Inapakia...
Inapakia...

Dr Brighton Shoo
Mwandishi na Mwenyekiti
“SUKARI ZA KISASA ‘’Artificial sweeteners’’ Soko la vyakula linahitaji sana bidhaa za sukari kama nilivyo elezea katika sura iliyopita. Na pia, miili yetu inahitaji na kupenda sana sukari kama nilivyoe…”
SUKARI ZA KISASA ‘’Artificial sweeteners’’
Soko la vyakula linahitaji sana bidhaa za sukari kama nilivyo elezea katika sura iliyopita. Na pia, miili yetu inahitaji na kupenda sana sukari kama nilivyoelezea katika sura zilizopita. Katika uzalishaji wa bidhaa za sukari, kiwango kikubwa sana cha sukari katika aidha juisi au vitafunwa ni hatari sana. Hii ni kutokana na kuwa, kama watu watakuwa watumiaji sana wa sukari ya asili, yaani ‘’sucrose’’. Basi kuna asilimia kubwa sana ya kupata matatizo ya vitambi ‘’obesity’’ ambayo ni kutokana na kuwa, sukari inapokuwa nyingi mwilini zaidi ya inayohitajika, hubadilishwa iwe mafuta. Na haya mafuta, huambatana na changamoto nyingi za kiafya. ikiwemo matatizo ya moyo na presha, hii ni kwasababu ya uwepo wa kiwango kikubwa cha mafuta, katika mishipa ya damu, kiasi cha kufanya presha ya damu iwe kubwa kutokana na matundu madogo ya kupitisha damu.
Sukari isiyo tumika mwilini hubadilishwa kwa matumizi mengine, na huko ndiko kunakoleta changamoto. matatizo ya sukari nyingi mwilini ni mengi sana, hasa kutokana na kuwa, sukari hupunguza ufanisi wa utendaji kazi wa tishu, na seli mbalimbali kadri inapozidi kubadilishwa kuwa aina nyingine ya kemikali. Mabadiliko ya sukari aidha kuwa mafuta, au chembechembe zinazoitwa ‘’glycogen’’ ambazo huwa zikitunzwa katika ini, huambatana na mabadiliko ya kihomoni, ambayo kadri yanavyozidi kubadilika badilika yanaathiri ufanisi wa mifumo ya homoni.
Kuikimbia hii adha, namna nyepesi ya kisayansi ya kuepuka ni kupitia kutafuta mbadala wa hizi sukari za asili, lakini bado tukiwa tunahitaji Ladha ya sukari. Na hapo ndipo ilipoibuka mbinu mbadala nzuri kabisa ya kutumia sukari za kisasa, au ‘’artificial sweeteners’’.
SUKARI ZA KISASA ‘’artificial sweeteners’’.
Hizi sio sukari au jamii ya wanga. Nyingi zake ni protini. Hizi huwa ni protini lakini huwa na Ladha ya utamu kuliko hata sukari yenyewe. Hizi zipo za aina nyingi sana. Na zilizo maarufu zaidi ni ‘’Aspartame’’. hizi ni protini ila zina Ladha kama ya sukari. Na kwa mantiki hiyo, mtu kama atatumia atahisi kana kwamba amelamba au amekunywa sukari, lakini kumbe ni protini au ‘’amino acid’’.
Kwa mfano aspartame ambayo ndiyo inapatikana kwa kiwango kikubwa sana. Yenyewe imeundwa kwa muunganiko wa amino acids mbili, zinazoitwa ‘’phenylalanine na nyingine ni aspartic acid’’. Na aspartame ina utamu mara 200 zaidi ya utamu wa sukari. Kwa hiyo watu wengi hupendelea sana aspartame, kwa kuwa ina utamu kama sukari, lakini siyo sukari. na kwa hivyo, hata mraibu wa sukari, anaweza kuridhika kwa matumizi ya sukari hii ya kisasa. na tena bila kuathiriwa na madhara yale ya sukari tuliyokwisha yaona. Hebu tazama siyo aspartame tu zipo na protini na kemikali nyingine nyingi mbadala wa sukari, tena tamu kuliko sukari.
Unaweza ona hiyo kemikali neotame, ni tamu mara mpaka elfu kumi na tatu zaidi ya sukari.
‘’artificial sweeteners’’ kama vile Aspartame.
