Inapakia...
Inapakia...

Dr Brighton Shoo
Mwandishi na Mwenyekiti
“KISA KIDOGO CHA KUSHINDA NA MIANGA USIKU NA VITAMBI Sayansi ya mionzi ya vifaa vya umeme, na kuchelewa kuamka Kama hutaki kusoma sana jua hii Mwanga wa taa, tv, simu wakati wa usiku huzuia homoni ya m…”
KISA KIDOGO CHA KUSHINDA NA MIANGA USIKU NA VITAMBI
Sayansi ya mionzi ya vifaa vya umeme, na kuchelewa kuamka
Kama hutaki kusoma sana jua hii
Mwanga wa taa, tv, simu wakati wa usiku huzuia homoni ya melatonin. Homoni hii huchuja sumu za mwili zote, na kusaidia mitochondria ijizalishe, izalishe nishati na kutozalisha sumu ‘’ROS’’. Unapokuwa sana katika mianga hii usiku, sumu hujaa, na mwili huchochea zaidi mafuta ili kujilinda. Kwa hiyo mafuta kwanza kabisa huwa ni namna ya mwili kujilinda. Pili, mitochondria zinapoathirika, sukari nyingi hubadilishwa kuelekea zaidi kuunda mafuta. Ukitaka kujua tatu mpaka kumi, soma chini.
Hii ni miongoni mwa biolojia ambayo watu wachache sana wanaweza kuielewa, natoa shukurani zangu kubwa sana kwa mtaalamu mkongwe wa Ubongo Dr. Jack kruse, kwa ufupi sana, viumbe ni matokeo ya asili yao, viumbe wametoka katika udongo na maji, na wanaishi kwa sababu ya hewa na mwanga. Ni muhimu sana kujali mfumo wako wa asili unaokushikilia. Watu wengi hupuuzia sana biolojia hii, sehemu ya mbele tutaangalia kiundani zaidi sayansi hii.
Kuhusiana na Mafuta ya miili ya viumbe, ni muhimu kutambua kuwa, mafuta ni tabaka pekee la kulinda kila kilicho hai. Unapoelekea katika ubongo, seli za ubongo huitaji kufunikwa na tabaka hili la mafuta, ambayo huitwa ‘’myelin’’, hata kila seli, huwa na ukuta ambao huwa umejaa mafuta. Mwili hutengeneza kiwango cha mafuta kulingana na sumu zinazouzunguka, popote pale panapokuwa na changamoto nyingi zaidi za kuudhuru mwili, mwili huongeza kiwango cha mafuta.
Kutanuka marazote hutokana na kuisha, kila kitu kinapokuwa kikiisha, huwa kinatanuka. Kuanzia katika mifumo ya galaxy, nguo za watu, moyo tuliona unapoisha hutanuka, moyo unapozeeka hutanuka pia, hii ni sheria kubwa sana ya sayansi, inayosema vitu huelekea marazote katika kuchoka, na katika kuchoka, kani zinazoshikilia vitu hivi huishiwa nguvu, na hivyo vitu huanza kutanuka vikijiachia. Kama ukiona maiti ya siku moja tu iliyoachwa huru, utagundua maana ya kauli hii ya kutanuka, kadri vitu vinapokuwa na saizi ya wastani, maana yake huwa vinakuwa na nguvu kubwa zaidi. Kuna sheria nyingi sana fizikia zinazofuata uhusiano huu, ikiwemo kani ya gravitation, kani ya chaji za umeme, kani ya usumaku, kani ya mvuto wa vitu elastic,n.k.
Lengo ni hili, hata seli za mwili nazo hufuata sheria hizi, kadri ambavyo seli huwa zikiisha, huwa zinazalisha mafuta mengi zaidi. Watu wengi wanene huwa na wastani wa matatizo mengi zaidi ya watu wa saizi ya wastani, penginepo hata zaidi ya watu wembamba. Huu unene huanzia katika seli zao, na katika seli zao stori huanzia katika kiwango cha mafuta. Na kiwango cha mafuta huanzia katika kiwango cha sumu. Na katika sehemu nakueleza kuwa, kiwango kikubwa sana cha sumu kinatokana na watu kutozingatia utaratibu wao wa asili yao waliyotokana nayo.
Kiumbe yeyote aliyemzima amelala anapaswa kuamshwa asubuhi na mfumo wake wa homoni na ubongo, na anapoamka anapaswa Kwenda kufanya kazi, na hapa anahitaji kuwa na nishati ya kutosha ya kusukuma misuli yake. Matendo haya huitaji sana mfumo unaoitwa ‘’Hypothalamo-pituitary-adrenal axis’’, ambapo huwa unaenda sambamba na utendaji wa tezi ya pineal ‘’pineal gland’’, hii huusiana na mzunguko wa siku. Kitu pekee ambacho huratibu mzunguko wote huu, ni mipishano ya mianga ya asili, katika namna za frequency, kutoka kubwa sana ya mwanga, mpaka hafifu sana ya giza, na kuendelea huku ikipishana kidogo kidogo kama ambavyo tezi na mifumo hii hufanya kazi.
Kazi kubwa sana za ubongo kipindi kiumbe anapolala huwa ni kuchuja sumu zote, figo pia hukusanya uchafu wote, kila kiungo wakati wa usiku huwa ni wakati wa usafi. Misuli yote huwa ime paralaizi ili kurekebisha vidonda, michubuko, kutoa sumu, na kujenga kinga ya mwili.
