Inapakia...
Inapakia...

Dr Brighton Shoo
Mwandishi na Mwenyekiti
“MSINGI WA TOFAUTI ZA KIJINSIA KATIKA UBONGO Jifunze Sayansi Ya Utofauti Wa Ubongo Kijinsia . Kila familia inalia na matatizo mbalimbali yanayotokana na namna ambavyo jinsia mbili kuu duniani zinavyoch…”
MSINGI WA TOFAUTI ZA KIJINSIA KATIKA UBONGO
Jifunze Sayansi Ya Utofauti Wa Ubongo Kijinsia.
Kila familia inalia na matatizo mbalimbali yanayotokana na namna ambavyo jinsia mbili kuu duniani zinavyochangamana. Kitambo nyuma watu wengi walikuwa wakiishi vizuri kwa kuzingatia mafundisho juu ya mienendo ya kijinsia kutokana na maelekezo ya vitabu vya Imani na mila na tamaduni. Lakini ghafla hayo yote yamepuuziwa sana, na watu wanategemea sayansi iwaambie, lakini nayo ghafla imejawa na jinsia mpya.
Madhara yake makubwa zaidi ni wanawake na wanaume kuishi tu kulingana na namna ambavyo muelekeo wa Maisha unawataka, na huu ndio msingi wa kuibuka kwa matatizo mengi sana, maana ni kweli unaweza amua kuishi vyovyote, lakini fiziolojia za ubongo haziruhusu kufanya lolote.
Malezi ya Watoto wa kiume ni sawa kabisa na malezi ya Watoto wa kike kwa miaka hii, kitu hiki hakijawahi tokea kabisa katika karne za nyuma. Yapo mengi tutakayo yaangalia katika kitabu hiki ambayo ukirejea katika jamii unaweza gundua ni kwanini sayansi hii inapaswa kusomwa tena.
Utangulizi
Mnamo mwaka 2001, taasisi ya afya ‘’institute of medicine’’ ambayo ni tawi la tume kubwa zaidi ya kisayansi ya taifa la Marekani ‘’National Academy of Science of U.S.A’’ walihitimisha kuwa, mara nyingi sana kumeonekana tofauti za kijinsia katika ubongo, kwa mtu mzima au hata aliye na shida, ijapokuwa bado tofauti hizi za kijinsia hazifahamiki kiundani zaidi (nukuu:Wizemann na Pardu, 2001)
Miaka kumi mbele tena taasisi nyingine kubwa ya kitaifa ya marekani inayoshughulika na matatizo ya kikakili ‘’National Institute of Mental Health’’ iliandika Jarida lenye kichwa kilichoandikwa ‘’Tofauti za Ubongo Kijinsia katika Ubongo, Tabia, Afya ya akili ‘’mental health’’ na Shida za Akili ‘’mental disorders’’. Na katika jarida hili walihitimisha kwa kusema, 1. Kuna upungufu mkubwa wa tafiti zilizojikita katika kugundua tofauti za ubongo kijinsia katika ngazi ya biolojia ya seli za ubongo ‘’neurobiology’’ na kiwango cha utendaji wa chini kabisa wa seli za ubongo ‘’mechanistic level’’, 2. Kuna tofauti Dhahiri kabisa za kijinsia katika ubongo na 3. Kuna uhitaji wa wanasayansi wengi zaidi wa ubongo ‘’neuroscientists’’, kuihusisha jinsia au sex, kama kitu kisichofanana katika tafiti zao au ‘’using sex as variable’’. ( nukuu: National institute of mental health, 2011)
Kuna tofauti nyingi sana za kijinsia katika namna jinsia ya kike na ya kiume wanavyo yadadavua mambo au yatambua mambo ‘’cognitive functions’’. Lakini pia kuna tofauti katika namna wanavyochakata hisia ‘’emotions’’, katika kujifunza, kumbukumbu, Lugha, Hofu, Wasiwasi ‘’anxiety’’, maumivu ‘’nociception’’, lakini pia tofauti za kijinsia zinaonekana katika namna baada ya kupata madhara ya ajali za kichwa ‘’brain traumatic injury’’, Shinikizo la damu ‘’stroke’’, matatizo ya umri ya ubongo ‘’neurodegenerative diseases’’ kama ugonjwa wa ‘’Parkison’s disease’’, ugonjwa unaoitwa ‘’Alzheimer’s disease’’, ugonjwa wa Amyelolateralsclerosis syndrome au ALS na ugonjwa wa Huntington’s disease.
Mfano, tazama jedwali hili.
Unaweza rejea nukuu kuhusu jedwali kwa (De Vries and Simerly, 2002; Simerly, 2002; Morris et al., 2004; Baron-Cohen et al., 2005; Cahill, 2006; Forger, 2009; McCarthy et al., 2009; Abel et al., 2010; Jazin and Cahill, 2010; McCarthy and Arnold, 2011)
Huu ni mfano mdogo tu wa namna ambazo hata magonjwa tu ya kiakili, nayo, hutokea kwa viwango vya kutofautiana kijinsia. Hivyo ndivyo ilivyo pia hata kwa namna za ubongo zinavyotofautiana kijinsia kwa sehemu kubwa zaidi, ambazo tunaenda kuziangalia.
Makundi Makubwa Matatu Ya Tofauti Za Ubongo Kijinsia.
Aina Ya Kwanza Ya Tofauti Za Kijinsia
Unaweza kugundua kuwa katika aina ya kwanza ya tofauti za kijinsia, zote zimejikita katika uzalianaji au uzazi. Hii ina maanisha katika swala la kuzaliana, kila jinsia huwa na sifa zake za upekee. Mfano mzuri ni tembo jike anayekuwa kwenye joto la kutafuta dume, huwa anatembea ya kipekee sana, huwa akibinua kiuno chake juu huku akitanua masikio yake, na huwa akijitembeza maeneo yenye madume, na wanapokuwepo madume hukimbia kidogo wamkimbize, na kisha husimama kwa mbele, hii inaitwa pia ‘’estrus walk’’, lakini kwa matembo dume huwa inakuwa tofauti kabisa, wao huwa na hasira kali sana na pia huzalisha mithili ya maji maji ambazo ni homoni katika tezi zao za pembeni ya kichwa ‘’temporal glands’’, tabia hizi hufanana kidogo na ngamia ambao nao, kwa ngamia dume huwa wanapohitaji majike, hutoa nje ulimi wao mpaka sehemu ya nyuma kabisa inayoitwa ‘’soft palate’’. na hapo huwa wakijisisimua kwa harufu za majike ‘’pheromones’’ lakini pia huwa wakizalisha homoni kutoka nyuma ya vichwa vyao ‘’poll gland’’ kwa ajili ya kuwasisimua pia majike, na huwa wakali sana. lakini pia unaweza Jifunza kwa kuku ambao wanapotoka kuhatamia mayai yao, huwa na hasira sana ukilinganisha na majogo. pia kuna aina nyingi sana za ndege wa kiume ambao huwa wanaimba katika kutafuta wachumba. Hizi sifa zote za nje ni matokeo ya mifumo tofauti kabisa ya kijinsia iliyomo ndani.
Aina Ya Pili Ya Tofauti Za Kijinsia
Aina ya pili ya tofauti za kijinsia, haijikiti kwenye sababu za uzalianaji tu, bali inajikita kwa sababu kiupana zaidi. Hapa kuna sababu mbalimbali ambazo zinaonekana kuhusiana. na miongoni ni sababu za kijenetikia. Tofauti nyingi hapa za kijinsia zipo kwa namna ya viwango. mfano uwezo wa kujifunza, kushikilia kumbukumbu za maneno kwa muda mrefu, kuhisi maumivu, uwezo wa kuhisi harufu, stress, msongo wa Mawazo, shida za misongo ya Mawazo n.k. sababu hizi hutokea kwa wote, lakini kuna jinsia moja huwa inaathiriwa zaidi. Kwa mfano, kuna ugonjwa wa akili ambao mtu akiwa nao, huwa anapitia vipindi viwili, kimoja huwa cha msongo mkubwa sana wa Mawazo, hata mtu anaweza kujinyonga au kuwa na hasira sana, au anakuwa anataka tu awe peke yake, na huwa ana msongo mkali sana wa Mawazo akiwa hana raha kabisa. lakini ugonjwa huu baada ya muda, huwa unahama na kuingia katika hali ambayo unakuta mtu, anakuwa na hisia za furaha sana, akiwa anahisi raha kupindukia. Huu ndio ugonjwa unaoitwa ‘’Major depressive syndrome au bipolar disorder’’. ugonjwa huu hutokea zaidi kwa wanawake. Ugonjwa huu umeonekana kuwa na sababu zaidi za kijenetikia, ambapo, kunakuwa na shida katika vinasaba au ‘’genes’’ ambazo zilipaswa ku control aina Fulani ya channel katika ubongo zinazoitwa ‘’L-type Voltage gated Calcium channels au Cav1.2’’, na tatizo hili kutokea zaidi kwa jinsia ya kike kuliko jinsia ya kiume kama ambavyo tafiti zilizofanywa kwa panya zimeonesha. tafiti zinathibitisha kuwa, tofauti za kijinsia zina sababu zilizo kwa upana zaidi. Huko mbele tutaona namna ambavyo wanawake wanauwezo mkubwa sana wa kumbukumbu za maneno na kuchakata lugha, wanauwezo mkubwa sana wa kuhisi harufu na Ladha n.k. na hizo zote zina maana kubwa sana kuzifahamu sababu zake kiundani kabla mtu mmoja hajachukuliwa faida ya kuchezewa kiakili kirahisi. Kwa tafiti hii unaweza pia rejea nukuu toka kwa (Dao et al., 2010)
Aina Ya Tatu Ya Tofauti Kijinsia
Aina ya tatu ya tofauti za kijinsia. hii ni aina ngumu kidogo kueleweka maana si rahisi kuigundua. Hapa kinachotokea ni kuwa, jinsia zote zinaonesha sifa moja au matokeo Fulani tu. Lakini namna ambayo wamefikia hatma hiyo ni tofauti. Mfano mzuri hapa ni swali la hesabu ambalo mwalimu aliwauliza wanafunzi wake baada tu ya kuwafundisha namna ya kulifanya. wanafunzi wa kiume walilifanya kwa kichwa tu, na tena kwa haraka sana. lakini wanafunzi wa kike walitumia muda mrefu sana kwa kurejelea maelekezo ya mwalimu. Wote walipata jibu sawa. lakini namna za ubongo za kuchakata lile swali zilikuwa ni tofauti. Kama tutakavyoona huko mbele, wanaume wapo vizuri sana katika kufanya kazi kwa kutengeneza taswira kichwani, hii huitwa pia ‘’spatial abilities’’. wanawake wapo vizuri sana kufanya kitu kwa kurejelea maelekezo ya maneno ‘’verbal abilities’’. kipindi utafiti huu ulipofanyika, wavulana walifanya fasta kwa kuwa wao huutumia sana uwezo huu wao wa asili kuliko wasichana, kipindi wasichana wanapotumia uwezo wao wa asili, ilionekana kana kama wapo nyuma ya wavulana, lakini haswa kilichotokea ni kuwa, walipita tu njia ndefu ila wote walifikia hitimisho lilelile.