Wajanja sana. Tatizo ambalo wengi hulijadili juu ya madhara ya utumiaji wa hizi sukari za kisasa, ni juu ya uhatarishi wake wa kusababisha saratani au cancer. Na mara nyingi, tafiti huwa zinafanywa kwa kuwajaribisha panya. kwa kuwawekea viwango kadha wa kadha vya hizi sukari za kisasa, na inapotokea kukawa na utokeaji wa visababisha cancer vingi. ‘’carcinogens’’. basi hiyo sukari ya kisasa huzuiwa kutumika kwa watu. Lakini pia, panya ambao hupewa hizi sukari za kisasa, huchunguzwa kiwango chao cha sukari ndani ya mwili, pia huangaliwa hata homoni kadhaa, na mabadiliko mengine.
Kwa mfano wa kemikali ya Aspartame ambayo ni protini inayoundwa na Phenyalanine na Aspartic acid, basi wapinzani wengi wa utumiaji wa sukari hizi za kisasa, hujikita katika kuzungumzia madhara ya kiwango kikubwa cha ‘’Phenylalanine’’ ndani ya mwili, baada ya aspartame kuvunjwa vunjwa katika mwili. Hii ni kwasababu kwa kawaida, mwili huwa hauwi na kiwango kikubwa cha amino acids za phenylalanine, kama zinazokuwepo kama mtu atatumia sukari hizi za kisasa. Na wateteaji huwa na Ushahidi mwingi sana wa ya kuwa, phenylalanine haina madhara yenye kuleta maana yoyote ile kwa viumbe. ‘’insignificant findings’’.
Na pia wateteaji husema hata kiwango cha sukari ya kisasa wanayo itumia wakosoaji katika tafiti zao, ni kikubwa sana kuweza hata kupelekea matokeo wanayoyaona. ukilinganisha na kiwango anacho kitumia mtu mmoja mmoja. Na mjumuisho wa sababu hizi umepelekea nchi kadhaa zikiongozwa na Marekani, mashirika yake ya ubora wa chakula na dawa, yaani FDA. Kuruhusu matumizi ya sukari hizi za kisasa. Na kama mtu mmoja ataingia mitandaoni, atakutana na taarifa nyingi sana za kutetea ubora wa matumizi ya sukari hizi za kisasa, kuliko hata kukutana na taarifa za lawama. Na pia, hata kama mtu mmoja atakutana na lawama juu ya madhara ya matatizo ya utumiaji wa sukari za kisasa, basi kuna hatihati ni madhara feki. Hebu tazama taarifa moja hapa chini.
Taarifa za mtindo huu, ambazo zinathibitisha kuwa Aspartame ambayo ndiyo sukari ya kisasa maarufu kabisa, kuwa haina shida. ndizo zilizo sambaa zaidi.lakini jiulize swali moja kwanini hawajiamini?
USHAHIDI WA TAFITI ZA KISAYANSI JUU YA MADHARA YA SUKARI ZA KISASA
Utafiti uliofanywa na (NIH/NCBI 2011 Oct 21 juu ya sukari za kisasa ‘’artificial sweeteners) na nukuu kauli moja ‘’Bado matokeo ya umeng’enyaji wa bidhaa hizi za sukari za kisasa, una mkanganyiko mkubwa ‘’controversial effects’’ katika afya na matendo ya kibiolojia ya mwili’’metabolic effects’’. Na katika tafiti zao, hawa wanasayansi wakuaminika sana, ambao ulichambua aina kadhaa za sukari za kisasa, unaonesha kuwa, aspartame inatia mashaka bado juu ya hatarishi za madhara ya ongezeko la Phenylalalnine, Methanol, na visababisha saratani ‘’carcinogen’’. Sucralose ilionekana kuwa na hatarishi za shida za figo, Saccharins ilionesha hatarishi ya hatari katika matendo ya kibiolojia ya mwili ‘’metabolism’’ na visababishi vya saratani, Cyclamate ambayo hata marekani imezuiliwa ilionesha bado inahitaji utafiti zaidi, Neotame ilionesha pia kuwa na madhara japo kidogo kutokana na matendo yake ya kibiolojia.n.k
Nukuu pia ya Utafiti uliofanywa na Joanna Foley,RD,CLT. 2023July,20 na kupitiwa na Patricia Pinto Garcia MD,MPH. tafiti hii ilijumuisha na matokeo ya tafiti nyingine kadhaa ambazo nitaweka reference zake mwishoni, ilionyesha. Upo mgogoro juu ya Utokeaji wa saratani, na magonjwa ya moyo, kutokana na matumizi ya sukari za kisasa. Lakini hakuna mgogoro wa matokeo yafuatayo juu ya utumiaji wa bidhaa za sukari za kisasa ‘’artificial sweeteners’’.