Viumbe wanapolala miili yao huwa haina stress hata kidogo, maana mfumo wa stress wa ubongo wa ‘’sympathetic nervous system ‘’ huwa umezima kabisa, na homoni za stress kama adrenaline, na cortisol huwa chini kabisa. Na hapa ndipo hata kumbukumbu huboreshwa kipindi watu wanapokuwa wanalala katika hatua ya usingizi ya ‘’rapid eye movement’’, ambapo mtu huwa akiota. Usiku huambatana na giza kwa kuwa asili imeutengeneza ubongo usipate taarifa wakati wa usiku mfano kwa kuona, ili usizingatie, utulie sasa uweze kurelax, na hata hali ya hewa ya usiku huwa ni ya baridi, kutengeneza mazingira ya ‘’hibernation’’, yaani, mwili uweze kupooza mpaka utendaji wa seli, au metaboliki za mwili.
Wakati wa usiku giza linapoingiza, husisimka mfumo wa protini wa tryptophan ambao huambatana na uzalishwaji wa homoni kama za ‘’melatonin’’, ambayo hii ndiyo kama sabuni kuu ya ubongo ‘’major antioxidants’’, husafisha sana ubongo. pia huzalishwa sana serotonins, ambazo hizi hutuliza mood za akili, watu wengi wakati wa usiku akili zao huwa zimetulia sana, na hata viumbe wengi wakati huu huweza kufanya mapenzi kwa kuwa stress huwa chache sana zinazozuia mfumo wa parasympathetic nervous system, ambao ndio unahusiana na kujaa kwa damu katika via vya uzazi, na mara nyingi nyakati hizi, tryptophans huzalisha pia homoni za endorphins, ambazo hutengeneza hisia za raha, kabla ya kulala. Asili ipo vizuri sana katika kusapoti maisha, sifa hizi zote ziende kwa Mungu muumbaji wa mbingu na nchi.
Chanzo cha Tatizo
Usasa mwingi sana ulioanza karne ya kumi na tisa, ambapo kazi kubwa ya engineer Nicola Tesla ya taa za AC, au umeme wa kisasa ulipofikia jamii za watu, ijapokuwa awali hakukuwa na shida sana kutokana na matumizi ya taa za mwanga hafifu-mwekundu, baadaye matumizi ya taa zenye nguvu za mwanga mkali, wa frequency hizi za kawaida, kama za mchana za -Blue zilishamiri sana.
Mianga unayotumia katika simu yako, katika gari lako, nyumbani mwako, na maeneo kadha wa kadha hata hospitalini, kipindi cha upasuaji, na mashine nyingi za kuonea, ndiyo mwanga ninaouzungumzia kuwa ni hatari sana.
Mwanga huu kwanza kabisa ni tofauti na wengi wanavyouhisia, wengi wanahisi mwanga huu hauwezi kupenya katika vichwa, na pili, wengi wanahisi mwanga huu hauna madhara ya kuendelea zaidi ukiachana na tu na kutua katika jicho. Lakini ajabu ni kuwa, mianga hii kama ambavyo unapokuwa ukiangalia mpira, au filamu wakati wa usiku, au ukisoma kompyuta wakati wa usiku. Mianga hii huingia moja kwa moja mpaka kwenye jicho, mingine hupenya katika Ngozi, na hii mianga husisimua maelfu ya sensa za mwanga mfano zinazoitwa ‘’melanopsin’’, ambazo zimetapakaa kutoka kwenye ubongo, mpaka kwenye utumbo, na huko huuambia mwili kuwa upo katika mazingira sawa kabisa na mazingira ya mchana. Yaani, mazingira ya stress, mazingira ya kuzingatia, mazingira ya kutohitaji biolojia yote ile niliyoielezea ya umuhimu wa usiku. Watumiaji wa taa hizi, Biolojia yao yote hubadilika.
Watu wengi hawaelewi kwanini madaktari wengi hasa wa shift za usiku wanazidi kuwa vibonge, kama ilivyo kwa manesi, kama ilivyo kwa madereva pia. Usipolielewa hili unaweza kuhisi kuwa watu hawa hawazingatii afya, lakini ukweli ni kuwa. Kama ambavyo wakati wa usiku watu wanapolala huwa hawahisi tena hamu ya kula. Hii ni kutokana na kuwa, mfumo wao wa hisia ya kula huwa chini sana. Lakini mianga hii ya blue husisimua mifumo hii, hasa mfumo unaoitwa ‘’leptin melanocortical pathway’’, ambapo mfumo huu huathiri kabisa mfumo wa homoni wa kuridhika, na mwilini kubalansi kiwango cha chakula mwilini. Madhara yake watu huwa walaji sana, lakini pia hata kiwango cha mafuta ambayo huwa yanaundwa huwa ni kikubwa sana, sababu zikiwa zifuatazo.
Mwanga na Mitochondria
Mwanga wa giza ndiyo swichi kuu ya kuwasha mfumo wa ubongo wa kusafisha uchafu na sumu zote, kwa kuchochea uzalishaji wa homoni ya melatonin. Homoni ya melatonin ndiyo huusika moja kwa moja na kurekebisha makosa yote yanayofanyika katika chembechembe za nishati za mwili, yaani Mitochondria. Melatonin unaweza iita kama ‘’major brain anti-oxidant’’. Inapotokea mwili, au ubongo upo katika mwanga wa mchana, hasa kwa matumizi ya balbu za taa za mwanga mkali mpaka usiku, mfano, watu wanapokuwa wanaangalia mpira, au wanapokuwa wakichati kwenye simu zao, au wanapokuwa wanaangalia filamu, au wanapokuwa wakisoma usiku. Frequency za mianga ya blue wanayoitumia, hupelekea ubongo kutozalisha homoni hii ya melatonin.
