Inapakia...
Inapakia...
Uchambuzi Sahihi wa Kifalsafa na Kiteolojia
Injili ya Sayansi inaamini katika uchambuzi sahihi wa mada za kifalsafa, na kiteolojia, kupitia kwa wanachama wake wenye msingi mpana wa kifalsafa na kiteolojia.
Ndani ya Injili ya Sayansi wapo wachungaji kadhaa kutoka imani tofauti tofauti. Katika Injili ya Sayansi tunaamini katika Biblia kama isemavyo, na kama ijitafsirivyo yenyewe.
Bado asilimia kubwa ya watu wanakumbwa na changamoto zinazotokana na mitazamo yao ya kiimani. Tunalenga kuwaongoza kwa ukweli.
Masomo yanayounda msingi wa teolojia na falsafa katika Injili ya Sayansi
Kujifunza na kuelewa Biblia kama inavyojitafsiri yenyewe bila kutegemea dhana za wanadamu
Soma ZaidiKutathmini mafundisho ya kifalsafa kwa kutumia mantiki ya msingi na ukweli wa maadili
Soma ZaidiKufanya kazi na waumini wote wanaoamini katika Mungu na wanaokemea uovu
Soma ZaidiInjili ya Sayansi inashirikiana na waumini wote wanaoamini katika Mungu na sayansi. Tunakubaliana na masomo yote ya kiimani yanayokemea uovu na kuhamasisha upendo. Tunajikita katika sera za ukweli, sio uhuru wa kifalsafa.
Nguzo nne zinazojenga msingi wa teolojia na falsafa katika taasisi
Wapo wachungaji wengi na wasomi kutoka imani tofauti tofauti ambao tunashirikiana nao kufundisha ukweli wa Biblia na kukemea uovu.
Wapo wanafalsafa wengi sana ambao Injili ya Sayansi inakubaliana nao, na masomo yao huwasilishwa na wanachama kadhaa, ikiwemo Ernest B Jonass.
Masomo yetu yanajenga msingi wa kukubaliana na changamoto mbalimbali za kimaisha, na pia yanahamasisha hisia za asili za kiume, au za kike.
Tunakinzana na wanafalsafa wanaokinzana na msingi wa kweli wa ubinadamu, na kimaadili. Tunakemea kila namna ya falsafa inayoshutumu uovu.
Katika sehemu ya vitabu na nakala, masomo mbalimbali yanapatikana kulingana na asili yake, kama ni teknolojia na uchumi, au sayansi za afya, au teolojia na falsafa. Tunalenga kuwawezesha watu kuwa na uelewa sahihi wa Biblia na falsafa inayokubaliana na ukweli.
Masomo ya kibiblia na tafsiri sahihi
Uchambuzi wa kifalsafa na kiteolojia
Ushirikiano kati ya madhehebu mbalimbali
Mwongozo wa kiroho na kimaadili
Vitabu na makala za kiteolojia na kifalsafa
Laboratory Technologist — MUST Mbeya
Augustino Joseph Mrombo ni mtumishi wa Mungu wa kanisa la Waadventista Wasabato. Pia ni Laboratory Technologist aliyehitimu masomo yake mwaka 2022 kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).
Kwa Augustino, Injili ni sayansi inayogusa nyanja zote ulimwenguni. Injili ni tiba ya mwili na roho. Sayansi ya dunia peke yake ina mipaka, lakini sayansi ya Injili haina kipingamizi chochote. Injili inaponya kila kitu.
Augustino ni mwanachama wa Injili ya Sayansi ambaye anatumia muda wake mwingi sana kutoa masomo katika jamii kupitia uandishi wa vitabu. Pia hutumia mtandao wa YouTube kwa account yake ya "Neno Lenye Nguvu" kuwasilisha masomo yake ambayo yamejikita kutoa nuru ya ukweli, kupitia maandiko na taaluma yake ya sayansi.
Msaada wake mkubwa katika kuelimisha watu kuhusu ukweli wa Biblia na sayansi ni wa thamani kubwa kwa Injili ya Sayansi.
Pata elimu ya kiroho na uchambuzi sahihi wa kifalsafa kutoka kwa wataalamu wetu.