1.Kuongezeka kwa hamu, hasa kwa watumiaji wa aspartame. Na hii ni kawaida sana, hata katika jamii zetu wazoefu wa unywaji wa soda, huwa na hamu sana ya kuendelea kuzitumia. Mfano watumiaji wa Coke products.
2.Ongezeko la Uzito. Watumiaji wa sukari za kisasa kwa muda mrefu, hata kwa wale wazazi wanaowazoesha Watoto wao tangia wakiwa wadogo, matokeo yake watumiaji huwa wakiwa na mafuta mengi mwilini na hata BMI ya mwili huongezeka.
3.Mwongozo mbaya wa uongozaji wa sukari katika damu. ‘’poor regulation of blood sugar’’. Utafiti unaonesha ya kuwa, ijapokuwa sukari za kisasa haziongezi zenyewe sukari, ila kuna Ushahidi wa kuongezeka kwa kiwango cha homoni ya Insulin katika damu. Na Ushahidi huu umekwisha onekana kwa watafiti wengi.na tafiti imejaribu kuhisi wenda Kongosho au Pancrease, inaweza kosea kwa kuichanganya na sukari.na pia imeonesha kuna uhusiano wa muda mrefu, kati ya sukari ya kisasa, na ukinzani wa insulin ‘’insulin resistance’’ au kisukari (type 2-Diabetes).
4.Pia tafiti imeona kuna uhusiano wa utumiaji wa sukari za kisasa, na ongezeko la hatari ya Kushuka ghafla kwa sukari ya mwili. ‘’Reactive Hypoglycemia’’.
5.Kuathiri mfumo wa bakteria wanaosaidia kumeng’enya chakula tumboni. ‘’Alteration of Gut microbiome’’. Kwa kawaida, katika mfumo wetu wa chakula huwa kuna baadhi ya bakteria ambao huwa tunaishi nao, na hawa huwa wanasaidia katika umeng’enyaji zaidi wa chakula tunachokula. Sasa basi, unapotumia sukari za kisasa au ‘’artificial sweeteners’’. basi unawadhuru hawa bakteria wenye faida, na sukari za ‘’Saccharins na Sucralose’’ ndizo zilizoonekana zaidi kuleta haya madhara.
6.Ongezeko la uwezekano wa kupata shida ya moyo, au Stroke. Hii ilichapishwa na shirika la ‘’American heart association’’.
7.Ongezeko la uwezekano wa kupata changamoto za matatizo ya matendo ya kibiolojia ya mwili. Au yanaitwa ‘’metabolic syndrome’’. Utafiti unaonyesha, matumizi ya sukari za kisasa yanaambatana moja kwa moja na kulimbikizana kwa mafuta ‘’fat deposits’’, kiwango kikubwa cha chembechembe za mafuta ya Triglyceridedes’’, na kupungua kwa chembe za mafuta ya HDL cholesterol. ambapo haikupaswa kuwa hivyo. Hii hupelekea ongezeko la presha ya damu na sukari ya damu.
Pia tafiti zinaonesha ya kuwa, zipo faida kadhaa za utumiaji wa sukari hizi za kisasa, na hasa! Ni kuwa hazina kiwango kikubwa cha wanga ‘’calories’’. haziongezi kiwango cha sukari katika damu. Pia zinasaidia kujikinga na matatizo ya meno. Ambayo yamekuwa yakisababishwa zaidi na ulaji wa sukari.lakini huwezi acha ukweli kuwa, kama kuna mafanikio makubwa zaidi ya sukari za kisasa, basi ni utamu wake.
TATIZO HALISI LA KUDANGANYA ULIMI NA NDIYO HATARI KUU ZAIDI YA HIZI SUKARI
Ubongo unatumia kiwango kikubwa sana cha sukari ukilinganisha na kiungo kingine chochote kile. Hii inatokana na kazi zake. Hata wakati ambapo viungo vyote vya mwili vinapolala, ubongo bado huwa unakuwa kazini au active. matumizi ya sukari katika ubongo huongezeka zaidi kipindi cha kazi za kufikirisha, kuliko kazi za kawaida. Tabia na mapenzi yetu ni matokeo ya ubongo wetu.