Na sababu ya kutozalisha ni kuwa, mwanga wa blue, au huu wa kawaida wa hivi vifaa na taa, huwa ukichochea stress wakati wote. Yaani, unachochea uzalishwaji wa homoni ya ‘adrenaline’’, na kwa wakati wa usiku unapowashwa, huchochea uzalishwaji wa homoni ya stress ‘’cortisol’’. Na kumbuka watu hupenda kuutumia sana wakati wa usiku kwa kuwa, huwa unachochea sana uzalishwaji wa homoni za ‘’dopamine’’, ambapo hizi hutengeneza hisia za uzingatiaji na motisha. Na sasa basi, homoni zote zinazochochea stress huathiri utendaji wa mfumo wa protini wa tryptophan, ambayo ndiyo huusika pia na uzalishwaji wa homoni ya melatonin zaidi kwa usiku, na serotonin kwa mchana (serotonin ndiyo hubadilishwa kuunda melatonin), homoni ya melatonin moja ya kazi yake kubwa kabisa huwa ni kusafisha sumu za ubongo, na kurekebisha makosa ya Mitochondria, ambayo ndiyo kiungo kinachozalisha kemikali sumu nyingi sana, ‘’producer of free radicalss’’.
Mitochondria huzalisha sumu nyingi za free radicals kwa kuwa yenyewe ndiyo huusiana na uzalishaji wa chembechembe za elekroni, na sasa inapopata changamoto, hupelekea hizi elektroni kuzalisha kemikali sumu nyingi sana. Ni jukumu kubwa la melatonin kuhakikisha inarekebisha makosa ya mitochondria yenyewe, na pili inafuta uchafu wote uliotokana na kemikali hizi sumu. Melatonin pia huchochea kuzalisha kemikali zingine kama (superoxide dismutase, glutathione peroxidase, catalase) za kusafisha chembechembe hatari za free radicals kama (hydroxyl radicals, superoxide anions, n.k). mtu anapokuwa macho usiku katika mazingira ya mianga ya kisasa, huchochea stress kama ilivyo kawaida, na stress hizo husisimua chembechembe zinazoitwa IDO ‘’indoleamine 2,3-dioxygenase’’ ambazo hizi huzuia uzalishaji wa melatonin, na kuchochea uzalishaji wa chembechembe nyingine inayoitwa ‘’kynurenine’’. Hii hupelekea kuzalishwa kwa chembechembe za ‘’NAD’’, na chembechembe inayoitwa ‘’Picolinic acid’’. Chembechembe ya NAD inafahamika kutumika katika kuzalisha chembechembe za kubeba nishati, na Picolinic acid inahusiana na matatizo mengi sana ya ubongo. hizi zote ni lugha ya kuwa ubongo upo katika mazingira ya hatari.
Ajabu zaidi ni kuwa, kiwango kikubwa cha chembechembe zilezile za awali za ‘’IL-1, IL-6, na TNF-α”” humchochea sana chembechembe IDO ili kuzuia uzalishwaji wa melatonin, na kuchochea uzalishwaji wa kynurenine. Hii inaweza kukwambia nini? Giza na maji ni vitu vyenye umuhimu sana katika kuondokana na madhara ya uvimbe, na shida za ubongo. unapokosa wakati wa giza wa kutosha, unaongeza kiwango cha stress, unaongeza kiwango cha sumu taka za mwili, na mwili unaanza kusisimka kwa kujihami kwa kulinda kuta zake kwa uvimbe. Na hapo ndipo tunapopata chembechembe hizo za kinga za uvimbe, na mwili kujirekebisha. Ajabu ni kuwa, tryptophan kutokana na stress za kukosa mwanga, hubadilishwa kupitia chaneli hiyo ya kynurenine, na kuzalisha kemikali mbili, picolinic acid, na quinolinic acid. Kemikali ya kwanza huchochea uvimbe, na ni sumu kwa namna husisimua sana mageti ya ubongo yanayoitwa ‘��NMDA’’ yanayohusiana na kumbukumbu, kujifunza, na kukua kwa ubongo kimaarifa. Na huu ndiyo mwanzo wa magonjwa mengi kama ya kupoteza kumbukumbu, kuishiwa uwezo wa kutawala misuli, kukosa balansi ya homoni za kuongoza utendaji wa ubongo, yaani magonjwa kama ‘’Parkison disease, Alzheimer’s disease, Schizophrenia, Huntington’s, na amyotrophic lateral sclerosis, na hata cancer’’. Upande wa picolinic acid, yenyewe huwa na kazi ya kuulinda ubongo usivimbe.
Kama unaweza kuelewa ubongo unachosema pale unapokuwa na mwanga wa kisasa wakati wa usiku kutokana na tryptophan metabolism ni kwamba, ‘’mfumo wa utoaji taka umezuiwa, mfumo wa uzalishaji nishati umezuiwa, na sasa hebu tuongeze vizalisha nishati, tutengeneze mazingira ya kutoshambuliwa na sumu zitakazoanza kujaa, na mwisho tujilinde tusidhulike sana’’. Kutokana na hili tatizo, basi ndipo ubongo husisimka hata kuepelekea matatizo mengine kama ilivyokuwa kwa mifumo mingine.
Mwanga na Kujaa Mafuta
Katika Mitochondria huwa kuna protini zinaitwa ‘’UCP, au Uncoupling Proteins’’. Hizi huwa na kazi moja kubwa sana, zenyewe wakati wa usiku, huwa zinapunguza kiwango cha chembechembe za Proton zinazoingia ndani ya mitochondria, na kwa kufanya hivi huzuia uzalishaji wa chembechembe za nishati za ATP, na madhara yake nishati yote hubadilishwa na kutengeneza Joto. Kiwango hiki cha Joto husaidia sana katika kuvunja vunja mafuta yaliyo katika seli, na hata kuzalisha nishati katika mazingira ya baridi ‘’cold thermiogenesis’’. Miongoni mwa makosa makubwa ya kukaa usiku na mianga ya taa za kisasa ni kuwa, huwa inaathiri protini hawa wa ‘’UCP. Madhara ya kuwaathiri hawa protini huwa ni kupelekea kujaa sana kwa mafuta katika mwili, hii ni kwa kuwa, mfumo wa kuvunja haya mafuta umeshaathiriwa.