Mpaka sasa hivi tafiti iliyofanywa tena, ya kuwafundisha baadhi ya wanawake nao kutumia mbinu kama wanayotumia wanaume, katika kutatua swali lilelile kwa kichwa, nao wameweza kufanya vilevile, na tena wengine hata wakagundua kuwa, kwa msichana yuleyule ambaye angecheza gemu la video kwa muda wa saa moja tu, basi angeweza kufanya kama walivyokuwa wanafanya wanaume. Aina hii inachoonesha ni kuwa, haimaanishi sana kuwa wanaume au wanawake wametofautiana katika namna ya kuchakata mambo mbalimbali, bali pia vipaumbele vya ubongo wao katika kutumia njia Fulani ni tofauti. Namna hii ya kutatua mambo kwa mbinu za kuvuta taswira ni moja tu kati ya maelfu ya tofauti za namna za kuchakata taarifa. Zipo namna ambazo haiwezekani kabisa kuigizia ambazo zinatokana na namna ya aina hiihii ya utofauti, mfano ni namna na tabia za uleaji, namna ya uleaji wa wamama ni tofauti kabisa na namna za uleaji wa wababa. Inaaminiwa kipindi kirefu cha mtoto kukaa tumboni kwa mama yake humpelekea mama kuwa na muunganiko mkubwa sana wa kihisia na mtoto wake, kutokana na mchanganyiko wa kihomoni baina yake na mtoto wake kwa muda mrefu. hii ndio sababu ya hisia za umama na malezi ya mama ‘’maternal care’’, lakini pia homoni za Vasopressin kwa wababa zimeonekana kuwa chanzo kikubwa cha hisia za kujali na matunzo kwa Watoto wao. wababa huwa na malezi ya upekee sana kwa Watoto wao ‘’robust care’’ kama tutakavyoangalia zaidi.
Jambo Moja laweza kuleta madhara tofauti kwa jinsia ya kike na kiume
Hii pia ni miongoni mwa sifa ya hapa. kitu ni kimoja ila kinaleta matokeo tofauti. Mfano mzuri ni ukiwapa wakati mgumu au stress au maumivu ya kisaikolojia wanaume na wanawake, namna watakavyoichambua watapelekea matokeo tofauti kabisa. Hii pia huitwa ‘’latent sex differences’’ na tena matokeo yanaweza kuwa kinyume kabisa kama ilivyo kwa tafiti iliyofanywa kwa panya jike na panya dume. Hawa walikuwa wakisumbuliwa kwa mtindo wa kila baada ya muda Fulani, kuwatishia kuwaingizia kitu fulani jichoni ili wafumbe macho, lengo lilikuwa kuona, je? Baada ya muda Fulani watazoelea na kufumba tu wenyewe hata bila ya kusumbuliwa. Matokeo yalionesha kuwa, wanaume walizidi kuonesha ubora wao kadri stress zinavyoongezeka. Na wanawake ilikuwa kinyume kabisa, wao walionesha kuzidi kudorora au kuathiriwa kabisa stress zilivyozidi kuongezeka. Tafiti ilibaini madhara zaidi katika chembe za Mikia ya seli za ndani kabisa ya ubongo au ‘’Dendrites’’ zenye kuhusika na kuchakata uundwaji wa uzoefu huu mpya zinazoitwa ‘’CA1 Pyramidal neurons’’ unaweza rejea nukuu ya tafiti hii (Shors et al., 2001)
Sababu Na Asili Ya Jinsia
Inafahamika kuwa zipo sababu kubwa tatu ambazo ndizo msingi unaopelekea jinsia ya kiumbe kuwa ya kike au ya kiume. Na sababu hizo, ni 1. Homoni 2. Jenetikia 3. Msukumo wa mazingira ya ndani ya mwili. Lakini hata hivyo bado wanasayansi wengine wameendelelea kusukuma hoja zao kuwa yawezekana kukawa na sababu zinginezo kama sababu za kisaikolojia. Kiuhalisia kumekuwa na Mdahalo mkubwa sana kutokana na hoja hizi.
Mpaka sasa hoja yenye nguvu zaidi ni hoja inayoonesha kuwa kiwango kikubwa sana cha tofauti za kijinsia ni sababu za kihomoni. Hii haimaanishi kuwa sababu zingine kuu mbili hazihusiki, ila ni kwakuwa imekuwa na Ushahidi mkubwa zaidi wa kisayansi. Mtazamo huu kwanza kabisa ulianza miaka ya 1800 ambapo mtafiti Arnold Berthold aliondoa korodani au testes kwa majogoo, na kisha akaona yamekuwa mapole sana ukilinganisha na tabia za majogoo wa kawaida. akaanza kwa kuhitimisha kuwa, kwa kuwa korodani au testes ndizo huwa zikizalisha homoni inayoitwa ‘’Testosterone’’. hii kwa wanaume ipo kwa wingi sana, na ndiyo huusika na tabia za ukali au ‘’aggressiveness’’ kwa wanaume, basi homoni ndiyo sababu kubwa zaidi ya tabia na msingi wa jinsia. Mnamo mwaka 1940 mpaka mwaka 1959, ndipo kulipofanyika maendeleo makubwa sana na kuzaliwa kwa sayansi ya Kugundua Tabia kama matokeo ya homoni katika ubongo ‘’behavioral neuroendocrinology’’. Hapa alikwepo mtaalamu Frank A. Beach ambaye tafiti yake ilichochewa zaidi na wataalamu wengine Phoenix, Goy, Gerall na Young ambao hao walitengeneza nadharia inayoitwa ‘’Organizational/ Activational hypothesis of Hormone action’’, hii nadharia inaelezea kuwa, homoni ‘’steroid hormones’’zinazozalishwa na tezi za uzazi ‘’gonads’’ kipindi cha awali kabisa cha Maisha ya kiumbe, ndizo hutengeneza msingi wa tabia za jinsia za huyo kiumbe, hutengeneza tofauti za kudumu za kijinsia katika seli na mifumo ya ubongo wa huyo kiumbe na tofauti hizi huchochewa na vipindi mbalimbali vya mabadiliko ya kihomoni kwa kipindi cha ukuaji wa kiumbe hata utu uzima wake.
Nadharia hii ikapata nguvu zaidi kwa sayansi za maendeleo ya kiumbe awali kabisa katika ukuaji wake. Imeonekana kuwa, Viumbe wote huanza awali kabisa wakiwa ni kama wana jinsia inayofanana, si ya kike, lakini inafanania. kuna sehemu chache kwa kila kiumbe ambaye anatengenezwa tumboni, ambazo hizi sehemu ndizo zinazohusika na kuamua jinsia ya kiumbe. Sehemu hizi pia unaweza ziita Nyuklia zenye seli kadhaa kadhaa hivi. Kuna nyuklia inaitwa ‘’INAH3’’ au ‘’Interstitial nuclei of Anterior Hypothalamus’’ . hii nyuklia ipo upande wa kushoto wa sehemu ya ubongo inayoitwa ‘’Hypothalamus’’, hii nyuklia inaaminika kuhusiana na kupendelea kutokea kwa jinsia Fulani. pia kuna nyuklia nyingine inayoitwa ‘’BSTc’’ au ‘’Bed nucleus of Stria terminalus’’, hii upo upande wa kulia wa sehemu ileile ya ubongo inayoitwa hypothalamus. Hii inaaminika kuhusiana na utambulisho wa jinsia Fulani tu.
Namna Jenetikia Na Homoni Zinavyosababisha Jinsia Ya Kiume Na Kike
Jinsia ya kiume huwa na chembechembe ‘’Chromosomes’’ zenye XY na jinsia ya kike huwa na XX. Hizi XY huambatana na vinasaba au genes zinazoitwa ‘’SRY’’. Hizi SRY sifa yake kubwa huwa ni kusisimua sensa au receptors za homoni za kiume ‘’androgens’’. Na baada ya kuzisisimua hizi hupelekea ukuaji au kuendelea kwa korodani ‘’testes’’ ambazo hizo hupelekea kuzalishwa kwa homoni inayoitwa ‘’Testosterone’’ kwa wingi sana. Hii Testosterone huelekea moja kwa moja mpaka kwenye Nyuklia inayoitwa ‘’INAH3’’, na hapo huisisimua hii nyuklia na kuifanya ikue. INAH3 inapokuwa imemwagiliwa na testosterone vya kutosha kwa wiki 12 toka mimba inapotungwa, basi hukua na kupelekea kuendelea kwa sifa na tabia za kiume. Ila inapokuwa haijamwagiliwa vya kutosha basi huiishia kwa kiumbe kuzaliwa na jinsia ya kike. Hii ina maanisha kuwa, Sifa za kiume huchochewa zaidi na homoni ambazo hupigilia msumari tabia za kijinsia. Lakini pia testosterone inapokuwa kidogo hata kushindwa kuzidi homoni zingine za kike zinazoitwa ‘’estrogens’’, huifanya INAH3 kushindwa kuendelea sana kwa ukubwa na hujibadilisha na kufanya kazi hata kupelekea msingi wa tabia za kike.
