Inapakia...
Inapakia...
Dr Brighton Shoo
Mwandishi na Mwenyekiti
“Kwanini Parachich lina Mbegu moja, na huku Limao lina mamia ya mbegu? Tunda lolote linapokuwa na mbegu moja humaanisha kuwa linawekeza zaidi kwa mtoto huyo mmoja. Hii ni kama ambavyo tembo huzaa mtoto…”
Kwanini Parachich lina Mbegu moja, na huku Limao lina mamia ya mbegu?
Tunda lolote linapokuwa na mbegu moja humaanisha kuwa linawekeza zaidi kwa mtoto huyo mmoja. Hii ni kama ambavyo tembo huzaa mtoto mmoja tu, huku panya akizaa Watoto kuanzia 10 mpaka 18 kwa mzao mmoja tu. Mimea ambayo huzaa mbegu moja tu huwekeza virutubisho vingi sana kwa mbegu zake, mimea ambayo huwa na mbegu nyingi huwekeza kidogo sana kwa mbegu zake, na hili lina siri kubwa sana.Kwanini kuna matunda yasiyo na mbegu siku hizi?
Mmea kama viumbe, huwa na nishati ambayo unaweza wekeza aidha katika ukuaji wake, au katika uzazi wake. Mmea unaowahi kuzaa hukua kidogo, na huwahi kufa pia. Kama mmea utawekeza sana katika uzao wake utakufa haraka zaidi. Na hii ndiyo sababu mimea ya matikiti na maboga hufa haraka sana, kwa kuwa Watoto wake huwa wakubwa sana. Mimea kama ya Mapera huchelewa sana kuzaa na huwa na matawi, mizizi, na mashina makubwa na imara sana.
Wana teknolojia wa kilimo hujitahidi kucheza na jenetikia za mimea kwa kutafuta mimea yenye shida za vinasaba vya kuzalisha mbegu, au kubadilisha jenetikia kwa kuathiri vinasaba vinavyohusiana na ukuaji wa tunda baada tu ya mbegu, vinasaba mfano vya ‘’AGL11, INO, SIMBP3, IAA9, ARF7, n.k. teknolojia hizi nimezielezea kwa kina sana katika blog yangu ‘’Dr Brighton shoo’’, hasa teknolojia za CRISPR/cas9, GMO, n.k. Wanabioteknolojia kwa kuzuia ukuaji wa mbegu hufanya matunda kuwa makubwa sana, hii ni kwa kuwa, hufanya nishati yote ya Mmea ya uzazi, kutoelekezwa zaidi katika Mbegu kama ambavyo huwa katika asili, na hivyo nishati hii yote kutumika kutengeneza sukari, au wanga, ambayo ndiyo hulifanya tunda kuwa kubwa.
Je wajua!!
Asilimia 70% ya antioxidants zote zilizopo katika Parachichi huwemo katika Mbegu yake tu. Matumizi ya unga wa mbegu ya Parachichi Kwa kiasi kidogo huwa na faida kubwa sana katika afya.
Mwandishi na Mwenyekiti
Mtaalamu wa sayansi ya wanyama, mwanabiofizikia, na mwandishi wa vitabu vya kisayansi. Mwanzilishi wa Injili ya Sayansi — taasisi inayounganisha maarifa ya kisayansi na imani.
Shiriki makala hii
29 min
1 min
11 min