Na sababu ya kwanini hizi protini zinaathiriwa huanzia kulekule ya kuwa, mwanga wa blue huathiri utendaji wa homoni ya kuridhika, ya Leptin. Unapokula mafuta siku zote katika chakula, huwa mafuta yakisisimua homoni hii ya leptin na kukufanya usijisikie hamu ya kula zaidi. Mwanga wa blue huathiri kabisa uwezo huu wa leptin wa kutuliza hamu ya kula, na madhara yake mtu hula na hula zaidi, hii ni sababu ambayo hupelekea watu kuwa wanene sana, au kuwa na cholesterols sana. Lakini pia, leptin huchochea mfumo wa ubongo unaoitwa ‘’Leptin melanocortical pathway’’, ambao mfumo huu ndiyo husisimua sasa wale ‘’UCP’’, na kwa mantiki hii, chaneli moja, huchochea chaneli nyingine, lakini zote huishia kujaa kwa mafuta.
UTANGULIZI
Injili ya sayansi Q4 imejikita katika kuzungumzia udanganyifu wa milango, na mifumo ya fahamu. ni kitabu ambacho msomaji anapaswa kuwa makini sana. kwa maana, ni tofauti na vitabu vingine vya afya. Vinavyozungumzia, madhara ya vitu Fulani tu katika mlango Fulani, au mfumo Fulani wa fahamu. Mfano, katika mlango wa fahamu wa ulimi ,vitabu vingi vingezungumzia madhara ya ulaji wa vyakula Fulani, au vingezungumzia ushauri wa ulaji wa vyakula Fulani kisayansi. lakini kitabu hiki, kimejikita katika kuvumbua namna ambavyo, mifumo ya fahamu huwa ikidanganywa. na lengo au madhara makuu, ya kudanganywa kwake. Pia, kitabu kimejikita kutoa siri za kisayansi, za uwezo wa kudanganya milango ya fahamu. Msomaji atanufaika kujua udhaifu wa tabia za milango ya fahamu. na pia, atagundua nini hasa ni sababu zilizo nyuma ya tabia hizi za uharibifu. kitabu kinatoa mwangaza Kwa milango yote ya fahamu. yaani macho,masikio,Ngozi,pua na ulimi. na mifumo ya jenetikia. tutaangalia sayansi kadhaa. za misingi ya ufanyaji kazi wa milango hii ya fahamu. na kisha, tutaangalia nini hufanywa, ili kuiteka milango hii ya fahamu. na fahamu kwa ujumla.
Sababu za kuandika kitabu hiki, zimeanza baada ya kugundua ongezeko la ushindani wa kiviwanda, na nia za kukuza nguvu za kiutawala, zimepelekea kupungua kwa upendo kwa wengine. na kuongeza uhitaji wa wengine. na hii imechochewa na dhiki za kiuchumi, mpaka kuanza hata kutumia sayansi, ili kufikia malengo hayo makuu. Sio kwamba utafiti wangu ni mkubwa sana kuweza kugundua haya! La hasha, ila ni Upendo wa Mungu ulioniongozea Maarifa ya kuona, namna Uongo ulivyotapakaa mpaka kuifikia milango na mifumo ya fahamu .
USHAURI KWA MSOMAJI
Msomaji anapaswa kuwa makini, kutokuza au dogosha matokeo ya tafiti, na taarifa kadhaa, hasa, kuhusu taarifa za vitu ambavyo amekuwa akivizoelea. Pili, msomaji anapaswa kuwa mdadisi zaidi, juu ya taarifa za nukuu kadhaa. Ambazo, atakuwa na mashaka nazo. na kitabu hiki kinaweza toa mwangaza mzuri kwa tafiti nyingi zaidi binafsi. Hasa, katika kizazi hiki chenye uwingi wa taarifa. Tatu, msomaji anapaswa kutambua kitabu hiki chenye nukuu ‘’references’’ nyingi za taarifa zilizokwisha fanyika, pia kinahusisha mitazamo mizuri ya kisayansi ‘’scientific guesses’’ za mwandishi. Hasa, katika maeneo yenye taarifa zenye mashaka au pungufu. Na pia katika kugundua siri. Mwisho, kitabu hiki kinatoa elimu za Fiziolojia na jenetikia ya utendaji kazi wa milango ya fahamu. kwa kiwango kadhaa cha kumnufaisha msomaji.
MATUMIZI YA LUGHA KATIKA KITABU HIKI
Lengo la kitabu hiki ilikuwa ni kutumia lugha ya Kiswahili, tokea mwanzo hata mwisho. Lakini, kutokana na changamoto ya misamiati kadhaa. kumekuwa na uchanganyaji wa lugha ya kiingereza na Kiswahili, katika maeneo mengi sana. Hasa, yanayohusu uorodheshaji wa majina ya kisayansi. Natamani msomaji atambue changamoto ya uandishi, kipindi anajifunza, lakini ajikite katika lengo husika. Kitabu hiki kimeandikwa kwa namna ya kitaalamu sana, na hivyo msomaji awe makini sana.
