kuwa, Je space inatanuka au vitu vinatanuka ndani ya space? Ni ajabu sana, na inaleta mantiki nyepesi sana kutambua, Mbingu katika siku hii ya pili, ilikuwa ni Dunia. Ambayo ndiyo Biblia imeiita Firmament au ‘’kitu kigumu’’. ukisema ni sehemu kati ya maji, aidha kwa nadharia ya Canopy iliyofeli, haitaleta mantiki. au ya Russel Humphreys, pia haina mantiki.
Mbingu Iliumbwa Siku Ya Kwanza Au Ya Pili? Rejea Mwanzo 1:1. ‘’Aliumba Mbingu Na Nchi’’
Hii haina changamoto kwa niliyeanza naye katika mwanzo 1:1, maana hapa tuliona mwanzo wa muda, mbingu, na nchi. kama ‘’time, space and matter’’. kwa maana haya yote yanayofanyika, yanahitaji hizo fremu kuu tatu, na ndiyo maana Biblia imeandika, neno Nchi au Earth katika siku ya kwanza, lakini inakuja kuonyesha Mungu akiita Nchi au Earth kwa mara ya kwanza katika siku ya Tatu. kwa hiyo pale neno Earth au Nchi lilitumika kutoa msingi au utangulizi na maana ya matter kwa ujumla, kabla haijakamilika kuunda kitakachotokea. Kiufupi mstari wa kwanza unaweza utumia kumaanisha ufupisho ‘’summary’’ ya mwisho wote wa uumbaji, au mwanzo wote wa uumbaji, maana kote ni matokeo ya hizo fremu kuu tatu, ‘’matter, space, and time’’.
To be continued....
Mwandishi na Mwenyekiti
Mtaalamu wa sayansi ya wanyama, mwanabiofizikia, na mwandishi wa vitabu vya kisayansi. Mwanzilishi wa Injili ya Sayansi — taasisi inayounganisha maarifa ya kisayansi na imani.
Shiriki makala hii
29 min
82 min
6 min