Ubongo sio kama kompyuta yenye teknolojia ndogo sana. Ubongo sio kama roboti kama Chat GPT. Ubongo huwezi ulinganisha uwezo wake. Ubongo ni mtambo complex zaidi katika ulimwengu. Bado dunia haijashuhudia ufundi mkubwa zaidi ya teknolojia ya ubongo. Lengo hasa la kupotosha milango ya fahamu limejikita katika kuua mtambo huu wa ubongo.
Kabla hatujaenda zaidi kwenye lengo kuu, ni muhimu msomaji kutambua ya kuwa, kiwango cha sukari katika ubongo nacho kipo katika utaratibu maalumu. Na ndiyo maana, hata takwimu zitakwambia ubongo hutumia asilimia 20-22% ya sukari yote ya mwili. tena peke yake. tena zaidi ya kiungo chochote kile. Kutokidhi mahitaji haya kunaweza leta changamoto nyingi sana. hasa juu ya zile kazi zote za upekee za ubongo, zinazomtambulisha mtu ni nani.
SAYANSI YA KUUDANGANYA UBONGO KUPITIA SUKARI ZA KISASA
Ubongo hauitambui sukari ya kisasa. Sukari ya kisasa au ‘’artificial sweetener’’ zinapofika katika seli za kuhisi katika ulimi, hasa zile za sukari tulizokuwa tukiziita (T1R2/T1R3). huzisisimua tena kwa kiwango kikubwa sana kushinda hata sukari yenyewe. Na Ubongo kama tulivyouona kuwa mara zote huusianisha kiwango cha sukari na hitaji la nishati. Kitendo cha msisimko wa sukari ya kisasa kuwa mkubwa katika seli hii ya kuhisi, basi ubongo huamini kuna sukari nyingi sana. Na madhara yake husababisha ubongo kutenda kama vile ambavyo huwa ukitenda sukari inapokuwa nyingi sana. Lakini kumbe, huyu mtu amekula tu protini au amino acids.
Chini nitaonesha tafiti mbali mbali zinavyokubaliana na ukweli huu unaoumiza sana dunia. Watu wengi wamejikita kutafuta matatizo ya sukari za kisasa katika kundi la matokeo madogo madogo kama vile saratani, tatizo la uzito, hamu za kula n.k.
Kwanini tatizo hili halionekani?
Kwa kawaida watu huona tatizo katika gari lililosimama lisiweze kutembea zaidi. lakini ni vigumu kutambua tatizo kwa gari linaloenda lisijue linaenda wapi, au linaendaje endaje? Ni rahisi kuona matatizo kwa mtu aliye kilema, kwa kuwa unauona mguu ni mmoja tu. Lakini ni vigumu sana kuona tatizo kwa mgonjwa wa akili, kwasababu tu anaweza cheka na kulia kama wengine. Hebu tutazame matokeo ya tafiti zifuatazo kabla hatujaliangalia tatizo kwa undani zaidi.
MATOKEO YA KUATHIRI UBONGO KUPITIA SUKARI ZA KISASA KAMA SODA
Utafiti wa 1 uliofanywa na (Nutrients | Free Full-Text | Daily Early-Life Exposures to Diet Soda and Aspartame Are Associated with Autism in Males: A Case-Control Study, n.d.)
Huu utafiti ulibaini matumizi ya soda za diet ,matumizi ya sukari za kisasa ‘’aspartame’’ za kama kwenye Coca cola. zinaambatana na hatari za kutokea kwa tatizo la usonji ‘’autism’’. yaani mtoto anazaliwa akiwa anashida ya akili, hata hawezi kujamiiana na wenzake na kukua vizuri. Katika tafiti zao waligundua yafuatayo kuhusiana na matumizi ya sukari za kisasa.
kutokana na viwango vya aspartic acid kutoka kwenye aspartame, basi kuna madhara yafuatayo.
1.mhemko mkubwa unaosababishwa na sumu, kwenye seli za ubongo ‘’excitotoxicity’’ na ongezeko la sumu katika ubongo.