SHUKURANI
Namshukuru sana Mungu kwa kunipatia roho ya udadisi. Hasa, wa kuwa na mashaka ya udanganywaji wa milango ya fahamu, tangia nikiwa mdogo. Lakini pia, ni Mungu ndiye aliyenipitisha katika njia ambayo, nimeweza kuona nilichokuwa nikikihisi.Nashukuru sana familia yangu, Baba yangu Godwin E. Shoo, Mama yangu Dementina F. Mkote, ndugu zangu Neema, Catherine, Grayson, Eunice, Victor, Alen, Hellen na Abigaili. Shangazi yangu Lilian E.Shoo na Mjomba wangu Ignas Mkote. na ndugu zangu wengine wengi kuweza kuwaorodhesha, wote nawashukuru kwa maombi yao. Nawashukuru sana Rafiki zangu Dr.Magesa Matiku,Dr. Issa Mpogo ,Dr.Fidel anatory ,Dr.Hamis ,Dr.Mwaipape Luckydube, Dr.Aweza James, Mr.Fred Mushi,Mr.Zebedayo Dr.John Fikiri. Mwinj.Samweli Musa ,Rafiki yangu Bright Nyongole, Ernest B.Jonass, Kanolo na Dr.Aidan Angelo.Nashukuru pia kwa ushirikiano mkubwa wa kirafiki, na kiufundi kwa rafiki yangu Miss.Evaline Josephat kwa uchapishaji, phD Katemi kwa sapoti ya taarifa, na utaalamu wa kiuandishi. Prof.Walter Veith, shirika la tafiti la NCBI, Research gate na mengineyo. Ambayo, nimeyanukuu kwa taarifa nyingi sana kitafiti, na shukurani nyingi zaidi kwa wanasayanansi wengi, niliyopitia kazi zao. Na nukuu zao, nimezigawanya katika namna ya kutambua michango yao, kwa references, kwa hoja.
KWA MSOMAJI ASIYE NA MSINGI MKUBWA WA SAYANSI
Anaweza kuachana na sura zinazozungumzia Fiziolojia moja kwa moja. Fiziolojia ya kuona, fiziolojia ya kunusa na Ladha, Fiziolojia ya Kusikia, Misingi ya sayansi za Jenetikia na Undani wa sayansi za madhara kwa tafiti kadhaa. Pia anaweza kuachana na sehemu zinazozungumzia sayansi kwa undani. Hapaswi kuacha sehemu zingine zote. Kitabu hiki kina mada ambazo, ni muhimu sana kwa watu wote kuzisoma, iwe kwa urahisi au kwa ugumu.
MAONI JUU YA CHANGAMOTO ZA KITAALUMA
Msomaji anaweza kutoa ushauri, maboresho, pongezi na hata malalamiko moja kwa moja kwa kuwasiliana kupitia blogspot ya Injili ya sayansi, au kupitia njia za mawasiliano zilizowekwa. Tunathamini hatua zote katika kujifunza.
YALIYOMO
KISA KIDOGO CHA KUSHINDA NA MIANGA USIKU NA VITAMBI 2
UTANGULIZI 11
SURA YA 1 27
SAYANSI NA SANAA YA KUTRIKI MACHO KUDANGANYA MFUMO WA FAHAMU 27
UTANGULIZI 27
KWANINI MACHO YANAJENGA IMANI? 28
MAISHA YAMEJAA FAHARI ZA MACHO!! 30
MACHO NDIYO DIRISHA LA WEWE USIYEONEKANA ‘’CONSCIOUSNESS’’!! 31
SAYANSI YA HISIA ZA KUONA KWA VIPOFU WA MACHO!! 32
SAYANSI NA SANAA YA KUTRIKI UFAHAMU KWA KUPITIA MACHO!! 33
MBINU YA KWANZA YA UHARIBIFU 34
Kubadilisha uelekeo wa umakini ‘’attention’’ kwa kutumia tabia ya ubongo na macho katika mifumo ya utambuzi. 34
taarifa zenye mhemko wa kuhamasisha hatari au uhitaji mkubwa. 36
KWANINI UBONGO HUTEKWA KIRAHISI KWA TAARIFA ZA MIHEMKO? 37
SAIKOLOJIA MBAYA YA WANA HABARI KUTUMIA HUU MTINDO KUHATARISHA!! 38
taarifa zilizobeba msisimko mkubwa wa kihisia. 39
KWANINI UBONGO HUTEKWA KIRAHISI KWA TAARIFA ZA HISIA!! 39
SAYANSI YA NDANI ZAIDI YA KUTEKA UMAKINI KWA PICHA ZA NUSU UCHI 45
MADHARA YA KUSISIMUA SISIMUA MFUMO WA UMAKINI!! 47
MBINU YA PILI 52
Kubadilisha wastani au ‘’standard’’ ya viwango vya mifumo ya kifiziolojia, kwa kutumia ukawaida wa uonaji wa taswira. 52
BADILIKO LA FIZIOLOJIA 54
Namna Za Kubadilisha Fiziolojia Za Watu Kwa Kupitia Taswira Kupitia Macho 56
KUTUMIA TASWIRA KUDANGANYA MIFUMO YA FAHAMU 56
SELI ZA UBONGO ZA KUIGA ‘’mirror neurons’’ 56
NAWEZAJE KUBADILI FIZIOLOJIA? 58