Kinasaba au gene hii inayoitwa ‘’SRY’’ ukiiondoa kwenye chembe au chromosome ya XY utaishia kupata kiumbe mwenye XY lakini ana tezi za kike ‘’Ovaries’’, na kama utaiweka hii gene ya SRY kwa viumbe wenye XX utaishia kupata viumbe wenye XX lakini wana tezi za kiume au korodani au testes. Na ndivyo itakavyokuwa pia sifa zao, atakuwa ana sifa za kike ila ana chromosomes za kiume au anasifa za kiume ila ana chromosomes za kike.
Tofauti nyingi sana za kijinsia zilizo katika kundi la pili, zimejengwa zaidi na msingi wa sababu za kijenetikia. Hapa tunazungumzia mfano utokeaji sana wa magonjwa Fulani kwa jinsia Fulani, au uwezo mkubwa wa kuwa na sifa Fulani kwa jinsia Fulani. Hii ni kutokana na kuwa, hizi X na Y chromosomes huwa zina genes mbalimbali ambazo huusiana na sehemu nyingine mbalimbali za mifumo ya utendaji wa kifiziolojia za jinsia Fulani. Mfano ile gene ya SRy pia imeonekana kuhusiana na utendaji wa nyuklia mojawapo ya ubongo inayohusiana na kuhamasisha au kudidimiza tabia kadhaa za ubongo, nyuklia inayoitwa ‘’Substantia nigra’’. Na pia inafahamika kuwa, kwa kuwa wanawake huwa na chromosomes za X nyingi, basi huwa kuna namna ya kuzifanya zisiwe sana na Nguvu kwa kuzimaliza nguvu baadhi, hii huitwa pia ‘’X inactivation’’, lakini bado baadhi huwa zinaponyoka kutomalizwa nguvu, na kujaa kwake huchochea zaidi baadhi ya sifa za kike. Na ni muhimu pia kutambua kuwa binadamu wote hurithi genes za Mitochondria kutoka kwa mama zao, na hii huchangia matokeo baadhi ya kijinsia.
Kuna sehemu za ubongo ambazo ni tofauti kabisa kati ya wanaume na wanawake, na mfano wake mkubwa zaidi ni sehemu inayoitwa ‘’SDN-POA’’ au ‘’Sexually dimorphic nuclei of preoptic nuclei’’ hii inatoa mwanga zaidi wa nguvu za miundo ya kijenetikia katika tofauti za kijinsia.
Mazingira ya ndani ya seli na mwili pia huchangia sana maendeleo ya jinsia moja zaidi ya nyingine. Mfano mzuri zaidi ni namna ambavyo stress, huwa na matokeo makubwa sana ya kuzisisimua genes za seli za ubongo, zinazohusiana na kumbukumbu kwa wanawake, zaidi ya kwa wanaume. Ambazo huitwa pia ‘’genes on hippocampal neurons’’. Lakini pia inafahamika kuwa , kwa mtoto ambaye anakua kuwa mwanamke huwa kuna mgandamizo mkubwa sana wa maendeleo ya ukuaji wa misuli ‘’masculinization’’, kupitia kitendo kinachoitwa ‘’DNA methylation’’, hiki kitendo kipo katika kundi la matokeo ya mazingira ya ndani ya seli au unaeza yaita ‘’Epigenetics factors’’.
NADHARIA ZA UTOKEAJI WA MASHOGA AU USHOGA
1.
Sababu za maendeleo ya ukuaji tumboni
Baadhi huanzia katika ile nyuklia inayoitwa ‘’INAH3’’ au ‘’interstitial nucleus of anterior hypothalamus’’, na kusema ikitokea kile kiwango cha testosterone ambacho kilipaswa kuisisimua hii nyuklia vya kutosha kikapungua kuwezesha kuikuza ile nyuklia kwa kiwango cha kutosha, basi huu ndio huwa msingi wa kwanza kabisa wa kuzaliwa mtoto mwenye sifa za ushoga. ambaye atakuja kuwa na sifa zinazofanania kidogo na za dada zake, kwa kuvutiwa na kaka zake.
2.
Sababu za Mama kuzaa Watoto wakiume wengi
Wapo wanasayansi ambao huja na nadharia nyingine kusapoti ajenda hii kwa kuonesha kuwa, Mama ambaye ana Watoto wakiume, kila anapozidi kuzaa Watoto wa kiume, wanaozaliwa huwa na asilimia kama 33% na kuendelea zaidi ya kumzaa mtoto wa kiume mwenye sifa za ushoga. hawa husema kuwa, mtoto wa kiume kadri anapokaa tumboni, baadhi ya seli zake zenye chembechembe za kiume (XY) zinapoingia katika mzunguko wa mama, basi mfumo wa kinga wa mama, huzitambua hizi kama hatari. ‘’hapa huzitilia mashaka chembe za kiume zinazoitwa Y-linked antigens’’ na kuzalisha chembechembe za kinga za kuziua hizi, au ‘’antibodies’’. na inapotungwa mimba nyingine ya mtoto wa kiume, basi chembechembe zake nyingi sana zinakuwa zikiuawa na mfumo wa mama hata kupelekea upungufu ambao ndio msingi wa kuzaliwa shoga. Na hawa wanasayansi wanathibitisha hoja yao kwa kupima viwango vya chembechembe za antibodies kwa wamama wenye Watoto mashoga, na kuwakuta wakiwa na uwingi sana wa chembechembe za protini kinga za ‘’NLGNY4-Y Protein’’ ukilinganisha na wamama wasio na watoto mashoga.
3.
Sababu za jenetikia za Kinasaba cha Ushoga ‘’Xq28’’
Hapa pana hitaji umakini sana, wanasayansi baadhi hukubaliana na kuwa, kuna uhusiano wa moja kwa moja wa hisia za ushoga, na sababu za kijenetikia za ndani ya viumbe. Yapo majaribio kadhaa ya kujaribu kutetea hoja hii ikiwemo, kupima uhusiano wa utokeaji wa tabia za ushoga kwa Watoto na ndugu zao, na kugundua kuwa, mashoga wengi huwa na wajomba wenye sifa pia za ushoga, hii ni kwa lengo la kuonesha kuwa, kwa kuwa sifa nyingi hubebwa na upande wa mama, basi kuna msingi wa kijenetikia nyuma ya sababu hizi. Iliwahi kutangazwa mwaka 1998 pia, kuwa chromosome X 28 (Xq28) ni gene ya ushoga, kwa kuwa ilionekana kufanana kwa asilimia 67% ya mashoga, haikuchukua muda hata kuonekana si kweli baada ya jaribio la kuthibitisha lililofanywa na wanasayansi wengine, kutokubaliana na hoja hiyo. na haikuishia hapo hata shirika lingine binafsi la tafiti za kijenetikia, lilipofanya nalo utafiti kwa sample kubwa zaidi, na kusema kuwa, wamegundua kuwa kuna uhusiano, lakini chromosome hii haihusiki na sifa za mipangilio ya kijinsia.
Kielelezo kwa Kondoo na ushoga
Wanasayansi baadhi waliendelea na uchunguzi wa sababu za kijenetikia za ushoga, hasa kwa kuwatumia zaidi Kondoo. ambao huonekana sana kuwa na asilimia 6-8% kuonesha kupenda kupandana madume kwa madume. na hivyo wanasayansi hawa kwa kufananisha nyuklia ya kondoo inayotofautiana kijinsia, inayoitwa oSDN ‘’ovine sexual dimorphic nucleus’’, na nyuklia ya binadamu. basi wakawa wakitengeneza uhusiano wa sababu zinazoweza kuwepo za kijenetikia. na hapa walisema kuwa, hii nyuklia ya oSDN kwa kondoo wanaopanda madume wenzao, au mashoga, ni ndogo kama vile ilivyo ndogo kwa binadamu mashoga. na wakagundua kuwa, nyuklia hii huanza kuundwa mtoto akiwa tumboni, hivyo hapa wakahitimisha kuwa, tabia za ushoga zaanza hata kabla ya kuzaliwa .Kielelezo cha mapacha na ushoga
Pia watu hawa wakafanya tafiti kwa Mapacha, hasa wale wakufanana, ambao hawa siku zote huwa wanafanana sana kutokana na kuchangiana sana jenetikia zao. Na hapa wakaja na hitimisho la kugundua kuwa, kuna asilimia kubwa sana ya pacha mmoja akiwa shoga na mwingine kuwa shoga, kama watakuwa mapacha wakufanana ukilinganisha na mapacha wasiofanana. Hii nayo kwao ilikuwa ni hoja ya kulenga kuwa, kuna sababu za kibiolojia kabisa za msingi Za utokeaji wa ushoga.
3.
Tezi ya Thyroid na Ushoga
Haukupita muda tena wakageukia na tezi ya Thyroid, ambayo ikaaminiwa kana kama ni miongoni mwasababu kubwa sana ya utokeaji wa ushoga. Hii ni kutokana na kuwa, wengi wa wamama wenye Watoto mashoga huwa na changamoto kadhaa za tezi za thyroid. na hata homoni za thyroid. ambazo huusiana na matendo mbalimbali ya kibiolojia ya maendeleo ya Watoto.
4.