2.madhara makubwa katika mfumo wa ubongo, wa kujikinga na sumu zinazosababisha kuisha kwa seli. kupitia tendo la ‘’oxidative stress’’.na mfumo huu wa ubongo wa kujilinda unaoathiriwa, unahusisha kemikali nyingi sana za muhimu za ndani ya ubongo, kama (genes za ocm, au one carbon metabolism, kupungua kwa enzyme inayoitwa ‘’glutathione’’, ambayo husaidia sana kujikinga sana na madhara ya sumu zinazotokana na mabaki ya matendo ya kibiolojia, ‘’major anti-oxidant’’, kuathiriwa kwa methionine cycle, na folate cycle, na transsulfuration pathways. Matendo haya yote ni ya ulinzi mkubwa wa ubongo, yote huathiriwa kwa kutumia sukari za kisasa)
3.kufeli kwa seli za kuzalisha nishati ‘’mitochondrial dysfunction’’. Unapotumia sukari za kisasa.
4.kuongezeka kwa udhaifu wa kujikinga dhidi ya sumu, na kuisha kwa uwezo wa seli za ubongo. ‘’oxidative stress’’.
Kutokana na viwango vikubwa vya phenylalanine kuliko vilivyo standard katika ubongo, hupelekea madhara yafuatayo.
1.kuathiri kiwango cha vitoa taarifa vya ubongo, na homoni za ubongo au niziite ‘’neurotransmitters’’. Hii ni sawa na kusema, hata homoni ambazo huwa ndo zinakufanya wewe ufurahi, au ufanye maamuzi yoyote, hata ya hasira au woga. mfumo huu wote nao huathiriwa.
2.kuathiri mfumo wa ubongo unaowasiliana na mfumo wa chakula, na hisia, na utambuzi kwa Pamoja. na unahusiana pia na mifumo mingine midogo ya fahamu. Hii pia huitwa ‘’microbiome gut brain axis)
3.Ongezeko la asidi inayoitwa ‘’proprionate’’. na hii huambatana na tatizo la kushindwa kubalansi Maisha ya bakteria wazuri wa tumboni. ‘’dysbiosis of gut microbiota’’. Na matokeo yake ni ongezeko zaidi la sumu kwa seli za ubongo, au ‘’neurons’’ Kila unapotumia sukari za kisasa.
4. Hudhoofisha Mfumo wa chakula, kuruhusu vitu vipite kuingia sehemu zingine. au ‘’leaky gut’’. Na hii huambatana na kuongezeka kwa upitishwaji wa vitu hatarishi, katika geti kuu la ubongo. linaloitwa BBB au ‘’Blood Brain Barrier’’.
Uwepo wa Methanol inayopelekea kuzalishwa kwa Formaldehyde na formic acid, huchochea zaidi madhara yote tuliyoyaeleza hapo unapokula vyakula vyenye hizi artificial sweeteners, au sukari za kisasa.
Kwa Pamoja hayo ni sawa na kusema, husababisha madhara makubwa ya sumu ‘’excitotoxic damage’’, madhara ya sumu za asidi ‘’lipid peroxidation’’, kuvimba kwa seli za ubongo ‘’neuroinflammmation’’, kuathiri mfumo wa uhusiano wa ubongo-mfumo wa chakula-hisia-utambuzi-mifumo mingine ya ufahamu.’’microbial-gut-brain axis. Haya yote huathiri ufanisi wa seli za ubongo ,kazi na Maisha kwa ujumla.
Picha ya sura za mbele za tafiti mbili nilizokuwa nikizizungumzia hebu tuendelee kuangalia zaidi.
UTAFITI:SUKARI ZA KISASA ZINAVYOHARIBU MFUMO WA UBONGO
(Arbind Kumar Choudhary & Yeong Yeh Lee (2017): Neurophysiological symptoms and aspartame: What is the connection? Nutritional Neuroscience, DOI:
Hawa wanaanza kutoa utangulizi kuwa, unapokula sukari za kisasa, ambazo hasa zina hizi ‘’aspartame’’ zilizojaa kwenye bidhaa za viwandani. Hii aspartame huvunjwa kwenye utumbo kwa asilimia 50% kuwa phenylalanine, kisha 40% kuwa aspartic acid na asilimia 10% kuwa methanol. Methanol huvunjwa zaidi kuwa Formaldehyde na formic acid. Kadri unavyokula sana bidhaa hizi ndivyo hizi kemikali zinapozalishwa zaidi.