Kupitia Kutengeneza Mazoea Ya Hali Za Tabia Zisizo Za Kawaida ‘’Za Kutisha’’ 58
madhara ya filamu za kutisha kwa Watoto na watu wazima. 60
Ubongo Unavyo Chochewa Kipindi Cha Kuangalia Picha Za Hatari!!! 63
Kuchosha Akili Za Watu Na Fiziolojia Zao Bila Wao Kujua. 63
Kusababisha Uraibu ‘’Addiction’’ 64
TAFITI JUU YA URAIBU WA FILAMU au ‘’MOVIES’’ 65
TATIZO FEKI: MOVIE NI HATARI NA HUPASWI KUANGALIA +mitandao ya kijamii 68
TATIZO HALISI: MOVIE NI HATARI TUNAPASWA KUWA MAKINI + mitandao ya kijamii. 68
MBINU YA TATU 69
Kuharibu uwezo wa upokeaji wa taarifa halisi. kwa kutumia usisimuaji wa taswira fikirishi, zenye matokeo katika mfumo wa fiziolojia. 69
Utangulizi 69
SAIKOLOJIA YA WANYAMA MBUGANI 70
SAYANSI NA SANAA YA KUHARIBU UWEZO WA KUPOKEA TAARIFA HALISI 71
TEKNOLOJIA KATIKA UTENGENEZAJI WA FILAMU, NA MBINU ZAKE KATIKA KUUTRIKI UBONGO 72
DIGITAL CINEMATOGRAPHY 72
‘’camera za kisasa zaidi za kidijitali kama Arri Alexa, RED cameras n.k” + Sound Recording + Lighting’’ 72
GREEN SCREEN ( CHROMA KEYING) TECHNOLOGY 74
SPECIAL EFFECTS (PRACTICAL) TECHNOLOGY 75
VISUAL EFFECTS (VFX) TECHNOLOGY 76
EDITING TECHNOLOGIES 77
MOTION CAPTURES TECHNOLOGY 77
3D AND STEREOSCOPING FILMING TECHNOLOGY 78
ANIMATION TECHNOLOGY 79
VIRTUAL REALITY (VR) AND AUGMENTED REALITY (AR) TECHNOLOGY 80
TEKNOLOJIA NYINGINE NYINGI 81
NAMNA TEKNOLOJIA ZINAVYO DANGANYA MIFUMO YA FAHAMU!!! 82
KUTUMIA MIANGA ‘’CONTRAST NA BRIGHTNESS’’ 82
KUTUMIA RANGI ‘’COLOR THEORY’’ 83
MIONDOKO ILIYONYOOSHWA ‘’SMOOTH MOTIONS’’ 83
TABIA YA KULIANDAA TUKIO KABLA YA KULITENDA 84
GREEN SCREEN 84
VISUAL EFFECTS 84
MBINU ZA TEKNOLOJIA ZA MITANDAO YA KIJAMII NA PICHA ZA KU EDIT !!! 86
Kutumia Mbinu Za Mwanga ‘’Contrast Na Brightness’’ 86
Color Correction Na Filters 86
Viongeza Urembo Wa Sura ‘’Face Recognition Na Enhancement’’ 87
SIFA ZA SURA NZURI 87
Je Wajua Kwanini Watoto Wote Huvutia? Hata Wa Simba! 88
VIONGEZA UREMBO KATIKA EDITORS ZA MITANDAO YA KIJAMII 88
Face Detection Na Modification 88
Augmented Reality Filters 89
Cropping, Framming, Symmetry Na Alignment 90
Mng���ao ‘’Sharpness Na Clarity’’ 90
MWONEKANO WA KINA NA UMBALI WA MAZINGIRA ZUNGUKWA 91
MADHARA KATIKA UBONGO!!! 92
MADHARA YA KISAIKOLOJIA!! 93
KUNA UHUSIANO GANI KATI YA SAIKOLOJIA NA FIZIOLOJIA? 94
MADHARA MAKUBWA KWA VIJANA NA WATOTO WANAOTAZAMA PICHA FEKI 99
Je Waujua Vizuri Uzuri Wa Mtu 100
Hakuna Mtu Asiye Mzuri 101
SAYANSI YA KUMALIZA NGUVU ZA KIUME NA SIFA ZA KIUME KWA KUTUMIA TASWIRA FEKI!! 103
Utangulizi 103
TABIA AU SIFA ZA KIUME!! 103
NGUVU ZA KIUME!! 107
SAYANSI YA KUMALIZA NGUVU ZA KIUME 108
Kutibua Mfumo Wa Homoni 109
Ubongo Hutatua Tatizo Kwa Kupunguza Msisimko Wa Taswira Za Macho 111
Kutibua Saikolojia Ya Nguvu Za Kiume 113
Madhara Katika Tabia Za Kujiridhisha!! 114
Utangulizi 114
Sayansi Ya Uharibifu 115
Madhara Katika Ubongo Yanayoshusha Nguvu Za Kiume!! 116
Sio Tu Nguvu Za Kiume Hata Uwezo Wa Kufikiri 119
Kila unaposisimuliwa mfumo wa hisia, huusiana na kushuka kwa kazi za kufikiria katika sehemu ya ubongo ya mbele. 120
Kupungua kwa Ubongo ‘’Grey Matter’’ kwa kuangalia picha za mihemko 120
Madhara Zaidi Katika Ubongo Yanayoathiri Nguvu Za Kiume 122
MAUAJI MAKUBWA YA UBONGO WA WATOTO 125
Utangulizi 125
UGUNDUZI WA ULIOCHOCHEA MAPINDUZI ZAIDI 127
TELEVISHENI 127
RADIO 128
SIMU 129
TEKNOLOJIA ZA MAWASILIANO KWA MAWIMBI 129
MITANDAO YA KIJAMII 130