Ushoga na faida za ‘’natural selection’’
Haikuchukua muda tena hata wanabiolojia kadhaa walipoanza kutafuta sababu za ndani kabisa za kwanini kuwepo na watu mashoga. Wengi wakawa na nadharia lakini nyingi zaidi zimejikita katika mtazamo wa kuwa, Familia inapokuwa na vijana mashoga, maana yake hao hawatazaa, maana yake vyakula na malighafi nyingi zaidi zitabakia kwa wanafamilia wengine ambao watastawi zaidi, kwa hiyo mashoga wapo ili kustawisha familia, na jamii zao. kwa kupunguza ugombaniaji wa maliasili zilizokuwepo. Lakini pia wapo wachache ambao walisema kuwa wapo mashoga ambao huwa na sifa chache baadhi za jinsia nyingine. hawa wakasema mashoga siku zote hupendwa sana na jinsia nyingine, mfano, shoga wa kiume huwa anapendwa sana na wasichana kwa jamii nyingi sana. huweza kuunda urafiki kirahisi na kushirikiana sana kutokana na kufanana kimitindo ya Maisha. na hivyo hii huwapa nafasi yao kuweza kupata wanawake kirahisi hata kama watakuwa na uwezo kidogo wa kuzalisha.
5.
Sababu za Ushoga kwa tafiti za kisaikolojia
Haikuishia hapo baadhi ya wanabiolojia wanasaikolojia wakaja na sababu zao kuwa, kila kiumbe huwa na aina mbili za uchaguzi wake wa jinsia, aamue kuwa kama mwanaume, au awe kama mwanamke. Na hivyo basi hayo ni maamuzi ya mtu. Kuna utafiti uliwahi fanyika huko miaka ya nyuma, ambapo wanaume waliokuwa wamepata ajali mbaya sana za kutoweza kufanya kazi kama wanaume imara, walihasiwa kama ilivyokuwa kwa matowashi, na wakawafanya waishi na wanawake na kushirikiana nao katika kila jambo. lengo lilikuwa baada ya muda wanaume hao wawe kama wanawake. Lakini cha ajabu ni kuwa, wanaume wale waliendelea kuvutiwa na wanawake, na kamwe hawakuwahi kuwa kama wanawake. Lakini hoja hii huendelea kutumiwa na wanasayansi baadhi ili kuonesha kana kama mtu kwa akili zake tu, anaweza kuamua kuwa mwanaume au mwanamke. kama vijana baadhi katika zama hizi wanavyoweza tu kuamua mashoga au wasiwe.
Mafanikio Makubwa Ya Nadharia Za Ushoga Kwa Jamii Za Wasomi
Kwa mara ya kwanza ikaonekana kuwa Ushoga ni matokeo ya kibiolojia ya mtu ambayo hana uchaguzi nayo. na ikaonekana kuwa hata wanasayansi makini kabisa wanaoweza aminiwa na jamii zao, pia wanatambua ushoga ni hali ya kibiolojia ya mwili ambayo inapaswa kuzingatiwa na kuheshimiwa, na tena, sio tu kuwa iheshimiwe kama hali inayotokana na changamoto, au kufeli kwa maendeleo ya mfumo wa jinsia ya mtoto tumboni, au matatizo ya akili (kama ulivyokuwa mtazamo wa wanabiolojia wakwanza kabisa wa Ubongo, Sigmund Freud). Bali iheshimiwe kama namna ya asili bora kabisa. ambayo asili tu haijaipa kipaumbele sana kwa kuwa haina ufanisi zaidi, katika kuongeza ongezeko la uwezekano wa uzalianaji. hii ni kama kusema, hii nayo ni jinsia. Kumbuka pia sayansi kwa karne na karne haijawahi kukubaliana na matendo ya ushoga, au matendo yanayoonesha kuvunja maadiili ya jamii. na hata Alan Turing mwanasayansi aliyefanya kazi kubwa sana katika maendeleo ya Computer na hata Artificial Intelligence, aliuawawa kwa kuhisiwa na kuthibitika kuhusiana kwa mapenzi ya jinsia moja au ushoga. Wanabiolojia wengi wamekuwa wakiutambua ushoga kama changamoto ya kisaikolojia inayohusiana na changamoto za uzazi. na sio hali yenye upekee kijinsia. lakini mpaka sasa mtazamo umebadilika sana hata ushoga kutambuliwa kama hali isiyo changamoto za kiakili.
Mafanikio Makubwa Ya Nadharia Za Ushoga Kwa Jamii Za Wana Dini
Hii ni hoja ya pili ila ndio kubwa zaidi. Kuweza kushawishi Taasisi za Dini ulimwenguni kuutambua Ushoga kama hali ya kibiolojia, ambayo inapaswa kukubaliwa kwa Upendo wa kiimani, kama vitabu vya Imani vinavyohamasisha upendo kwa mmoja mmoja, yalikuwa ni mafanikio makubwa sana. Vitabu vya Imani mara zote havijawahi kuukubali Ushoga, na ndio huitwa ‘’Sodomy’’ au matendo ya kichafu zaidi katika historia ya ulimwengu. Kitendo cha Dini mbalimbali kuweza kuukaribisha tena ushoga katika taasisi zao kama vile baadhi ya maKanisa, ni mafanikio makubwa ya ushoga hayajawai tokea. Kumbuka asilimia kubwa zaidi ya watu ulimwenguni na katika kila taasisi ni waumini wa dini zenye misingi mikubwa ya maadili. na ishara chafu zaidi ya mvunjiko wa maadili katika vitabu vyao, huwa ni ushoga. hivyo ushoga kuweza kukubaliwa tena kwenye taasisi hizi ni jambo la ajabu sana.
Ukisoma kwa mfano kwenye Biblia kitabu cha Warumi, sura ya kwanza kabisa, Paulo anakosoa na kuchukia vikali hisia za kuvutiwa na jinsia yako na ushoga kwa ujumla. lakini pia katika hiyo hiyo Biblia kuna kitabu kina sura moja tu kinaitwa Yuda, ingawa hakijaandikwa na yule Yuda iskarioti aliyemsaliti Yesu, ila hiko kitabu kinaonya na kutabiri kutokea kwa matenda ya kisodoma ya ushoga kwa siku za mwisho. hii tabia inakemewa sana pia kwa Imani zingine kama za Uislamu. kwa hiyo ushoga siku zote ulikuwa ni adui wa Imani za kidini. Ukristo haukuwahi ukubali ushoga hata mara moja. lakini sasa hivi zipo nukuu na rekodi mbalimbali hata za viongozi wakubwa zaidi wa Imani Duniani kama Papa wa Katoliki, ambapo Ukatoliki ndio Tawi Mama lenye wakristo wengi zaidi Duniani, utamwona mfano Hayati Papa Francis wa mwaka 2013-25 akiwashawishi wakristo na watu wote Duniani kuwakubali mashoga bila kuwashutumu. Japokuwa imekuwa ni sera ambayo hubadilika kulingana na Papa aliyepo. Lakini hata hivyo bado madhehebu mengi kama ya Anglican yamenukuliwa yakikubaliana na mitazamo hii. hoja kubwa ambayo imekuwa ikitumika imelenga hisia za kutohukuma wengine, au kutokukubaliana na ushoga lakini kuupokea kimtazamo wake. hebu tuliangalie jambo hili kwa upande mwingine tena.
Namna Biolojia Ya Kisasa Zaidi Inavyoshirikiana Na Biblia Kuwa Ushoga Sio Hali Ya Kijinsia Yenye Sababu Za Kupokelewa Kimaadili
Hoja ya kwanza
Mtazamo wa kuwa vinasaba vya jenetikia, kuanzia molekuli kuja Genes na DNA kwa ujumla vinahusika na Tabia ya mtu, au mwonekano wake ‘’phenotypes’’, ulikuwa ni mtazamo wa zamani sana. Hakuna namna ambayo unaweza mweleza mwanabiolojia ya kisasa kuwa kuna kinasaba cha ushoga ‘’Gay gene’’ kama ile chromosome ya 28 (Xq28). Na hata kama zingekuwepo za mtindo huo elfu na zaidi, bado kusingekuwa na hata hoja ndogo ya kutengeneza msingi wa kuwa hiyo ndiyo sababu za utokeaji wa ushoga.na hata hoja hiyo juu ya kuwa ipo hiyo chromosome ya 28 na zingine chache sana zinazohusiana na ushoga sio ya kuaminika sana kwa kuwa bado ina mashaka ya ukweli wake.
Tabia na Sifa ni muunganiko wa mifumo mingi ambayo haitokani na sababu za kijenetikia tu. Na hata mwonekano wa kitu kimoja ni matokeo ya maelfu ya vinasaba ‘’polygenes’’ , ambavyo bado havileti matokeo vyenyewe bali kwa nguvu za mazingira ya ndani ya mwili na ya nje ya mwili. mifumo ya mwili yenyewe tayari inajua inataka kuumba nini na kuamua kuumba kwa kutumia viilivyomo tayari katika mwili ambamo vinasaba ni sehemu moja tu kati ya maelfu ya vitu. Hakuna vinasaba vya kuunda jinsia ya kiume au kike au ushoga. Kuna mifumo mipana kupita kawaida inayopelekea uumbaji wa jinsia ya kiume au ya kike, na mifumo hii hutumia maelekezo toka juu kabisa kuanzia kwenye utambuzi, mazingira, mifumo ya mwili, ogani, tishu na seli na pia hutumia maelekezo toka chini kabisa kama molekuli, vinasaba yaani genes, DNA na protini na channel za protini. Na huchakata taarifa hizi toka pande zote mbili na kurekebisha changamoto kama ipo katika sehemu mojawapo, na kuboresha uumbaji hata kuunda sifa Fulani nzuri bila kujalisha changamoto mojawapo.