Phenylalanine na aspartic acid huvuka geti la ubongo linaloitwa BBB au ‘’blood brain barrier’’. Zikishaingia kwenye ubongo hupunguza uzalishaji wa homoni za ubongo zinazoitwa Catecholamines. Hizi catecholamines ni homoni za msingi sana katika ubongo ambazo huusisha homoni inayoitwa ‘’Dopamine na Serotonin’’. homoni hizi huusiana na hali za kiakili kama mood ‘’. hii ni ile hali ya unajisikiaje!’’. motivation ‘’hii ni hali ya kuwa na motisha ya kufanya kitu”. Na pia furaha. Na hii ipo hivi. ‘’kwa kawaida serotonin huitwa homoni ya furaha au happy homoni, au hali ya kutulia. Kwa hiyo hali hizi zote huathiriwa baada ya mtu kutuimia kemikali hizi. Pia Aspartic acid huusiana na kuharibika kwa seli za usaidizi wa seli za ubongo ‘’astrocytes’’na pia huaribu seli za ubongo ‘’neurons’’.
Hawa waligundua pia kuwa, kemikali hizi za sukari za kisasa zenye aspartame, huweza kupunguza kiwango cha homoni ya ubongo ya furaha ‘’serotonin’’ kwa kuzuia au kublock wasafirishaji kwenye ubongo, wanaoitwa ‘’NAAT’’. ambao hao ndiyo msingi wa ujenzi wa protini au amino acids za ubongo. Na protini zinazoathiriwa kuundwa katika ubongo zinaitwa ‘’Tryptophan na Tyrosine’’. protini hizi ni za muhimu sana kwa ufanyaji kazi wa mfumo wote wa akili ya hiari ‘’voluntary’’ na isiyo ya hiari’’non voluntary’’. Kiwango kikubwa cha Aspartic acid, baada ya kula mfano pipi, hubadilishwa kuwa Glutamate kupitia seli zinazoitwa ‘’astrocytes’’.
Na kiwango hiki kikubwa cha Glutamate, huelekea kwenye sensa au receptors muhimu sana za ubongo zinazoitwa ‘’NMDA’’ au ‘’N-methyl-D-aspartate’’. na pia huenda kwenye sensa zingine za ubongo zinazoitwa mGluRs au ‘’metabotropic glutamate receptors’’. Na huku zikifika, husababisha yafuatayo. huzuia seli za ubongo ‘’astrocytes’’ kuchukua zaidi homoni glutamate kwenye visafirishaji vya ubongo vinavyoitwa EAAT au ‘��excitatory amino acid transporter’’. Pili, hutoa nje glutamate kwenye seli. hiki kitendo huitwa pia ‘’exocytosis’’. na husababishwa na ongezeko la ‘’Calcium’’ ndani ya seli, kutokana na kusisimuliwa kwa zile receptors nilizoziita ‘’mGluRs kwenye seli za ubongo ‘’astrocytes’’. Na haya hupelekea misisimko zaidi ya viwango vya seli za ubongo, au ‘’hyperexcitability of neurons’’.
SUKARI ZA KISASA KATIKA AFYA YA UBONGO
1.Kufa kwa seli za ubongo. Hasa ukizingatia seli zinazoathiriwa pia ni astrocytes, ambazo ni walinzi na pia ni seli za ubongo.
2.Maumivu ya kichwa tofauti tofauti. Huitwa pia headaches. lakini kuna aina ya kipekee ya maumivu ya kichwa ambayo inaitwa ‘’Migraines’’. Na haya ni maumivu ambayo huwa ni ngumu sana kutambua chanzo chake, mara nyingi hupotea yenyewe baada ya muda, ila pia huweza kuambatana na matatizo makubwa zaidi.
3.matatizo ya kuona.
4.kusikia sauti masikioni mfululizo ‘’tinnitus’’. Najua unatambua kuwa hata kukiwa hakuna kelele, bado ubongo wako huwa unaisikia sauti ndogo sana toka kwenye masikio yako, na sasa basi, Sauti ile inapokithiri huwa ni tatizo linaloitwa ‘’tinnitus’’.
5.Shock za ubongo, hivi huwa ni vipindi vya mhemko mfanano wa ugonjwa wa kifafa. Huitwa ‘’seizure’’.
6. N.k..
Mwandishi na Mwenyekiti
Mtaalamu wa sayansi ya wanyama, mwanabiofizikia, na mwandishi wa vitabu vya kisayansi. Mwanzilishi wa Injili ya Sayansi — taasisi inayounganisha maarifa ya kisayansi na imani.
Shiriki makala hii
15 min
128 min