HUDUMA ZA MITANDAO NA HUDUMA ZA KIDIJITALI 131
KARNE YETU (1914-2024)NGUMU KULIKO ZOTE, YENYE VIFO VINGI NA AINA NYINGI ZAIDI 131
MAJANGA YA ASILI 132
VITA NA MAUAJI YA MASHAMBULIZI 132
MAGONJWA NA MILIPUKO 132
MAPINDUZI YA VIWANDA NA MAJANGA YA TEKNOLOJIA 133
MAJANGA YA KIMAZINGIRA 133
SAYANSI YA UUAJI WA UBONGO WA WATOTO 135
Uangaliaji Sana Wa Televisheni, Simu + Kwa Watoto 135
Gunduzi Za Tafiti Mbalimbali Juu Ya Madhara Katika Ubongo 135
Sababu Za Kisayansi Za Kupungua Kwa Ubongo Kwa Kuangalia Televisheni 137
UBONGO WA MTOTO!!!! 138
Watu wengi hawajui kwanini Watoto huwa hawatulii 138
MADHARA MAKUBWA YA KUPUNGUKIWA MUDA WA KULALA KWA KUANGALIA TV NA SIMU USIKU 139
Madhara Ya Ubongo Kusisimka Kipindi Mtu Amelala Kutokana Na Homoni Cortisol!! 140
KOSA KUBWA LA KUSHINDWA KUELEWA MUDA WA UKUAJI 142
KUATHIRI MAENDELEO YA UBONGO NA UWEZO WA AKILI 145
MADHARA MAKUBWA YA KUWAONESHA WATOTO TASWIRA ZENYE MISISIMKO YA KIHISIA 147
Kuanza Kuonesha Dalili Ya Kupevuka Kabla Ya Wakati Kwa Vijana Wadogo 148
Kupunguza Hisia Juu Ya Mapenzi ‘’Desensitization’’ 150
Kuua Uwezo Wa Kufikiri Kwa Kuchochea Fikra Za Mapenzi 150
MADHARA YA KITABIA 151
Jibu La Kifalsafa La Kwanini Sio Vizuri Kuangalia Uchi 152
SURA YA 2 156
SAYANSI YA UDANGANYIFU WA MASIKIO NA UBONGO 156
Utangulizi. 156
SIFA KUU YA MFUMO WA KUSIKIA 157
KWANINI KUNA UHUSIANO WA KUSIKIA NA KUFIKIRIA 158
JE WAJUA SIFA ZA UVIVU WA KUSIKILIZA 160
UBONGO KIPINDI CHA KUFIKIRIA NA KUVUTA TASWIRA. 161
TRIKI NA MADHARA YA KUSIKILIZA MIZIKI YA MIDUNDO HASA YA MISISIMKO 164
SAUTI INAVYOATHIRI MAUMBO YA MAJI 164
MSINGI WA KWANZA WA UHARIBIFU KATIKA MIZIKI YA MIDUNDO!! 167
UTAFITI WA MADHARA YA SAUTI KUBWA KATIKA AFYA 169
Sauti na Ukuaji kwa viumbe. 170
Sauti na madhara ya DNA 170
Uwepo wa genes mbili za mekaniki. Mfano, ya (sauti) tu 171
Sauti na mabadiliko ya maumbo ya protini 171
Sauti na neva za fahamu 172
Muziki Na Kula Sana Na Ongezeko La Uzito 172
Muziki Wa Pole Hushusha Presha Kwa Wenye Presha 173
Mabadiliko Ya Muziki Toka 440-432hz Hupelekea Kushuka Kwa Presha Na Hali Ya Kutulia Ya Mwili 173
Muziki Wa 440hz Na Hisia Mbaya Kama Hasira 174
Mabadiliko Ya Mawimbi Ya Muziki Na Madhara Katika Dna 174
Bado Sehemu Kubwa Haifahamiki Kuhusu Utendaji Wa Muziki 175
MADHARA YA MUZIKI KATIKA SAIKOLOJIA YA WASIKILIZAJI 176
Utangulizi 176
MISINGI YA UHARIBIFU WA SAIKOLOJIA ZA WATU KUPITIA MUZIKI 180
Kutumia Mabiti Ya Nyimbo Zenye Midundo Kuondoa Uwezo Wa Kutafakari 180
Kwanini Watu Wanacheza 181
Sayansi Ya Muziki Iliyofichika Ya Utofauti Wa Nyimbo Za Midundo Ya Kucheza Na Nyimbo Za Utulivu. 183
Siri Ya Ubongo Wasiyoijua Wasanii Na Wapenzi Wa Nyimbo Za Kizazi Kipya 185
JE KUCHEZA NI VIBAYA? 187
Kucheza Sio Kushangiilia 188
Sio Nyimbo Zote Zisizo Za Dini Zina Madhara Na Sio Kila Nyimbo Ya Dini Haina Madhara. 189
Je Wajua Kuna Nyimbo Za Dini Zilizojaa Rhythms 190
Je Wajua: Msifu Mungu Kwa Kucheza!!! Neno Kucheza Sio ‘’Dance’’ Ni Kifaa 191
Uraibu Wa Midundo Sehemu Ya Kwanza 192
Sifa Ya Nyimbo Zenye Melody Nyingi Zaidi Ya Rhythms 193
Je Wajua Mabiti Yote Ya Kucheza Hufanana 194
Ushahidi Wa Nje Wa Watu Kukosa Uwezo Wa Kutafakari Kupitia Mapigo Ya Mabiti 194
Kutumia Kuchanganyikiwa Kwa Watu Kuingiza Tabia Mbaya Hasa Za Uhuru Wa Tabia Za Kichafu 197
Falsafa Tatu Katika Zama Za Muziki Na Sayansi Katika Zama Za Usasa 198
PRE-MODERN ERA ( tokea zamani za kale mpaka 1789) 198
MODERN ERA (tokea zama za 1789 mpaka 1970) 200