Ukitaka kuelewa kirahisi zaidi vuta picha nyumbani, Kisu kibutu, Nyanya moja imeoza nusu, kitunguu kimeanguka chini, maji yamebakia kidogo, mafuta yanaelekea kuisha, dagaa wapo wengi na vizuri, chumvi inaelekea kuisha na sufuria na moto vipo. Swali je, Unaweza pika mboga ya dagaa ikaweza lika tena ikiwa vizuri? Kwa kila mpishi aliyetimamu lazima atasema inawezekana. Kwa kuwa mboga haiamuliwi na kuharibika kwa vitu Fulani, ina amuliwa na akili ya mpishi, kama kuna maji na chumvi kidogo, maamuzi yanaweza kuwa ni kupika dagaa wachache ili kukidhi balansi ya viungo, nyanya mbovu inaweza katwa palipoharibika, kitunguu kilichoanguka kinaweza oshwa au ondolewa sehemu chafu kwa kutumia kisu kwa kutegemea na kiwango cha maji. Haya maelezo ni mfano tu wa namna ambavyo mifumo ya mwili huunda sifa Fulani hata kama kuna shida nyingi sana za mazingira yake au jenetikia zake. haiendi endi tu kama wanabiolojia hawa wanaohisi changamoto moja katika kinasaba Fulani au homoni Fulani au tezi Fulani basi moja kwa moja hupelekea matokeo Fulani. Unapokuta changamoto imejitokeza kibiolojia basi ujue, ni matokeo ya mifumo mingi katika kupambana na matatizo mengi hata kuishia katika hali hiyo. na sio kuwa yale matatizo ndiyo yamepelekea shida hiyo moja kwa moja. Rejea kwenye kisa cha juu, uchache wa mboga iliyopikwa katika mazingira yale, sio matokeo ya shida za wale dagaa, nyanya na vitunguu n.k ka tulivyoona pale juu, bali ni matokeo ya akili ya mpishi kuona walau hayo ndiyo matokeo yenye madhara ahueni zaidi, na wala sio lengo la mpishi, pia kumbuka ni namna tu hakukuwa na njia.
Jaribio zuri zaidi ninalopenda kulitumia nikirejea toka kwa Profesa wa Fiziolojia toka chuo cha Oxford, Ruparte Sheldrake katika kitabu chake ni hili, Kipindi cha awali kabisa cha ukuaji wa kiumbe kama mmea au mnyoo Fulani, huwa unaonekana kama ka umbile kadogo sana ka mviringo ambako tayari huwa kanakupa ramani wapi pataendelea kuwa sehemu za juu na wapi patakuwa sehemu za chini na sehemu za nje na za ndani pia. Sehemu zinazoendelea kuwa za juu kwa mfano, seli zake huwa zinaanza kuonesha upekee ili kuja kuunda upekee wa mmea au mnyoo. Huwa kwa sehemu zake za juu, hivyohivyo kwa sehemu za chini, kati, ndani na nje na ujumla. Sasa basi, kwa umakini sana Zitoe au ziue seli zote zinazoelekea katika uumbaji wa sehemu za juu kwa kulenga zaidi kuua mpaka vinasaba vyake. Na kisha usubirie matokeo ya kiumbe atakae kuwa mkubwa, je atakuwaje? Atakuwa mwenye kuzikosa hizo sehemu? Kwa kuwa umeshaua seli zake zote na chembechembe zake zote ambazo huwa anazitumia kwa ukuaji wa sehemu za juu. Matokeo: Maajabu. Kiumbe hukua akiwa mzima na sehemu zake zote. tena kama tu ambaye hakuondolewa chembe zake za awali kabisa za ukuaji wa sehemu za juu. Ila tu, atakuwa mdogo kiumbile ukilinganiisha na yule ambaye sehemu zake hazijatolewa, na sababu ni kwakuwa alikuwa na malighafi chache na si vingine.
Hii ina maana gani? Hii inamaanisha kuwa, Uumbaji wa Maisha na mifumo na sifa kwa ujumla, kama unavyozungumzia sifa za kuwa wa kiume au sifa za kuwa wa kike, ni matokeo ya mifumo ambayo inalengo maalumu la kuumba jinsia Fulani. Na sio Matokeo ya kilichopo pale. kama wanasayansi wote wanaosukuma ajenda ya kuwa, ushoga na jinsia zingine ni matokeo ya jenetikia au vinasaba Fulani au mazingira Fulani tu. Hiyo haina maana kabisa na wala haina nguvu kisayansi kabisa. Nukuu chini zote zinalenga kukuonesha kuwa, Jenetikia ni sehemu ndogo sana ijapokuwa ni ya muhimu inayoshiriki katika uumbaji wa Maisha. na katika nukuu za mwisho kuna hoja nitaielezea zaidi mbele.
Rejea kwanza nukuu zifuatazo:
Venter 2007 ‘’Moja ya Gunduzi kubwa zaidi nimeweza igundua katika Maisha ya utafiti wangu wote ni kwamba, huwezi kuelezea Maisha ya binadamu au Maisha ya kiumbe yeyote yule kwa kuegemea katika DNA pekee. kwanini? kwa kuwa mazingira ya kiumbe ni ya upekee uleule kama ilivyo jenetikia yake au genetic codes zake’’
Denis noble 2015 ‘’ Hakuna Computer ambayo unaweza ingiza DNA au kinasaba chako cha jenetikia na kisha ukatengeneza maisha zaidi ya Maisha yenyewe. achana kabisa na mtazamo wa Maisha kama chombo cha usafiri, Kiumbe hai ana funguo zake za kuifungua na kuitafsiri DNA yake yeye mwenyewe na kuitengenezea maana’’
Bird 2007 ‘’Kinachoamuru protini gani iundwe na kwa kiwango gani, sio vinasaba au DNA pekee, Seli mbalimbali na tishu mbalimbali hutumia DNA ileile kutengeneza miundo mbalimbali ya kuunda viungo mbalimbali ‘’various gene expressions from same DNA’’, Kinachotofautisha seli ya Moyo, seli ya mfupa, au seli ya kongosho ni seli na tishu zenyewe, za hivyo viungo, ambazo hutafsiri DNA zilezile, tofauti tofauti kuunda seli zao kwa kutokana na kuwa na viwango mbalimbali, vya chembechembe za kuunda protini ‘’transcription factors’’, na chembechembe za nje ya DNA, zinazoboresha miundo ya uundaji wa kijenetikia ‘’epigenetic marks’’
Hillenmeyer 2008 ‘’Tofauti nyingi za kijenetikia, aidha kutoka kwa vipisi baadhi ya chembechembe za DNA (knockouts), au makosa yanayoharibu mpangilio wa DNA (mutations), huonekana kabisa kutokuwa na madhara yoyote kwenye mwonekano wa kiumbe (no significant phenotypic effect) au huweza kuwepo madhara katika mwonekano lakini madogo sana, madhara huonekana mara nyingi zaidi pale ambapo kunakuwa na stress kwa huyo kiumbe.
Kwa mfano, Tafiti ya kuondoa kabisa, yaani unaondoa vyote vinasaba ‘’genes’’ kwa fangasi wa amila ‘’Yeast’’, hakukupelekea madhara yoyote kwa mwonekano wa nje wa fangasi huyu (no phenotypic changes) kwa asilimia 80% ya majaribio yote. Lakini hata hivyo, walipowatengenezea stress fangasi, matokeo katika ukuaji yalionekana kwa asilimia 97%’’
Noble 2008c ‘’tafsiri ya tafiti ya fangasi ni kuwa, Tofauti zote katika ngazi za kijenetikia (genome level) huwa zinarekebishwa na mwili wenyewe ‘’buffered’’, huwa kuna njia za alternative zinazoenda katika ngazi za chini kama kuelekea kwa chaneli za chini kabisa za gene na protini na kisha hurekebisha makosa yaliyotokea ili kuruhusu utendaji uendelee katika viwango vya juu kama katika seli, tishu na ogani na mifumo’’.
Laforge 2004, kaern 2005 na Kupiec 2008,2009, hawa wote walisema ‘’Kuna uwepo wa namna ambayo vinasaba au genes kama vinaelekea tu katika utendaji wa namna Fulani tu (existence of stochastic gene expression), hii namna inaruhusu tu utokeaji wa namna Fulani tu ya utendaji na mwonekano katika ngazi ya tishu na organs.’’ Inajaziwa pia kwa kusema ‘’ upendeleo huu au Selection kwa sifa Fulani tu, ndio msingi wa mafanikio ya viumbe hai kwa kuchagua tu zile tofauti zenye dhumuni katika maisha’’.
Weaver 2004, 2009 ‘’Wataalamu wa Ubongo waliofanya utafiti kwa makundi ya panya wamegundua kuwa, makundi ambayo hayakutani na changamoto sana, hulea Watoto wao kwa muda mrefu sana, lakini makundi ya panya yanayopambana sana na hatari za kuwindwa na predators, hulea Watoto wao kwa muda mfupi sana. Cha ajabu ni kuwa, hii tabia hurithishwa kwa Watoto wao, (yaani panya akianza kuwindwa sana, ataanza kulea kwa muda mfupi Watoto wake, na atarithisha hii tabia kwa Watoto wake), huu ni mfano wa moja kwa moja wa matokeo ya mazingira kuhamasisha sifa za kijenetikia (Epigenetic effects), na matokeo haya yalipimwa na kuonekana katika seli za sehemu ya ubongo inayohusika na kumbukumbu au hippocampus’’
Barbara McClintock kwenye presentation ya Tuzo ya Nobel prize yake,1983 anasema ‘’kuna uhusiano endelevu kati ya DNA na mazingira yake.
Je! Unaweza kuwajibu Kuhusu Xq28 (Gay Gene-Kinasaba Cha Ushoga)?
Naam, kama Ushoga utaendelea kufanyika kama tabia ya muda mrefu. Na akili za watu zitaelekezwa katika ushoga. Tunategemea kuona tabia hii ikishuka chini na kupelekea matokeo katika ngazi ya jenetikia au ‘’genome’’. Hii ni kopi tu ya tafiti ambayo imekwisha fanywa na Weaver kwa panya unaweza rejea nukuu ya juu. Kumbuka, wanabiolojia wasiojua na kuelewa swala hili wanaweza kuhisi kuwa genome hii ambayo ni matokeo ya juu kushuka chini, ndiyo sababu ya chini kuelekea huko juu. Ni kama sasa panya wote waliorithishwa tabia ya kulea kwa muda mfupi, itakuwa kana kama kwa mtu atakayewagundua kwa mara ya kwanza, basi jenetikia zao ndio zimewafanya kuwa hivyo. Kwa hiyo Xq28 haina sababu zozote zile za nguvu za kuhalalisha ushoga kisayansi na hapo ndipo tunagundua Biblia ilishaijua ‘’Epigenetics’’ kitambo kabla yetu na ndio maana imekataza ushoga hata kabla ya neno sayansi au biolojia linasimikwa.
Hoja Ya Pili
Ufanisi wa Uumbaji wa Kibiolojia. ‘’fine biological tuning’’. Tazama hatua kuu za uumbaji wa jinsia kwa kila kiumbe.
Hoja kuu ya pili ni kuwa, katika mfumo mzima wa uundwaji wa jinsia. Hakuna sehemu ambayo ina nafasi ya maendeleo ya hali tofauti na hali za jinsia ya kiume au ya kike. Hakuna kipindi ambacho jinsia ya kiumbe haifahamiki kama ni ya kiume au ya kike. Hata kipindi kabla ya wiki ya sita ambapo tezi za uzazi zinaanza kuundwa, tayari jinsia huwa zinafahamika, na hata muda unapoendelea, jinsia huwa pia inafahamika. Kitu pekee kinachotokea ni maendeleo ya jinsia Fulani kuzidi kujidhihirisha zaidi. Hivyo basi, katika mfululizo wa matendo haya, hakuna channel inayoelekea kuunda shoga na wala huwezi tabiri tokea hatua ya awali kabisa. Hivyo hoja za kuwa kuna sababu za ushoga kibiolojia hazina msingi katika fiziolojia inayoonekana ya uumbaji wa kijinsia.
Miongoni mwa hoja tulizoziona za kutokea kwa ushoga ambazo zilijikita katika utendaji wa nyuklia ya INAH3 ambayo ilihisiwa kuwa, kwa utendaji hafifu wa zile genes za SRY zinazohamasisha utendaji na uzalishaji wa Testosterone, katika kuhamasisha nyuklia ya INAH3 (hii inahusiana na sifa za kiume) na kupelekea kutokea kwa hali ya ushoga . hoja hii haina mashiko kabisa kwa kuwa mpaka sasa kinachofahamika ni kuwa, hauwi na sifa za kike kwa kupungukiwa ukuaji wa INAH3. unaotokana na vichochezi vya kuwa mwanaume, ambavyo ni SRY-protein. Bali imegundulika kuwa, Ovaries ambazo huchelewa sana kuanza mabadiliko yake kupelekea sifa za kike, huwa na matendo mengi ya kibiolojia ambayo ni complex sana. Na sio kama walivyohisi wanabiolojia waliohisi kwa kutumia tu INAH3 na nyuklia zingine chache zinazohusiana na tofauti za kijinsia, basi unaweza pelekea jinsia Fulani.
Hii ina maana gani?
Ushoga Kwa Namna Nyingine Ni Changamoto Ya Kibiolojia Na Sio Jinsia
Bila kutumia biolojia hii hauwezi mridhisha mwanasayansi anaeamini kuwa ushoga ni hali za kijinsia kama zilivyo zingine, akakubali. lakini kwa kurejelea matendo ya uumbaji yanayotokea kipindi cha uundwaji wa jinsia, tunaweza kuona Dhahiri kuwa, Hakuna njia zenye upekee zinazoelekea katika kuumba hali ya ushoga. ila tunaona hatua baadhi zinazofeli na kisha zinaishia kwa kutokea kwa hali ya kiumbe kuwa na changamoto za maendeleo ya kijinsia. Kumbuka, watu wengi wanachanganya hali za kutoendelea kijinsia vizuri, na hali za kutamani mapenzi ya jinsia moja. Hebu tuangalie zaidi hoja inayofuata.
Hoja Ya Tatu
Hoja zenye Kutetea Ushoga na mapenzi ya jinsia moja zinakosa nguvu kifiziolojia na kwa sayansi za asili. Kipindi mwanaume anapokuwa na mwanamke, hawa wawili kifiziolojia ni kama funguo na kufuri au ‘’complimentary pairs’’. Urefu wa uume ndio urefu wa uke, sperms za kiume zinahitaji oocytes za kike kuungana. Fiziolojia na homoni za kike ndizo zinazomvutia mwanaume, na vivyo hivyo kinyume. Saikolojia ya mwanamke, inamuhitaji mwanaume ili ilete maana na kinyume chake vivyo hivyo. Uwepo wa jinsia hizi ndizo sababu za uwepo wa kila kiumbe hata leo anayeitwa binadamu. Asilimia zaidi ya 99% ya viumbe wa jamii za binadamu, wote huifuata sheria hii. Kukubaliana na ushoga kama ajenda yenye sababu za kibiolojia kuna hitaji Imani kubwa sana na sio sayansi.
Kutamani kimapenzi jinsia yako sio ajabu. Ni kama isivyo ajabu kutamani kula nyama ya mwenzako. Ila Ajabu ni kuhisi hayo sio matatizo ya akili au saikolojia. Na kama matatizo ya kisaikolojia yanaweza kuwa na sababu za kibiolojia, basi biolojia imetumika kumaanisha sababu yoyote ile aliyonayo kiumbe hai. Ni kama ule msemo unaosema, kila jibu ni jibu. Ila kama Biolojia inatumika kama sayansi ya uhai na viumbe hai, hakuna biolojia inayoweza kuelezea hisia za kuunganisha aidha Uume na Sehemu ya kutolea kinyesi. na wala hakuna sababu za kibiolojia zinazoweza kuelezea uhusiano wa kuunganiisha uume na kinywa cha kumeng’enya chakula. Kwa kuwa tayari hii ni mifumo isiyo na uhusiano kabisa kibiolojia ya matendo ya kujamiiana kwa ajili ya uzazi. na kuna maelfu ya madhara na hatari za afya ambazo zinaweza kamilisha mamia ya vitabu kuonya tu hatari zake. Na ndio maana maelfu ya miaka imepita bila jamii za viumbe kukubaliana nayo kama desturi njema mpaka sasa wanasayansi wanapochochewa kukubaliana na ajenda zisizo na mashiko.
Kumbuka pia, namna ya kudanganya milango ya fahamu hata kupata msisimko kama inavyopaswa kwa matendo halisi ya kibiolojia, ni sayansi nyepesi sana. na kuna wakati huwa ina faida. ila sio kwa mazingira haya. kutumia sehemu ya aja ‘’Rectum’’ kama uke, kunaweza leta msisimko feki tu kama inavyowezekana pia kwa kutumia mikono na sabuni ‘’masturbation’’. au kwa kutumia midoli ya ngono ‘’sex toys’’, au uke wa kisasa ‘’artificial vagina’’ kama tunavyofanya tunaopokusanya mbegu toka kwa ng’ombe au farasi. Lakini uwezekano huu wa kupata msisimko haumaanishi biolojia inakubaliana na matendo hayo, hizo ni triki tu na hazipaswi kuwekwa mezani katika mijadala mizito ya kisayansi.
Hoja Ya Nne
Changamoto zote zinazohusiana, na kupelekea mwanaume kuishia au kuzaliwa akiwa na sifa chache za kiume, au akiwa na sifa baadhi za kike. na pia changamoto zote zinazohusiana, na kuishia mwanamke kuwa na sifa chache za kike, au kuwa na sifa baadhi za kiume. zinapaswa kuchukuliwa kama matatizo ya Kijinsia yaliyotokea kipindi cha uundwaji wa kijinsia. Na ni vyema wanasayansi kutumia taaluma zao zote, kufikiria kutatua au kuweza kutatua changamoto hizi, pale inapoonekana inaweza tatuliwa kabla haijatokea.
Hakuna Hisia Ya Asili Ya Mwanaume Kutamani Kuingiliwa
Hii ni mbinu ya kushawishi kuwa mfano mashoga huwa na misisimko ya kutamani jinsia zingine, kwa mfano. Tafiti nyingi zimebainisha kuwa, jasho la mwanaume ambalo hutoa harufu za homoni ‘’pheromones’’ zenye kuwasisimua wanawake wanapokuwa kwenye joto, zinazoitwa ‘’androstadinone’’, pia huwasisimua na mashoga wa kiume. Tafiti kama hizi ambazo mtu anayezisoma anaweza kuamini kabisa kuwa, basi watu hawa wanatamani kuingiliwa kinyume na maumbile, hazina kabisa maana hiyo. Hii ni kwa kuwa kipindi mwanamke anasisimka kwa harufu ya homoni za mwanaume, msisimko wake huusiana na mihemko ya neva za fahamu zinazoenda moja kwa moja mpaka kwenye Clitoris iliyopo katika uke, na sehemu zingine za via vya uzazi, na sio mfumo wa kutoa taka au rectum. Na ndiyo maana hata msisimko huu kwa wanawake huwatokea wanapokuwa tu katika siku zao za hamu, au joto. Kwa hiyo hakuna Ushahidi wa kifiziolojia wa msisimko wa Rectum kwa homoni za kiume. Wala hakuna muunganiko wa mfumo wa fahamu katika channel hiyo.
ila Inafahamika hasa kwetu wataalamu wa Wanyama ambao hutumia ‘’Rectal Probe’’, ambayo unaiingiza katika sehemu ya nyuma ya mnyama na kisha ukiisisimua, unamfanya mnyama anasisimka hata kumwaga shahawa au sperms zake, na unaweza zikusayanya. hapo kinachofanyika hasa ni kutumia mbinu zilezile za kutriki fiziolojia, ambapo, kwa kutumia uhusiano wa mazingira zilizopo neva za mihemko ya uume, na neva zinazoelekea kwenye sehemu ya haja, au ‘’rectum’’, zote huusiana kwa kutoka kwa tawi moja la neva linaloitwa ‘’sacral plexus neva ya S2 na S3’’. lakini pia, eneo hilo huwa linasisimka sana kwa mitetemo, lakini sehemu ya nyuma ‘’rectum’’ yenyewe haipo kwa ajili ya mitetemo hii. haipo kwa ajili ya uume na wala haina mikunjo ya kusapoti uume. na hata haina ute ute wa kuilainisha kama ilivyo kwa uke. kwa hiyo ushoga, na tamaa ya mapenzi ya jinsia moja, hayana nguvu kisayansi, ila yanawezeshwa tu kwa triki za kifiziolojia. Mashoga huweza kuvumilia na kusisimka kwa kuwa, pia sehemu ya ndani ya utumbo huu wa nyuma wa haja ‘’serosa’’, bado haina sensa za maumivu. Na kadri wanavyomwagiwa mbegu, ambazo huwa na enzyme zinazoitwa ‘’Transglutamase enzyme’’, sehemu yao ya nyuma hutanuka zaidi ukuta wake, na hii huwafanya kuwa hatarini sana kuharisha kwa utumbo wao kushindwa kufyonza maji vizuri, lakini pia huwa hatiani zaidi kupata mashambulizi mfano ya UKIMWI, Fangasi, na Bakteria. maana kinga ya sehemu hii hushushwa na enzyme hii ‘’TGE’’. Na hii ndiyo sababu zamani iliaminika Ushoga tu ndiyo unahusiana na maambukizi ya UKIMWI.