MWANAMAPINDUZI HASI ASIYESEMWA 203
Sababu Za Kutumia Taarifa Za Mihemko Ya Uchafu 207
POST-MODERN ERA (kuanzia 1970 mpaka leo) 209
Kilichofelisha Zama Za Modern Era 210
Kuzaliwa Kwa Zama Za Post-Modern Era 210
Siri Nyuma Ya Msukumo Wa Vipaumbele Vya Elimu 211
Sifa Za Zama Za Post-Modern Era 212
Kazi Ya Muziki Kama Msingi Katika Zama Mpya 213
Kufanya Vitu Kitofauti."kisanii" 214
Kutegwa kutamani umaarufu Kama mafanikio toka kwa mashabiki 216
Hali Za Wasanii Maarufu Zisizosemwa! 217
Kuaminishwa kuwa Mapenzi Ni mazuri Kuliko ndoa. 217
Namna Jamii Inavyoharibiwa Saikolojia Kwa Kusikiliza Nyimbo Hizi 218
Taaluma Ya Kuingiza Mitazamo Katika Ubongo Wa Msikilizaji Bila Msikilizaji Kujitambua 219
Kutumia Mabiti Ya Mawimbi Ya Mihemko Ya Kingono Na Sauti Za Mivuto Ya Hisia 220
Video Za Miziki Ya Midundo, Taa Za Mianga Hafifu Na Maonesho Ya Taswira Za Kimivuto Ya Mapenzi 221
SURA YA 3 223
MBINU ZA KUTRIKI UBONGO KISAIKOLOJIA. 223
Sayansi Ya Kutriki Ubongo Kupitia Magemu Na Michezo 223
MAGEMU 226
MICHEZO (URAIBU WA UTAZAMAJI) 230
JE WAJUA TOFAUTI ZA MASHABIKI NA WACHEZAJI 232
SAYANSI YA KUTRIKI UBONGO KUPITIA PESA 233
Triki za Ubongo kwa njia yapesa’ 234
HISABATI YA KAMALI 235
SURA YA 4 242
FIZIOLOJIA YA MSINGI KATIKA KUONA 242
MWANGA 242
JE WAMJUA MDUDU ANAYEONA ZAIDI!! 243
JE WAJUA VIPOFU WANAVYOONA!! 244
JICHO LINAVYOCHAKATA MWANGA 244
SEHEMU ZA MSINGI ZA JICHO 245
SENSA ZA KUHISI MWANGA ‘’PHOTORECEPTORS’’ 252
SELI ZA KUONA KWENYE MWANGA 253
MATOKEO YA BADILIKO LA cGMP 256
NAMNA TAARIFA MBALIMBALI YA TASWIRA ZINAVYOCHAKATWA 257
GANGLION CELLS 257
MAKUNDI YA GANGLION CELLS 259
UCHAKATWAJI WA RANGI ‘’COLORS’’ 259
SAFARI YA TAARIFA KUTOKA JICHONI KWENDA KWENYE UBONGO 261
CHANNEL TATU KUU ZA TAARIFA YA NEVA KUTOKA MACHONI KUELEKEA KWENYE UBONGO 263
UCHAKATAJI WA TAARIFA YA NEVA YA KUONA KATIKA UBONGO WA KUONA. 267
UHUSIANO MKUBWA WA UBONGO WA KUONA NA KUMBUKUMBU NA UTAMBUZI. 269
SURA YA 5 271
FIZIOLOJIA YA UTENDAJI WA MASIKIO NA KUSIKIA 271
MASIKIO 271
SEHEMU ZA SIKIO "EAR BRIEF ANATOMY AND PHYSIOLOGY" 273
SAFARI YA SIGNALS ZA NEVA YA SAUTI KATIKA SIKIO LA NDANI KUELEKEA KATIKA UBONGO 285
Kutoka Masikioni Mpaka Ubongo Wa Nyuma (Medulla & Pons) 286
Kuelekea Kwenye Ubongo Wa Kati ‘’Midbrain’’ 289
Kutoka Kwenye Ubongo Wa Kati ‘’Midbrain’’ 291
SIFA ZA UBONGO WA KUSIKIA AU ‘’AUDITORY CORTEX’’ 292
Tatizo Linalosababishwa Na Brain Plasticity!!! 293
Kutoka kwenye Ubongo ‘’cerebral cortex’’ 293
Namna Ubongo unavyojikinga na Sauti kali Endelevu 294
Sehemu ya Muziki katika Ubongo. 295
ENEO LA KUCHAMBUA LUGHA, NA KUZALISHA SAUTI, YOTE YANACHANGAMANA NA UBONGO WA SAUTI 296
SURA YA 6 298
SAYANSI YA UBONGO YA MUZIKI ‘’NEUROSCIENCE OF MUSIC’’ 298
Utangulizi 298
PREDICTIVE CODING MODEL 298
SYNCOPATION 302
MELODY 303
HARMONY 303
RHYTHM 304
MATOKEO YA SYNCOPATION 305
RHYTHM NA METER 307
LADHA YA MUZIKI ‘’GROOVE’’ 307
POLYRHYTHMS 308
Triple meter 309
Duple meter. 309
MUZIKI NA HISIA ZA KUSOGEA, TEMBEA AU CHEZA ‘’URGE TO MOVE’’ 310
MIMESIS 311
KUCHEZA ILI KUONGEZA ATTENTION 311
ENTRAINMENT NA EMBODIEMENT 312
JE WAJUA SABABU YA KUKINAI MUZIKI 313
DYNAMIC ATTENDING THEORY ‘’DAT’’ 313
Mwandishi na Mwenyekiti
Mtaalamu wa sayansi ya wanyama, mwanabiofizikia, na mwandishi wa vitabu vya kisayansi. Mwanzilishi wa Injili ya Sayansi — taasisi inayounganisha maarifa ya kisayansi na imani.
Shiriki makala hii
5 min
6 min
4 min