Wapo watu wanaotamani kufanya mapenzi ya jinsia moja, bila kuwa na udhaifu wowote ule, hawa wote wanashida za kibiolojia ambazo hasa ni za kisaikolojia. Tabia hizi zimejaa magerezani na kwa jamii baadhi za watu. Hizi tabia zinaweza kusomwa kiundani zaidi kwa wataalamu wa akili na tabia kama changamoto za kitabia, za kiuraibu, au mitazamo, au kama zinavyosomwa tabia zote zisizozoeleweka. Na kwa kitabu hiki, utazitambua zote kwa sehemu inayofuata.
Wanyama Sio Kielelezo Cha Ushoga
Mifano ya Wanyama sio kielelezo cha mwisho kabisa cha kuelezea tabia za binadamu. Wanyama huzaa na wazazi wao na kuna wakati hula hata wenzao. Hatuwezi Jifunza kila kitu, msomaji anapaswa kutambua kielelezo cha kondoo kwa kujifunzia ushoga hakina maana kabisa. Maana kondoo huwa hawafanyi ushoga kama wanavyoonesha katika vielelezo hivi, ni kama ilivyo kwa nguruwe ambaye anapoona tu muinuko, anahisi kuupanda kama anavyopanda majike, na ndivyo wanaokusanya mbegu za kiume za nguruwe, hufanya kwa kuwawekea ubao ambao wao huupanda. Hii pia hutumika kwa ng’ombe ‘’teaser bull’’, ambao husimamishwa na tena unaweza wamwagia homoni za estrogens, na ng’ombe dume mwingine anapomwona humpanda kwa kuhisi tu harufu, au bila hata harufu bali kwa kuzoea tu kama wanavyofanya NAIC Arusha. na hapo wakusanyaji hukusanya mbegu kwa kutumia uke wa kisasa ‘’artificial vagina’’. lakini kabla hujatumia kielelezo cha kumtumia mnyama kama kielelezo cha ushoga, unapaswa kujua nini hasa kilichopo katika ubongo wa huyo mnyama. Ubongo wa kondoo hauoni ulimwengu ambao ubongo wa mwanadamu unauona, hata angekuwa nyani bado, lakini bado naye hana uhalisia huu. Kondoo hafanyi ushoga kwa mantiki ya binadamu, anafanya kwa mantiki ya nguruwe, yaani tabia zao za uzalianaji zimejikita katika kuzoelea mazoea ya asili ya utendaji, na homoni, zaidi ya utambuzi wa wanachokifanya. Na ndio maana ng’ombe hawazi baada ya kumwaga shahawa zake kwenye uke kama ilivyo kwa binadamu, ambaye huwa akiwaza nini kitatokea baada ya hapo.
Hoja Ya Tano
Ushoga unaenda kinyume na hatua ya mwisho kabisa ya fiziolojia ambayo ndio Utambuzi au Akili. Tafiti kama tutakavyo angalia huko mbele zinaonesha kuwa, asilimia kubwa ya Watoto wakiume huwa hawapendi kabisa kufananishwa na wanawake, au huwa wanachukia sana Tusi moja kubwa zaidi kwao, ambalo hulenga kuwafananisha na kuwa, ‘’wanaingiliwa kinyume’’. Kwanini wanaume hawapendi kabisa hali hii, na ndio asilimia zaidi ya 99% ya wenye jinsia kamili ya kiume? Tafiti huonesha kuwa, wengi karibia na wote kuwa hawapendi, ina maanisha kuwa, sio maamuzi ya mmoja ila ni matokeo ya fiziolojia kuwajengea saikolojia hiyo. Na hii ndiyo sababu hata takwimu nyingi zaidi huonesha kuwa, Mashoga wengi hubaguliwa na jamii zao, hii ni kuonesha kuwa, wengi hawavutiwi na tabia hizi ambazo zinapingana na asili zao. Natambua kuwa kadri siku zinavyozidi Kwenda mbele, ndipo kiwango cha ushoga kwa watu kinavyozidi kuongezeka. Lakini sio lazima takwimu hizi zichukuliwe katika zama hizi. ila hoja ni kuwa, saikolojia za wanaume huwa dhidi ya utokeaji wa tabia za ushoga kwa mara nyingi zaidi, katika mara zote.
Kama ilivyo vigumu kupingana na biolojia ya mwili wako. mfano, kukubali maumivu. ndivyo ilivyo pia vigumu kukubaliana na mwanaume kujitangaza yeye yuko radhi kuingiliwa kinyume na maumbile. Mapenzi kati ya mwanaume na mwanamke ni sifa ya kawaida, na hata wanaume wengi wasanii huiimba pale wanapofanya mapenzi na wanawake. Hii inaweza kukupa majibu kuhusu ni kwanini hoja hii ina nguvu sana ya kuwa, Ushoga unapingana na hatma ya fiziolojia ya kijinsia kiakili.
Kitu kinachomaliza kabisa hoja za kuwa, uwepo wa ushoga unasaidia kupunguza ushindani wa maliasili, na kuchochea zaidi uwezo wa kuishi kwa wanaobakia, au Watoto, haina mashiko kabisa. maana imejengwa toka hoja ya Darwin ya kuwa, tuko tukishandana, na mshindi ndie ananafasi zaidi ya kuishi. Hoja hii imepitwa na wakati katika biolojia. Na hata wanadarwin wengi saivi hutumia msemo mwingine kuwa anaeishi ni mwenye bahati zaidi. Yaani, ‘’survival of the Luckiest not the fittest’’, hata hivyo hoja hizi zote bado hazina mashiko, mfano. Kama kuna kundi moja tu ndilo huwa na asilimia kubwa zaidi ya kuishi, kwanini kila muda huwa makundi yote yanakuwepo. Mfano kuna nadharia husema, kama wanaume wazuri tu ndio wananafasi kubwa zaidi ya kupata wanawake, na kusambaza uzazi wao, kwanini kusiwepo kwa kizazi chenye watu wazuri zaidi wengi zaidi. kwa kuzaliwa zaidi kutoka kwa baba zao wazuri, ambao ndiyo wanapata wanawake wengi zaidi? Nakumbuka miongoni mwa majibu ambayo wanadarwin walijaribu kuyajibu ni kusema kuwa, watu wengi wazuri pia huwa na asilimia kubwa zaidi ya kuwa na mfumo bora zaidi wa kinga. na hawa wanasema hivi kwa kuwa uzuri ni mfanano wa pande mbili za maungo au ‘’symmetry’’, ili uwe na huu mfanano unapaswa uwe na mfumo imara na usiofanya makosa mengi katika uumbaji wa kijenetikia. ili sehemu zifanane.
Kwa hiyo mtu mzuri, ana asilimia kubwa zaidi ya kuwa na kinga zaidi kwa faida za kijenetikia, na hii jenetikia yake imara huwa ina sifa ya kuwa pana sana ‘’more genetic diverse’’. na hivyo anapozaa anakuwa na uwezekano mkubwa wa kuzaa Watoto wasio wazuri, na kupelekea kuendelea kwa uwepo wa watu wengi wasio wazuri sana. Haya majibu sio ya biolojia, haya ni majibu ya nadharia za kutengeneza. Maana Biolojia inasema kuwa, Watu asilimia kubwa sana huzaliwa wakiwa wazuri kutokana na mifumo mizuri kabisa iliyowaumba mpaka wanazaliwa, lakini harakati za Maisha ndizo hutenganisha mionekano yao baadae. Hii ni kwasababu za mazingira magumu yanayoathiri matendo ya utengenezaji mzuri wa viungo vya mwonekano wa nje, mfano jua kali, vyakula visivyo vya afya, sehemu mbaya za kulala, stress, magonjwa, ajali n.k. na sasa basi, watu wengi wanaopambana zaidi hata kufanikiwa, pia wanaweza kuwa wasiwe na mionekano mizuri, na ndio huwa na nafasi nzuri zaidi ya kupata wanawake, na kumbuka matatizo haya hayatapelekea madhara kwa Watoto, na hivyo watazaliwa tena Watoto wazuri.
Na uwepo wa wazuri na wasio wazuri sana utaendelea kwa muundo huu, yaani ni kama chagua uzuri ufe, au ukane uzuri uishi na uwapatie uzuri wanao. Hoja hii ina maana kubwa sana ambayo ni hii, hakuna binadamu mwenye bahati au nguvu zaidi ya mwenzake, ila wote wanapaswa kupambana kwa akili na kufanya machaguo bora zaidi ili waweze kuishi vizuri wao, na vizazi vyao. Tukirejea kwa mashoga, Maisha hayategemei ushindani wa maliasili, Maisha yanategemea machaguo bora na ushirikiano. Ikitokea wakafa watu wote kijijini na ikabakia familia moja tu, ikiwa na mali zote za kijijini, bado haitakuwa na nafasi nzuri hata kidogo ya kuishi zaidi, maana itakosa huduma za wengine nyingi ambazo zinahitaji ushirikiano, kama familia hii itakuwa ya wakulima. Watakosa huduma za afya, huduma za usafirishaji, biashara, burudani na hata kilimo chenyewe, hawataweza kulima mazao yote. kwa hiyo mtu kuchagua kuwa shoga, atapelekea madhara makubwa zaidi maana jamii yake ingemuhitaji zaidi akiwa kama mwanaume mwenye nguvu na jeshi lake la familia, na sio kuacha maliasili ambazo zilishakuwepo.
Hoja Ya Sita
Shoo Hypothesis
Ni kinyume na maandiko ya Kiimani. Nikizungumzia zaidi Biblia. Biblia inamtambulisha Mungu katika umbile la Mwanaume. Baba ndiyo msingi wa Maisha. mzazi wa kwanza kabisa duniani alikuwa ni Baba, ambaye alikuwa ni Adamu. Adamu ndiye Baba aliyekuwa chanzo cha watu wote duniani kuanzia na mkewe Eva. kama ilivyo kwa Mungu Baba, alivyo chanzo cha watu wote ulimwenguni na kila kitu.
Unaweza jiuliza kwanini Ushoga ni hoja yenye mashiko na kushangaza zaidi kwa wanaume? Hii ni kwasababu mwanaume ndiye mzazi wa kwanza kabisa, anapoonesha kukataa asili yake anapelekea kitendawili kikubwa sana kisaikolojia. Mwanaume hata mmoja tu anavyoonesha kuwa anaweza kuwa kama mwanamke, na akaingiliwa kinyume na maumbile, anamaanisha kuwa, kila mwanaume kama yeye anaweza pia fanya hivyo, kama ataamua, maana tunafanana. hapa ndipo linapoanzia tusi na kufuru kubwa kabisa kwa kuwa, Aya za kwanza kabisa katika Biblia zinamweka Adamu aliye mwanaume kama kielelezo cha Mungu (Na tumuumbe mtu kwa mfano wetu). na ndiyo maana hata Yesu alikuja Duniani katika umbile la mwanaume. Na hata Biblia inasema ‘’nanyi wanaume wapendeni wake zenu kama vile Kristo anavyolipenda kanisa lake”. hii ni lugha ya kielelezo kilekile. Wamama wengi huumia sana wanapoona Watoto wao wakiume wanapotamani kuwa mashoga, hii inarejea katika hoja zilezile za awali.
Mungu aliweka kielelezo chake cha uwezo au Power ya uumbaji kwa mwanaume, katika namna ya kuweza kuzalisha mwanamke. Mungu alimuumba mwanaume mmoja, na kupitia mwanaume huyu, watu wote wanaendelea kuumbwa kila siku. Leo hii Mungu Muumbaji anapoona Nguvu yake ya Uumbaji wake, iliyo kwenye mbegu za kiume au sperms, inamwagwa kwenye Kinyesi. Hebu vuta picha hata ingekuwa wewe. Hebu mpatie mtu unaempenda zaidi kitu chako cha thamani zaidi kinachokutambulisha, halafu ushuhudie amekiweka kwenye kinyesi, ishara ya uchafu zaidi. je ungepata hisia gani? Hiyo inaweza kuwafungua zaidi wanasayansi wanaotumia nadharia za mabadiliko au evolution, kujua kwanini Mungu hataki mchezo kabisa wa tabia za ushoga.
Hoja za wanadini wote wanaokubaliana na kuwa, ushoga unaweza kubalika katika taasisi zao za dini kwa ajenda ya upendo. kwamba mpende hata adui yako na kuwa Yesu aliwafia wote, zimejawa na tafsiri hafifu sana za neno la Mungu, hasa kwa kutoelewa ajenda hizi zilipoanzia. Unaweza wauliza watu hawa kwa swali hili, Je, unaweza mpenda Shetani? Je, unaweza mkaribisha nyumbani kwako na kanisani kwako? Bila hata kukujibu, tayari atakuwa akisema Hapana. Na huo ndiyo ukweli, Upendo sio hisia tu, mpaka mtu atakapovua vazi lake na tabia yake ya ushoga, ndipo ambapo mtu huyo anapaswa kukaribishwa kwa upendo. la sivyo huo ni ujinga na sio upendo. hata kwetu madaktari, hatuwezi kukukaribisha tu katika wodi ya upasuaji hata tutakaporidhia akili yako, na sababu zetu za msingi, Je? Unaweza enda tu Ikulu ya Raisi unavyojisikia? Na kama hawawezi kukuruhusu je, ina maanisha kuwa hawakupendi? Iweje leo hii hoja ya upendo itumike kumaanisha kutokuwa na mipaka? Taasisi za dini za kweli haziwezi wakaribisha watu wanaosema tuna mabomu, na tunayaripua muda wote ndani yao. Maana hao wanakubali jiua ili hali Biblia imeandika, watu wangu wanaangamia (wanajiua) kwa kukosa maarifa (ujinga wa kutokuwa na mipaka).
Hoja Ya Saba
Namna Ya Kuwasaidia Mashoga Kwa Upendo
Wanaume wengi wenye changamoto za maendeleo ya kijinsia, hata kuishia na kuwa na sifa kadhaa za kike, na kupungukiwa Sifa za kiume. wanapaswa kwanza kuondokana na mitazamo hasi kuwa wao ni mashoga, (kumaanisha wanapaswa kufanywa kama wake). bali wanapaswa kuichukulia hiyo hali kama ilivyo hali kwa magonjwa mengine mengi sana ya shida katika mifumo ya kijinsia. Wanapaswa kuishi tu katika Maisha ya kawaida huku wakijizuia kuvuka mipaka, ambayo ni kujidanganya na kuwadanganya watu kuwa, wanatamani kuingiliwa kinyume na maumbile kwa sababu za kibiolojia. hilo ni kosa kubwa sana. (kumbuka mpaka sasa yapo magonjwa mengi sana yanayohusiana na changamoto za kutofanikiwa kifasaha kwa uumbaji wa kijinsia, na muda mwingine wapo hata mapacha ambao huungana wa jinsia tofauti) kwa hiyo haya yote yanapaswa kupokewa kama magonjwa, au changamoto, na sio kama aina Fulani ya uumbaji ulio special. Na kwa wale wanaume walio wazima wa afya kabisa lakini kwa akili zao binafsi na shida za kisaikolojia wanazoweza wasizijue wao, na wataalamu wao, mpaka wanaamua kutamani, na kuwafanya wenzao kinyume na maumbile yao, wanajitengenezea hatari zitakazo warudia wao wenyewe hapa duniani, na huko mbinguni.
Ufupisho
Jinsia sio kitu chepesi chepesi tu kuweza kuundwa. Jinsia zote ni matokeo ya mifumo mingi sana ambayo imeshawekwa tayari miaka mingi sana tangia asili ya binadamu wa kwanza kabisa. Hakuna jinsia iliyo rahisi wala hakuna namna ya kuweza kuongeza chochote katika asili ya biolojia hizi pana, ila ipo nafasi ya kuharibu.
Wataalamu wa Biolojia ambao wana teknolojia ya kuweza kuchagua jinsia Fulani, dhidi ya jinsia nyingine, katika hatua za awali kabisa za uundwaji wa mimba. aidha kupitia kuchagua mbegu za jinsi moja kama X, au Y, ili kuunda Watoto wa kike au kiume. Wataalamu hawa na hata wale ambao wanaweza tengeneza mazingira ya uundwaji Watoto wengi, na kisha kuwaua wa jinsia wasizozihitaji ili kulenga kupata jinsia moja tu, na hata wale ambao hutumia mbinu za asili katika kulenga kupata Watoto wa jinsia Fulani tu. Hawa wote hawaamui jinsia ya kiume au ya kike, ila wanatengeneza tu uwezekano zaidi wa jinsia Fulani, kama ambavyo tumeshaona hata jenetikia, ni sehemu ndogo sana katika kuamua jinsia Fulani. hakuna anayejua mtambo mzima wa uundaji unavyofanya kazi. sisi tunaona tu yanayoendelea, japokuwa tuna nafasi ya kusababisha madhara kama ilivyo kawaida ya wataalamu wengi wasiozingatia misingi ya asili, na kuiheshimu, ijapokuwa wao hawakuathiriwa. Unaweza jiuliza, ni kwanini? ni rahisi kumdhuru mtoto aliye tumboni kirahisi sana, lakini je, ungefanyiwa wewe ingekuwaje.
Unapokuwa mwanamke au mwanaume, kuna sababu za msingi sana zilizo nyuma ya kwanini una jinsia hiyo, na jinsia ni kama cheo, lazima uitendee kazi, au la sivyo itakudai. maana tayari kuna kazi kubwa sana imeshafanywa hata umeipata hiyo jinsia. Lakini unapaswa sana kuitunza jinsia yako, maana ni matokeo ya kazi na akili nyingi sana iliyotumika katika kukuumba. huku ikipambana dhidi ya maelfu ya hatari ambazo zingeweza kukutokea, ikiwemo na hatari kama za kuweza kuzaliwa ukiwa na mapungufu baadhi ya kijinsia. Na utambuzi huu utamsaidia msomaji kuwapenda na kuwajali wenzetu wenye mapungufu kama tuliowazungumzia katika sehemu ya juu. maana hawakupenda kuzaliwa wakiwa na madhaifu. ila ni mfululizo tu wa matatizo kama yalivyoruhusiwa kutokea katika sayari yetu ya dunia.
Mungu ndiye anaeamua jinsia zetu, na tunapaswa kuishi kwa kuziheshimu. hasa kwa kuishi Maisha yanayopaswa. Kumbuka seli zetu zinaonesha Ushahidi wa uwezo wa uumbaji ambao ni zaidi ya chembechembe zilizopo pale, na hii ndio Sababu ya msingi kabisa ya kuhitimisha na ujumbe huu katika mwisho wa sura ya kwanza.
Mwandishi na Mwenyekiti
Mtaalamu wa sayansi ya wanyama, mwanabiofizikia, na mwandishi wa vitabu vya kisayansi. Mwanzilishi wa Injili ya Sayansi — taasisi inayounganisha maarifa ya kisayansi na imani.
Shiriki makala hii
13 min
3 min
4 min